Nisamehe Mpenzi

57 2 0
                                    

"Maria Kash,"akajibu.

"Una uhusiano gani na barobaro tuliyemtia nguvuni?"
Swali hili lilimpata Maria sawasawa na akaamua kutodanganya hata ingawa alikuwa ameamua lazima amtie Kelvin taabani.Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.

"Kelvin alikuwa mpenzi wangu wa mpango wa kando.Yote tuliyoyafanya naye yalikuwa fiche ili penzi langu na Matuko lisiharibike."

"Matuko ni kijana aliyepigwa risasi alipopatikana akitaka  kushambuliana kwa panga."

Maria tayari alikuwa keshaanza kulia kwa uchungu.Alikasirishwa na usaliti wake mapenzini haswa akumbukapo kuwa Matuko alikuwa mtu mwongofu na mwenye maono maishani.Taamurini anafahamu kuwa asingesaliti penzi lao bila shaka Matuko angekuwa analibingirisha gurudumu la maisha.Hata hivyo,mwiba wa kujidunga hauna kilio.

"Ndiyo,"akajibu kwa upole baina ya kilio cha simanzi.

Inspekta aliwaangalia wote waliokuaa hapa kama mtu atakaye kitu kutoka kwao.Moyoni alihisi binti wa huyu hakuwa akiwaongopea lakini hakutaka kuonyesha hisia zake.

"Nini haswa kilichangia kioja kilichokuwa chumbani humo?"

"Usaliti tu.Binti huyo alijidunga mwenyewe kwani mimi nilikuwa nimejificha dirishani nisije nikaonekana kwani nilikuwa nikila asali mzingani mwa mpenzi wake.Kwa bahati mbaya mpenzi wangu akawa anakuja huko na kupata kufahamu kuwa nilimsaliti na mtu mwengine ndiposa akabwaga zani chumbani humo."

Wote waliokuwa hapo walionekana kutoshelezwa na maelezo ya binti huyu lakini pia wakataka kujua upande wa Kelvin ili kubaini ukweli wote kwa kina.Hakika walipomhoji Kelvin maelezo yake hayakuwa na ukinzano wowote na ule Maria alioeleza.Siku iliyofuatia ikabidi wameachiliwa huru na kila mtu kurejea katika maisha yake ya kawaida.

Kelvin na Maria hawakusemezana hata neno moja wala kuangaliana.Ungeweza kuona chuki na dharau machoni mwao.Kelvin aliulizia alipokuwa Monicah na alipopata habari kamili akafululiza moja kwa moja hadi hospitalini.Mkononi alikuwa na shada la maua na ndani yake barua ya kumtaka Monicah msamaha.Kando na hayo alikuwa na matunda ambayo aliamini Monicah angeyafurahia.Alipofika aliruhusiwa na wauguzi kumwona baada ya kuwaelezea uhusiano wao na mgonjwa huyu.

Kitandani Monicah alilala chali,uso wake ulisheheni huzuni na mawazo mengi.Hii si kawaida yake kwani Kelvin alimjua Monicah kama binti mpwamu sana.Alikuwa akiongezwa maji na damu ili kurejesha hali yake ya kawaida.

Monicah alipomwona Kelvin akiingia alianza kutokwa na machozi na kujaribu kugeuka aangalie upande mwingine.Hakutaka kumwona wala kusikia chochote kumhusu.Aliyafumba macho yake lakini vyovyote vile machozi yalipata nafasi ya kumtiririka tu.Alitaka kulaani kizazi chote cha jinsia ya kiume na kutotaka kusikia chochote kuwahusu.

Kelvin alitembea polepole mpaka alipokuwa laazizi wake na bila neno lolote akampigia magoti.Aliliweka shada la maua na matunda kando na kuushika mkono wa mwendani wake wa karibu na kuanza kuupapasa taratibu kisha akaubusu mara kadhaa.Monicah hakuwa akitaka chochote kuhusiana na mapenzi tena.Kwake penzi likawa kama nanga.Kelvin alidhani kupata penzi kutoka kwa binti huyu ni kanda la usufi.

"Nenda tafadhali.Sitakuekea fundo chungu moyoni asilani kwa sababu nilikusamehe kitambo ila sitaki mapenzi yako tena.Nimechoka na kuchoshwa na mapenzi haya.Nimevumilia kwa muda na sioni haja ya kuzidi kutumainia kupata mbivu mishowe.Naomba uniache tafadhali na uondoke."

"Usiseme hivyo tafadhali.Nakuahidi sitarudia kosa kama hilo tena na nakuhakikishia kuwa nitakutunza na kukulinda vizuri."

"Ahadi ulishanipa nyingi na hujawahi timiza hata moja.Ninakujua vizuri na matendo yako yaliyovunda siyataki tena maishani mwangu."

Kelvin alijaribu kujitetea hata kwa kilio akiwa amepiga magoti lakini wapi.Maji yalishamwagika!

"Nurse,"Monicah aliita kwa nguvu na bila kupoteza muda wauguzi wawili wakafika.
"Kuna nini," mmoja wao akauliza.

"Naomba kuwa peke yangu humu.Mtu mwingine asije huku ndani."

Kelvin alielewa habari ile na hakutakiwa kuambiwa atoke.Aliinuka taratibu na kuelekea mlangoni.

"Umesahau vitu vyako,"Monicah akasena.

Kelvin hakugeuka kuvirudia.Alienda na kutokomea kusikojulikana.Barua na matunda yale Yalichukuliwa na wauguzi na kutupwa manake Monicah hakuyataka.Miezi mitatu baadaye Monicah alikuwa keshapona na afya yake kurudi.Alikuwa tayari amejiunga na kanisa la katholiki na kuwa sista huko kwani hakutaka mwanaume maishani mwake tena.Aliamua kumtumikia Mungu maishani mwake kwa imani kuwa atapata tikiti ya binguni.





End.Thanks for the read,it's short but  I look forward to writing more.
@WeyeMatuko in Twitter.
Erick Ndungu in FB

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Feb 07, 2020 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

Nisamehe MpenziWhere stories live. Discover now