MIPANGO

0 0 0
                                    

Tuliingia kwenye Range na sasa tukaanza Safari ya kurudi Dar. Imma alinipa chipsi kuku na energy drink, nikala nikapata nguvu na sasa nipo tayari kuuliza maswali.
"Bro! Samahani lakini, sielewi kitu chochote... Unaweza ukanielezea nini kimenipata" nilianza kuuliza.

"Ngoja nipaki gari pembeni tuongee" Alinijibu huku anapaki gari pembeni kwenye kichaka. Moyo ulianza kunienda kasi kwani sielewi nini anataka kunifanya.

Baada ya kuegesha gari nje kidogo ya Baraba kuu, tulishika tukakaa mbele ya ile Range. Imma akachomoa bastola yake tena. Nilidhania anataka kuniua, aliniamuru nikae juu ya ile gari, nilifuata amri.
"ALEX, unakumbuka namba iliyokuwa ikikupa maelekezo kuhusu waziri!?" Aliniuliza, nikakumbuka siku chace nyuma, namba mpya iliyokuwa ikiniibia siri za Waziri.
"Ndio naikumbuka vizuri braza!"

"Aliyekuwa anakutumia SMS ni mimi, sawae,.. Sasa hapa una machaguo mawili. Kufanya kazi na mimi au kufa... Katika mtu hapendi kuongea sana ni mimi, nipe chaguo lako haraka"
Imma alikuwa ni mkali, mbabe na anajiweza kimwili. Sikuwa na chaguo zuri zaidi ya kufanya naye kazi japo sijui ni kazi gani.

"Kufanya kazi na wewe,.. hilo ndio chaguo langu braza" nilijibu huku natetemeka kwa uoga. Hakina hata ngedere anakatiza, hakuna hata sauti za ndege. Yaani ukiuliwa hapa hutokaa upatikane.

"Naitwa Imani Tumaini, nipo kwenye kitengo maalumu cha usalama wa taifa. Lakini kazi yangu ni kumlinda Rais, na ni shushushu wa Waziri mkuu. Nipo sana kwenye kitengo cha mawasiliano ya Rais, nina siri nyingi za nchi hii na nina siri nyingi za Waziri na Rais" Akanywa tena energy kisha akaendelea.
"Chuoni ulikuwa unafundisha historia kama sikosei, ila cheti chako kinaonyesha umesomea IT, si ndio?" Imma aliniuliza.

"Nilifundisha Falsafa na History pia. IT nilisoma tu kwa udogo kwaajili ni..." Akanikatisha.
"Hiyo hiyo kidogo. Nataka nikuingize kwenye kitengo cha mawasiliano ya Rais. Kuna mpango wa kumchafua Rais, huu tunautekeleza na Waziri mkuu, kisha nitakupa mpango wa kumpindua Waziri na kukitoa chama cha CUT (Chama cha Umoja wa Taifa) madarakani. Mimi ni kijana wa mzee Msheti, kiongozi mkuu wa CHACHAMA (Chama Cha Maendeleo) Chama kikuu cha upinzani hapa nchini"

Hee! Sikumuelewa, yaani mtoto wa mzee Msheti awe ndani ya mfumo, awe ndio mkuu wa mawasiliano ya Rais, tena awe karibu na Waziri mkuu! Mbona ananichanganya.
"Kwahiyo wewe ndio uliniambia nimuandikie CAREN kile kimeme!?"
"Ndio ni mimi na nilimpelekea. Nipo nafanya mpango wa kumtorosha naye atatusaidia sana kipindi cha kumchafua waziri" alinijibu huku anaendelea kuifuta bastola yake.
"Watoto wa Msheti mbona wanajulikana wote?" Nilimuuliza.

"Mimi mzee alinizaa nje ya ndoa, amekuwa akiniandaa kwaajili ya kuupindua utawala wa CUT, nchi inaelekea pabaya na namna pekee ya kuiokoa tunatakiwa tupatikane watu wenye nguvu ndani ya Mfumo wa watawala. Nipo na mwenzangu anaitwa Sarah, unamjua na anajulikana na taifa zima, ni mtoto wa Waziri!"

"Yaani mtoto wa waziri yupo tayari kumsaliti baba yake!?" Nilishangaa na sasa nikaanza kupata ujasiri wa kusimama na Imma.
"Nguvu ya mboo braza, nilifanya juu chini nikafanikiwa kuwa na mahusiano na yule demu, nikamtomba kisawa sawa, hadi akanizimia, nikamuonyesha unyama mzee wake aliomfanyia Caren, afu Sarah alikuwa ni shabiki mkubwa sana wa Caren, hivyo akakubali kuingia kwenye mpango wa kumpindua mzee wake"
Mambo niliyokuwa nayasikia ni kama naotea, yaani Sarah anavyokuwaga mwana CUT kindaki ndaki leo naambiwa yupo kwenye mpango wa mapinduzi.

"Ila ili kuendelea kuheshimiwa na kuaminika na Waziri, mahusiano yangu na Sarah ni ya siri sana. Na nisikufiche nampenda kweli, na yeye yupo tayari kufa kwaajili yangu... Sasa nikikuingiza kwenye system nataka tudanganye wewe na Sarah ni wapenzi, mfunge hadi ndoa..." Aliwaza kidogo, anaomekana amepania sana huu mpango wao.

"Yeah mfunge ndoa, ila usijaribu kumtomba nitakuua... Utaishi naye nyumba moja ila vyumba mtalala tofauti, tukifanikiwa kumtoa Caren atakuja kukaa na wewe ila tutasema ni mfanyakazi wako wa ndani" Imma alizidi kunipa mipango.
"Sasa waziri si ananijua, anamjua na Caren, nani hamjui Caren hapa nchini!" Nilianza kujaa kwenye huo mfumo.
"Teknolojia imekuwa sana, kuanzia leo tutakubadilisha sura na jina na sahau kuhusu Alex utaitwa Derick..."
Nikikumbuka mateso niliyopitia miezi iliyopicha, siwezi kukataa mpango wa kumuua Waziri hata kidogo nipo tayari kufanya kila baya juu ya waziri.

Kinachonifurahisha zaidi ni kuwa nitapata fursa ya kuwa na Caren utamu wangu, lakini vipi kuhusu aliyekuwa mke wangu na watoto wangu ilibidi nimuulize Imma kama ana taarifa zozote.
ITAENDELEA

THE COMEBACK Where stories live. Discover now