Nisamehe Mpenzi(iv)

67 4 0
                                    

Kelvin alipigwa na bumbuwazi akabaki kukenua,mwili mzima umekufa ganzi na miguu kutostahimili uzito wa mwili.

"Aimi!"Alishangaa, halafu akajikokota taratibu mpaka alipokuwa mpenzi wake.Machozi yalianza kumlengalenga alipoona jinsi mtoto wa watu alivyokishindilia kisu kitovuni.Damu imezagaa sakafuni na kwenye kitanda.Mtoto wa watu anapumua kwa shida na kutokwa na machozi.Nguvu zimemtoka na kumwacha mchege kama utumbo wa samaki.

Macho yao yalikutana.Kila mmoja wao uchungu tofauti na wa mwengine.Kilio cha kite na simanzi kikahanikiza kote.

"Nisamehe mpenzi," alisema Kelvin kisha akaendelea,"Sikunuia kukuvuaza.Ningali nakupenda.Mbona ukafanya hivi mpenzi wangu?Wajua uchungu wa majuto ulivyonivaa?"

Kelvin alitaka kuzungumza zaidi lakini maneno yakakwama koromeoni.

Monicah akausogeza mkono wake kinyonge na kumshika Kelvin mashavuni.Akamwangalia kwa takriban sekunde kumi hivi kisha akafumba macho.Mkono uliokuwa mashavuni ukaanguka kitandani bila mwendo.

"Usiniache tafadhali."Alimsihi Mola moyoni asimchukue mpenzi wake.Alitaka kukarabati mienendo yake na kumpenda kana kwamba hakuna kesho.

Papo na hapo,Maria akajivuta kwa nguvu na kurudi chumbani aliposikia huzuni kwenye usemi wa Kelvin.Alikuwa akisikia maneno yake lakini hakujua kuwa angekutana na alichokiona.Kelvin alikuwa amemlalia Monicah kifuani pake,analia kama mtoto atakaye titi la mamake,damu imeroa kwenye mavazi yake mpaka usoni.Machozi yake yamechanganyika na damu,akawa kama mwendawazimu manake alipogeuka na kumwona Maria alipandwa na mori na kusimama.

"Mbona umemuua?"

"Mimi?saa ngapi?"

"Usijaribu kunipayukia hata kidogo.Kama si wewe nani vile basi?"

"Si mimi wallahi!Lakini kifo chake si sherehe kwetu?"

"Maneno mengine kama hayo ya kipuzi yatoke,utakuwa mzoga sasa hivi!"Alitishia kisha akaelekea mlangoni aliposikia kana kwamba kuna mtu anaingia chumbani.Hakutaka kisa hiki kijulikane na mtu yeyote wala  wanahabari.

Mara tu Matuko akatokea mlangoni.Macho yamekodolewa kwa hasira,mashavu yamevimba kama mvua ya masika na kumwacha kama nduli asiyekuwa na shufaka.Mkononi ameshika panga aliyompokonya jirani ya Kelvin alipokuwa akichanja kuni zake.

Kelvin alichukua hatua chache na kurudi nyuma.Haonyeshi dalili zozote za woga manake moyoni hahisi maana ya kuishi tena.Alitaka tu kuchukua muda wake aone kama angeweza kukabiliana na Matuko.Alijua fika kuwa hapa patakufa mtu mwengine.

Maria aliushika mdomo kwa mshangao.Hakujua mbona Matuko alikuwa na damu mikononi na usoni mwake.Ama yeye ndiye kasababisha kifo cha Monicah?alinuiza.

"Ulinihadaa kuwa mpenzi wangu hayuko huku?Hiyo ni sanamu nyuma yako?Mbio za sakafuni huishia ukingoni"

Kelvin hakusema kitu.Alibaki kimya kama bubu.Aligeuza kichwa taratibu na kuelekeza macho yake alipokuwa amelala Monicah.Matuko hakuonekana kutekwa na hisia zozote za huzuni wala mshangao.

"Maria amemuua mpenzi wangu,"alisema Kelvin.Hasira ikidhihirika usoni pake.

"Mbona amuue?Wewe na yeye nani aliye na damu?"


Sura ifuatayo ndiyo mwisho wa kisa hiki.Unatarajia nini kifanyike kati yao?

Vote and comment♥

Nisamehe MpenziWhere stories live. Discover now