karata ya mahaba 2

5 0 0
                                    

Katega alikuwa ameketi kochini akitia na kutoa,amezama mawazoni kiasi kwamba hakusikia Hadasa akiingia nyumbani.
“Baba,simu yako inakiriza.”
Katega aligutuka na kuiangalia simu upesi,akavaa viatu vyake na kuipokea kama kwamba alijua mbona alipigiwa.

“Amepatikana?”Katega aliuliza.

“Ndiyo.Lakini amekataa kusema alikotoa habari ile.”Sauti fulani ikasema kutoka upande wa pili wa simu.

“Haya basi,hakikisheni mahali mlipo ni salama na mbali na watu.Nitumie,jumbe ya mahali mliko.Niko njiani.”

Hadasa alisimama pale na kumwangalia babaye akivalia sweta yake na kuchukua mkoba wake ambao alijua wazi kuwa una bunduki.Alishindwa kuelewa mbona hapati habari ya kinachoendelea.Ni juzi tu babake ameshinda kesi dhidi ya tuhuma ya mauaji ambayo alijua si tuhuma bali ni ukweli manake hata mashahidi walikataa kufika kortni na wengine kuawa kwa njia tatanishi.Mwezi uliopita alikabiliwa na kesi dhidi ya biashara ya magendo ya kuwateka wasichana wadogo na kuwahusisha na ngono katika madanguro yake.Mwezi ujao atakuwa kortini kujibu mashtaka ya ununuzi wa heroini na bangi na uuzaji wa dawa hizo kinyume na sheria.
Hadasa aliambua nyayo zake upesi na kwenda mpaka chumbani mwake.Alihisi kichwa chake kikiwa kizito kutokana na msongo wa mawazo,alikuwa na mengi yaliyokuwa yakimla akilini na kumwacha mnyonge kama unyasi.Alijaribu kumpigia John simu ili kumjulia hali bila mafanikio.Maisha yake ya mahaba yamekuwa na pandashuka nyingi kwani hata aila yake haikutaka kusikia kuwa anajihusisha na mapenzi na mtu yeyote wa taifa lao la Heri.

Katega aliwasili katika jumba lao la siri lililokuwa katika shamba lake la mahindi,kilomita takriban kumi kutoka nyumbani kwake.Abdul alimlaki kumwelekeza alipokuwa mateka wao.

“Wapi kanda ya video uliyorekodi?”

“Ni fununu kutoka kwa mahasidi wangu kuwa mimi ndiye niliyerekodi kanda hiyo ya video,sijui chochote kuhusu kanda hiyo wallahi bilahi.”

“Maisha yako yako mikononi mwako.Sitapoteza kitu chochote nikikuua sasa hivi manake kesi yangu itatupiliwa mbali.Nina habari tosha kuwa ulirekodi kanda hiyo na kuipeleka moja kwa moja hadi kituo chenyu cha habari,jambo lililofanya nifunguliwe mashtaka.Mavi usiyoyala wayawingiani kuku?”Katega aliingia mfukoni mwa mkoba wake na kuichomoa bunduki yake na kuiramia kwa risasi.

“Samahani,usiniue tafadhali.Nina mtoto mdogo na mke wangu ni mjamzito.Mimi ndiye uti wao wa mgongo.”

“Najua hayo yote.Huenda kuteswa kwako na kuuawa hakutanisaidia kwa sababu kanda ile ingali kule nje.”Katega alitoa sigara mfukoni na kuipiga kiberiti na kuhanikiza chumba chote kwa moshi.Abdul na wenzake walikuwa mlangoni kama walinzi huku wakifuatilia matukio yote.

“Naomba uniamini,”Opondo alisihi.

“Pengine nimwamini Bwana Matani.”Papo na hapo Opondo akajua wazi kuwa kitumbua kimeshaingia mchanga na mchezo wake wa paka na panya kujaribu kuficha uhalisia wa mambo ni sawia na ubahau wa mbwakoko kujificha kwa unyasi.
Bwana Matani alikuwa mkuu wa kitengo cha upeperushaji wa habari na mhariri mkuu wa habari zote katika runinga ya Leo.Baada ya kuipeperusha habari kuhusu ukiukaji sheria wa dawa za kulevya wa Katega,alipata barua fupi iliyotishia kuwaondoa wapendwa wake maishani kuanzia kwa mamake,mkewe na watoto wake na ndugu na marafiki zake asipojiuzulu katika cheo chake na kuwapa jina la mwanahabari aliyewasilisha kanda hiyo ya video.Lisilobudi hubidi.Aliona ni heri kumtoa mtu mmoja kama kafara ili wapendwa wake wawe salama wa salmini.

Opondo alipigwa na bumbuwazi alipoona mkewe akibururwa sakafuni hadi walipokuwa.Usoni alikuwa na majeraha ishara tosha kuwa manyanga'u hawa wamekuwa wakimtesa.Uso wake ulisawijika kwa huzuni na kuvimba kama andazi lililotiwa hamira,macho yakabadili rangi na kuwa na wekundu wa damu.Alipandwa na mori na vilevile huzuni ikamwingia kwa kuwa hangeweza kufanya chochote.

“Investigative reporter,heri ungenisikia na kuachana na hii kazi.”Janet alipata sauti ya kumtania mumewe.Aliishi kumwonya dhidi ya kupekua habari ambazo aliziona kuwa hatari katika usalama wao kwani baadhi yazo zilikuwa zikifichua mambo ya watu wenye nguvu serikalini.Huenda leo hii sasa ameshapata habari kuwa si jambo la busara kushindana na ndovu kunya manake atapasuka msamba.

“Janet,I Am sorry.”

“I know you are.Hatungekuwa katika halii hii iwapo ungenisikiza  nilipokuwa nikikuonya.”

Katega aliamuru Janet avuliwe nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na chini ya sekunde za kuhesabu Abdul tayari alikuwa kafanya hivyo.

“Utaketi hapo kuangalia mkewe akinajisiwa na mwanangu na wenzake au utanipa habari ya ninachotaka?”

KARATA YA MAHABAWhere stories live. Discover now