Mjomba: Pole sana mwanangu Malaika, Pole na yaliyokukuta mwanangu
Malaika: Asante sana mjomba
Ghafla sura yote ya Malaika iliyokuwa na furaha na tabasamu ilipotea na kugubikwa na huzuni na machozi, huku akilia kwa uchungu, Latoi alitoa kitambaa cheupe alichokichukua kutoka kwenye mfuko wa suruali yake na kumsaidia Malaika kufuta machozi. Alimshika mkono na kumuongeza kukaa pale alipokuwa amekaa mwanzo na kisha yeye naye akaketi pembeni yake.
Mjomba: Mama yako alinipa jukumu la kukutunza kabla sijaondoka hapa kijijini, kwahiyo Mzee Oldei aliponiambia kuhusu kifo cha baba na mama yako sikuweza kuwa na amani na nilihuzunika sana na kuamua kuja kutimiza ombi la dada yangu kipenzi.
Malaika: sikuwahi kufikiri kwamba unaweza kurudi kijijini, baada ya kuambiwa na kuhadithiwa uliko ni kuzuri sana kuna majumba mazuri na kuambiwa na mama unaishi na mzungu. Nilidhani nawe ukirudi utakuwa mzungu na ngozi yako itabadilika.
Akiwa amenyamaza kulia na kutamani kuambiwa Zaidi huko alikokuwa mjomba wake
Mjomba: Hahahahaha hapana Malaika siwezi kubadilika ngozi hii wala kuibadilisha ndio aliyoniumbia Mungu na kuona inafaa. Kwa kweli mambo kule ni mengi, na kazi ni nyingi, kwahiyo muda wa kusafiri kidogo unakuwa ni mfinyu sana,
Malaika: Mjomba lakini umekuwa mzuri kweliiii, na huko hawavai tena mashuka, mbona wewe hujavaa, umevaa kama watu wa mjini?
Mjomba: Malaika wanaume hawawi wazuri, ingawa nakubali nimenawiri kidogo, vyakula vya kule si kama vya huku
Malaika: Ni vitamu eee?
Mjomba: Hahaha Malaika viko tofauti, na kwasasa nimeshavizoea zamani nilikuwa sishibi, na nikaitamani sana mihogo, ugali na vyakula vya kwetu.
Malaika: Ooo ungeniambia ningekufungia na kukutumia, ningemuomba mtoto wa Mzee Oldei ambaye tunaendaga naye kanisani anisaidie, ananiambiaga anamtumiaga kaka yake barua huko Arusha
Mjomba: Hahaha Malaika si rahisi hivyo,
Malaika: Oooo kwahiyo sasa utaondoka na unga, bamia, mihogo uende ukaipike huko
Mjomba: Hahaha hapana sasa nitakuchukua na ukikubali tutaondoka wote.
Malaika: Ni kweli mjomba ni kweli umekuja kunichukua, mjomba nitafurahi sana nuru imenizukia Mungu amesikia maombi yangu, mjomba niko tayari maana nilishaipanga mizigo yangu kwasababu nilikuwa nataka kutoroka
Mjomba: Kutoroka (Kwa mshangao)
Malaika: Ndio mjomba
Mjomba: Ulikuwa unataka kwenda wapi

VOCÊ ESTÁ LENDO
MALAIKA
ContoMalaika alikuwa ni msichana mrembo sana aliyepata nafasi ya kutoka kijijini kwao Mbulu kuikimbia ndoa wakati akiwa mtoto na kwenda kuishi na mjomba wake nchini Canada. Maisha yalikuwa ni mazuri mpaka alipoamua kuyaharibu baada ya kukutana na kuwa n...