Sura Ya Sita

8 0 0
                                    

Ilikuwa karamu ambayo  katu haingekatika ila kwa shoka!

Msomi Bi.Arusi;Demathew Bw.Arusi.

Msomi alikuwa anafunga ndoa na mpenzi wake mzungu,mweupe pepepe!

Mrefu kasoro twiga!

Mpenzi aliyekuwa amekutakana naye kule Uholanzi,alipokuwa amehudhuria kongamano la wachoraji wabunifu wa miundo msingi.

Sifa za Msomi zilikuwa zimemrusha juu na kumtusha Uholanzi.

Mabawa yake alikuwa ndo mwanzo kayapanulia ulimwengu mzima!

Mvuto kati ya Msomi na Damata,kama alivyokuwa akimwita Mzee Moja;ulikuwa ule wa smaku na chuma.

Mvuto wenye nguvu na mnato usioweza kutengenishwa.

Damata alikuwa jamaa mrefu, mwenye misuli na tabasamu la kumtoa nyoka pangoni;kisha kumzubaisha akabebwa hobelahobela,makali kamtoka,mnyonge mikononi mwa nyani!

Bila kupangwa,waliketi bako kwa bako,ndani ya ukumbi wa mkutano.

Au labda kwa kupanga mwenyewe Maulana!

Wakawa hawana budi kuzungumziana,hasa pale mmoja wepo wa wazungumzaji alipowaomba kujumuika wawili wawili kwa ajili ya zoezi.

"Mwanamke kwa mwanaume ili waingie katika safina la Noa,mithili ya viumbe,wakati wa mafuriko ya kusafishia dhambi duniani",kwa utani,msemaji  aliwaomba wanakongomano.

Baada ya kicheko,Msomi alimgeukia Damata,huku akimnyooshea mkono.

"Hi,am Musomi,an archtect from Africa!"

Mkono wa Damata ulinatana na ule  Msomi.

Kwa butwaa,aliitikia;"Am DeMathew from Netherlands,pleasure to meet you"

Kwa muda wa sekunde,au pengine dakika kadhaa,Damata alimtazama  Msomi kwa macho makavu, maneno kamkwama mdomoni.

Akabaki tu kuutingiza mkono wa Musomi,nusra kuung'oa.

Alipogutuka alimwachilia na kumuomba msamaha.

Maskini,smaku ya mapenzi ilimpumbaza asibanduke wala kusema.

Wala tusingemalaumu!

Msomi livalia Rinda la aina ya kitenge.

Rinda lililomgandama na kuwacha umbo lake la chupa,likionekana kama sanamu.

Sanamu iliyochongwa na Maulana mwenyewe pasipo haraka wala tashwishi.

Mikononi alijivalia bangili zilizotengenezwa kwa pembe za ndovu au pengine kwa meno ya simba;kwa jinsi zilivyokuwa za dhamani.

Shingoni alivalia mkufu wa kimaasai,wenye kumetameta kama nyota wakati wa giza totoro.

Masikioni palining'ing'inia pete ziliundwa kwa miti ya thamani kutokea Kongo.

Miguuni alivalia bangili zenye rangi mchanganyiko.

Rangi zilizomfanya kuonekana kama upinde wa mvua kwa kupendeza.

Miguuni alikanyagia viatu vya kamba kutokea masaini.

Damata alivalia suti ya samawati iliyomkaa na kuonekana kana kwamba alizaliwa nayo.

Ilishikamana na ngozi yake na kumpatia umaridadi wa kipendee.

Suti ilikuwa imemkubali!

Baada ya semezana na kujuliana hali,walijikita katika mazoezi ya kongamano,wakionekana kama marafiki waliofahamikiana kwa siku nyingi.

Marafiki waliosoma pamaja na kukulia pamoja.

Na hii ikawa ndio lele ya ngoma  ya mapenzi yao kuisakata.

HIMAYA YA MZEE MOJATempat cerita menjadi hidup. Temukan sekarang