Ilikuwa ni safari ndefu na iliyojaa uchovu lakini walifanikiwa kufika Toronto salama salimini. Malaika aliendelea kushangaa kila kitu na alifikiri yuko kwenye ndoto kila wakati alifikicha macho yake na alifikiri anaota. Alijisemea moyoni kama ni ndoto hatamani kamwe kuamka, aendelee tu kulala. Aliona magorofa aliona wazungu na watu wengi wageni machoni pake, alikula vitu vigeni kwenye ndege vipisi vya mkate vilivyochanganywa na mboga mboga hakuvielewa lakini aliona vitamu na alivipenda. Safari nzima mjomba yake aliongea naye kuhusu ni kitu gani angependa kukifanya na kwa kuwa ndio kwanza alikuwa anatoka nje ya kijiji chao Malaika hakujua ni nini anaenda kukifanya huko anakoenda. Ingawa alimwambia mjomba wale anapenda sana kusoma na kuwa mtu muhimu kwenye jamii lakini hakujua anaenda kusomea nini maana alikuwa amefika darasa la 4 tu katika shule ile ile aliyosoma mjomba wake Orkesmet. Wakati wanaendelea kuongea haya mjomba wake alikuwa anajaribu kufikiria ni namba gani atamsaidia Malaika katika shule na ni namna gani anaongea na mke wake Lenny kuhusu Malaika kuishi nao.
Siku ambayo walifika Canada Lenny alishindwa kwenda kuwapokea kwasababu alikuwa na presentation kubwa sana chuoni kwake kwahiyo waliongea kwenye simu na mume wake kuwa atawakuta nyumbani kwasababu tayari kuna mtu alishamtuma kumpelekea funguo Latoi uwanja wa ndege. Baada ya kama masaa mawili Lenny alirudi nyumbani na kwasababu alikuwa amemmisi sana mume wake alifungua mlango kwa nguvu zote na kuanza kuita kwa sauti kubwa
Lenny: Baby baby where are you,........am home? (Mpenzi uko wapi)
Latoi: am here (niko huku)
Lenny alijua sauti inatokea wapi kwahiyo akienda jikoni akatoa viatu na kuweka laptop yake kwenye meza ndogo iliyokuwepo sebuleni, kisha akalitupa pochi lake kwenye kiti na huku akitoa hereni zake anaelekea jikoni. Latoi alikuwa ametoa juice ya machungwa ilikuwa kwenye jokofu na ameiweka kwenye bilauri tayari kwa kuinywa, lakini kabla haijafika midomoni mwake aliisikia sauti ya mkewe na kwa hamu kubwa akaiweka chini na kumsubiria mkewe akiua vema anamfuata aliko. Alivyofika jikoni walikumbatiana kwa furaha sana na kuanza kubusiana kisha Latoi alimsogeza mke wake
Lenny: I missed you so much baby, next time we will travel together (nilikukosa sana mpenzi, wakati mwingine tutasafiri pamoja)
Latoi: I missed you too honey (nilikukosa pia mpenzi)
Wakati Lenny anaendelea kutaka waendelee walichokuwa wameakianza na Latoi huku akianza kumfungua vifungo vya shati, Latoi alimsimamisha asiendelee na aliochokuwa akikifanya
Latoi: Honey we have a guest (mpenzi tuna mgeni)
Lenny: What? Who? (nini, nani)
Latoi: My nephew (mtoto wa dada yangu)
Lenny: Nephew...oooohhh Malkia,..oooh sorry Malaika(mtoto wa dada yako Malkia....oo hapana Malaika)
Latoi: Yes
Lenny: you promised to talk about her when you are here, can we talk now
Lenny alikuwa ameshabadilika kutoka kwenye hali ya uchangamfu ambayo alikuwa nayo mwanzo na kugeuka kuanza kutembea kuelekea sebuleni Latoi akimfuata nyuma. Alivyofika sebuleni alimkuta binti ameketi vyema kwenye moja ya sofa zilizokuwa zimewekwa sebuleni
Lenny: hi
Malaika: hi (huku akiwa na hisia za kutokujua aitikie nini lakini pia kumuona shangazi yake kama vile hana furaha)
Baada ya kusikia makelele yale shangazi yake alivyokuwa anamuita mjomba wake, alitoka nje ya chumba alichoambiwa akae na mjomba wake. Akafika sebuleni na kukuta vitu tu vimewekwa na aliyekuwa anapiga makelele hayo hayupo kwahiyo alisubiri akiwa amekaa hapo sebuleni katika moja ya sofa zilizokuwepo sebuleni hapo
Lenny: I am Lenny (Mimi ni Lenny)
Malaika: My name Malaika (akimaanisha jina lake ni Malaika Lyatong)
Lenny: Mambo
Malaika: Poa
Lenny katika kukaa kwake Tanzania hakujua Kiswahili vizuri kwasababu mara nyingi alikuwa anaongozana na mkarimani, na miongoni mwa maneno ambayo alikuwa anayaweza ni pamoja na Mambo, Poa, hivyo ndio aliona salamu inayomfaa Malaika. Baada ya kufika sebuleni aliokota viatu vyake, laptop na pochi yake na kumuangalia Latoi
Lenny: Can we go to our room please, Malaika give us a moment (tunaweza kwenda chumbani kwetu tafadhali? Malaika tunaomba tukuache kidogo)
Latoi: I am coming (nakuja)
Latoi akachukua remote yakufungulia luninga kubwa ya nchi 33 iliyokuwa sebuleni na kumfungulia Malaika, ili wakati wanaendelea kuongea yeye awe anaburudika na vipindi vya kwenye runinga asiwe mpweke na kisha kwenda chumbani ambako alimkuta mkewe ameshakaa kitandani anamsubiri.
VOCÊ ESTÁ LENDO
MALAIKA
ContoMalaika alikuwa ni msichana mrembo sana aliyepata nafasi ya kutoka kijijini kwao Mbulu kuikimbia ndoa wakati akiwa mtoto na kwenda kuishi na mjomba wake nchini Canada. Maisha yalikuwa ni mazuri mpaka alipoamua kuyaharibu baada ya kukutana na kuwa n...