Sehemu ya 1: JINA

639 13 6
                                    

Alikuwa ni msichana mrembo sana kutoka pande za kaskazini mwa Tanzania mwenye asili ya kimburu kabila linalopatikana wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara pembeni mwa mkoa wa Arusha. Alikuwa akiishi na wazazi wake wote wawili, wazazi wake walimpenda sana na walimlea kimaadili, ingawa waliishi kijijini lakini walikuwa ni waromani katoriki wazuri na walimpenda Mungu na kumtegemea kila wakati katika maisha yao ya kuhama hama. Kila siku msichana huyu mrembo alivaa rozari na alijua hasaa kuitumia.

Aliitwa MALAIKA jina alilopewa na wazazi wake ambalo liliendana sawia na uzuri, utulivu, kumcha Mungu, maadili na upole aliokuwa nao.. Alipofikia umri wa miaka 8 mama yake alipigwa pembe na ng’ombe wakati anakamua maziwa asubuhi na kufariki dunia hapo hapo. Akiwa hajapoa kwenye maumivu na simanzi ya kumpoteza mama yake mzazi na kuendana na hali halisi, baada ya miaka miwili akiwa na umri wa miaka 10 baba yake aliumwa na nyoka aina ya kifutu akiwa porini wakati wa kuswaga ng’ombe na kufariki dunia. 

Baada ya vifo vya wazazi wake ndugu za baba yake mzazi walijichukulia mali bila huruma na wala hawakumuachia kitu chochote, walibeba mbuzi, ng’ombe, na kondoo wote ambao wazazi wa Malkia walikuwa wanafuga wakamuacha Malkia akiwa maskini hajui afanye nini na wala hana mbele wala nyuma na hata hajui hatma ya maisha yake.

Mipango ya ndugu hawa ilikuwa ni kumuozesha Malaika kwa mzee mmoja maarufu sana kijijini hapo aliyeitwa Oldei. Mzee huyu alikuwa na wake kumi tayari na kuwajengea nyumba kila mmoja kiasi kwamba eneo lake na shamba na nyumba za wake zake lilikuwa kama kijiji. Malaika hakupenda mipango hiyo na aliamua kutoroka kijijini hapo na kwenda kusikojulikana ili mradi awe mbali na ndoa hiyo.

Akiwa kwenye mawazo mengi huku ameketi nje ya nyumba yao ya nyasi alimuona mtu kama mjomba wake kwa mbali akielekea pale alipokuwa. Malaika alifikiri anaota maana mjomba wake huyu hakuwahi kurudi kijijini toka alivyoondoka na mzungu mmoja aliyekujaga kijijini hapo kufanya utafiti. Ghafla Malaika akaondoka kwenye dimbwi lake la mawazo na kumkazia macho yule na kugundua ingawa ni miaka mitano imepita tangu waonana mara ya mwisho lakini mjomba wake huyo hakubadilika sana, zaidi sana alipendeza na kung'ara uso zaidi na ngozi yake ilionekana nyororo tofauti na alivyoondoka.

Zilikuwa zimeshapita wiki mbili tayari na hivyo Malaika hakuwahi kuzani kwamba kuna ndugu mwingine anaweza kuja kwa ajili ya msiba. Mjomba yake huyu alichelewa kama wiki mbili hivi baada ya mazishi ya baba yake kwahiyo alifika akakuta hata matanga yameanuliwa na Malaika akiwa amebaki peke yake. Malaika alitabasamu bila kujijua na kuamka haraka na kuanza kumkimbilia huku akimwita kwa sauti kali kama mtu aliye mbali wakati alishakaribia ni kama hatua tano tu na pale alipokuwa.

MALAIKAWhere stories live. Discover now