SIRI

4 1 0
                                    

Ilikuwa ni siku ambayo nchi nzima ilikesha mitandaoni, kila mwenye simu janja aliweka bando ili kuhakikisha kilichokuwa kikiendelea. Mawaziri na wabunge pamoja na viongozi wa chama tawala na wapinzani wote walipigwa na butwaa kwa kile kilichokuwa kikiendelea mitandaoni.

Vyombo vya usalama na mamlaka ya maswala ya mawasiliano vilikuwa bize kwenye vikao vya dharura kulizungumzia swala hili zito.Viongozi wa vyama vya upinzani waliona kabisa nuru ya kuichukua nchi katika uchaguzi mkuu kwa kutumia skendo hii chafu ya Rais iliyokuwa ikivuma mitandaoni.

Vijana wanaohusika na mawasiliano ya Rais pamoja na wanafamilia wa karibu na Rais waliitwa Ikulu ili kurahisisha uchunguzi. Derick alikuwa bize kwenye kompyuta yake na wale mahaka wakubwa wa kitaifa waliletwa ikulu ili kuchambua kwa kina nani alihusika kumchafua Rais kwa kiasi kile.

"Kila mtu aache anachokifanya sasa Mheshimiwa anaingia" Imma Mkuu wa mawasiliano ya Rais, alitoa oda kwenye kile chumba maalumu cha mawasiliano ya ikulu kilichokuwa kimejazana wataalamu wa kompyuta wakiongozwa na Derick pamoja na Mkewe Sarah.

Derick ni mtaalamu wa IT, aliaminika kufanya kazi na mahaka wakubwa duniani. Lakini sura yake imeungua kiasi ambacho sura yake haijulikani. Ni kijana muaminifu wa Waziri mkuu, na kipenzi cha wengi pale ikulu. Mara nyingi angevaa maski ya kuzuia sura yake iliyokuwa inatisha mnoo.

"Hadi sasa hamjagundua, Derick please nakuaminia" Waziri wa Ulinzi na usalama alianza kuongea baada ya Rais kuketi huku kichwa akikiinamisha mezani kwa aibu, hasira na wasiwasi.

Derick alimuangalia waziri na kutikisa kichwa kinyonge kwa ishara ya kukata tamaa huku Sarah akivuta pumzi nyingi na kuiachia kwa pamoja ishara ya kuchoka na kulikatia tamaa lile swala.

"Prisca, naomba ushauri wako tafadhali" Rais alimuangalia makamu wake kama mshauri pekee ambaye ataweza kumsafishia ile skendo.

"Tuseme imeeditiwa siyo sisi mheshimiwa! Bora tudanganye kwa nguvu zote" gafla pale chumbani paliibuka minong'ono kwani jibu la makamu liliondoa utata uliokuwa kichwani kwa wengi kuwa ni kweli au ni uongo.

"Kwa maana hiyo ni kweli ile video ni..." Mzee Tesha Rais mstaafu, alitamani kuuliza ila akaishia katikati baada ya kushindwa kulitaja lile tukio kwa kuona aibu.

"Kwanza kabisa, mzee wangu naomba nikiri ile video ni ya kweli kabisa, wahusika ni sisi kweli na lile tukio ni kweli kabisa. Sasa sijui cha kufanya ndugu zangu, Natamani kifo tu kwa sasa, naona kabisa ilivyokuwa ngumu kupingana na ukweli." Rais aliinamisha kichwa na kujifuta jasho kwa kitambaa moyo ukidunda kwa kasi kisha akaendelea.

"Hata kama tukimpata aliyevujisha hii video, labda tutamuua, labda tutamfunga au tutamfanya chochote lakini mimi haitanisaidia chochote katika kiti changu cha Urais. Haitatusaidia sisi kama Chama kikubwa hapa nchini, wala haitatusaidia kufuta chochote kinachoendelea kwa..." Kabla hajamaliza Imma alimkatisha.

"Itatusaidia mkuu, kwanza kabisa kumbuka video haijaisha, tukimpata huyo mjinga itatusaidia kujisafisha sanaa kulikoni unavyowaza."

"Kweli Mh, inabidi tumpate kwa haraka sana kwani atakapoipandisha video nzima basi ndipo itakaposhindikana kujisafisha" Derick naye aliendelea kumpa moyo bosi wake.

THE COMEBACK Where stories live. Discover now