karata ya mahaba 5

1 0 0
                                    

“Ulikuwa unafikiria nini kupeleka habari kama ile kwenye kituo cha polisi?Unadhanj kuwa mimi ni mpumbavu au kilema singeweza kujipeleka mwenyewe?”Matani alifoka kwani alijua fika kuwa makuu yatawakumba.

“Nilifanya hayo kwa hiari ya kupata haki na heri katika familia.”

“Unajisikia hata?Umetuchimbia makaburi tayari.Kilichomfika Opondo kinatuandama,ki njiani chaja.”

“Unastahili kuona haya na kujikemea kwa kusababisha kifo cha Opondo na mkewe.Sasa Kamata kubakia yatima inakupa raha gani?”

“Chunga mdomo wako.Mimi ni babako mzazi na nastahili heshima.Neno jingine kutoka kwako liwe la kunidunisha utajua nani ndiye kusema huku.Wewe,mamako na nyanyako na marafiki zetu wako hai kwa sababu ya uamuzi wangu.Watu wawili tu ndio wameaga na wengine wengi zaidi kunusurika.”

“Umesaliti heshima na miaka yako kwa hatua uliyochukua.Mbona huoni mbali lakini?Dawa za kulevya si zitazidi kumaliza vijana wa kesho?Si katega atapata sababu ya kuendeleza ukatili wake dhidi ya watu kwa kuliendesha taifa hili anavyotaka?”

Matani alimrukia John kwa makonde na kumkandika makofi kadhaa.Muda huu wote Jesinta alikuwa akifuatilia majibizano ya mumewe na mwanao na alipoona mambo yanaharibika zaidi alirukia na kuwatenganisha.John alikuwa akivuja damu mdomoni na puani huku machozi yakiichukua sura yake.

“Mhandisi uliyemwingiza kule kazini ni kinyume na sheria na ndio maana Katega aliachiliwa kwa kukosekana kwa kanda zile na ushahidi wa Opondo aliyekufa mikononi mwako!Sikukuambia uchague maisha yangu na kuchukua ya wengine.”John alikuli kwa hasira na kilio na kwenda chumbani mwake na kujifungia.

Simu yake ikakiriza na alipoona ni nambari ya siri,hakushughulika kuichukua kwani alijua wazi kuwa ilitoka kwa Abdul.

“John,fungua mlango,”Jesinta alisema ila John alikataa kuufungua mlango.”Kusanya virago vyako tuondoke sasa hivi.”

“Tuondoke tukienda wapi saa kumi na mbili?Naona kama tunatoroka.”

“Ndiyo tunatoroka kwa sababu yako.”

“Kwa sababu ya baba na katega,”John alimrekebisha Jesinta.”Mbona unaonekana kukubaliana na baba haraka hivyo?Sijasikia hata ukikosoa matendo yake.”

“Tuko hai kwa sababu yake.Sisi ndiyo tungekuwa wafu.”

John hakuamini haswa ilipombainikia kuwa yuko peke yake katika harakati za kukemea uovu.Moyoni alikuwa akijisemea kuwa tofauti ya wazazi wake ni jinsia tu na lebasi walizokuwa wakivalia.Mengine yahusuyo ubinadamu hayakuwa muhimu maishani mwao.

Baada ya kupakia vitu vyao garini walilitia moto tayari kuondoka.Kinyume na matarajio yao,gari jeusi likasimama katika lango lao la geti na kisha wanaume wawili wakaingia na kufunga geti hiyo.Bila kupoteza muda wakamwambia John na Matani wawakabidhi simu zao haraka iwezekanavyo au wamiminiwe risasi.

“Ukitaka salama ya dunia fyata mdomo wako.Mwambie mwanao ajifunze kumezea lolote lisilofaa.”Mmoja wao alisema.

Kamata alionekana kucheza garini na mwanasesere asijue kuwa maisha yao yananing'inia kwenye kamba.John naye alikuwa amekaa kimya na jasho kumtoka kwa wingi.Hapa ndipo alipopata kufafanukiwa kuwa taifa hili lina wenyewe ambao kujaribu kufichua uovu wao ni sawia na kucheza na shilingi kando ya shimo la choo.Jesinta na Matani walitupiana macho ya huzuni tu kana kwamba walikuwa wakipeana salamu zao za mwisho duniani.
Baadaye,Abdul alivua barakoa yake na kukataa kuuficha uso wake.Alitaka John aweze kujua kuwa alikuwa akichezea bomu lililokuwa tayari kulipuka.Mfukoni akatoa chupa  ya maji iliyokuwa na sumu na kuwalazimisha waikunywe kwa mtutu bunduki.Matani ndiye aliyekuwa wa kwanza.

“Ninawapenda sana.”Alisema kisha kwa ujasiri akaikukumia sumu yote na kumwaga iliyobakia kama njia ya kuwatafutia wengine muda zaidi wa kuishi.Abdul hakushangazwa sana na tendo hilo kwani alirudi mpaka garini walilokuwa wamekuja nalo.Matani alikuwa tayari keshaanza kutoa povu kinywani na kisha akakata roho.Jesinta alipiga ukemi uliomliza Kamata.

“Plan B,”Akasema na kuchukua petroli na kuimwagilia garini.

“Basi ondoeni malaika huyu wa Mungu.”Jesinta alijaribu kuwasihi wayanusuru maisha ya Kamata.

“Mtaenda naye ahera au peponi.”Abdul akajibu.

Angani helikopta ilifika ghafla na nje makaradinga yakazunguka eneo hilo lote.Walijaribu kutafuta kukimbia lakini kila walipoenda walikutana na askari walioonekana kujawa na hamaki.

“Wekeni silaha zote chini,mikono juu.”Waliamriwa.Hawakuwa na njia nyingine ya kujinusuru isipokuwa kutii amri.Walifanya walivyotakiwa na kutiwa pingu na mwenzake Abdul kuvuliwa barakoa yake na kutupwa kwenye karadinga moja huku jingine likiubeba mwili wa Matani.

Kwa umbali wa mita mia moja,John akamwona Hadasa akishuka kutoka katika moja ya makaradinga na kukimbia alipokuwa na kumkumbatia.

“Nilidhani nitachelewa kuripoti.”Hadasa alisema baina ya kwikwi na upendo.Jesinta alikuwa amempakata Kamata nyasini huku bado akionekana kutoamini jinsi kifo kilivyowaepuka.Kweli,Kalamu ya Mungu haikuwa imeandika leo kuwa siku yao ya kufarakana na sayari hii.
Jambo walilokuja kubaini baadaye ni kuwa  Hadasa alisikia babake akiwaamuru Abdul na wenzake kwenda kuitendea aila ya John haki ili kuondoa ushahidi huku mwanapolisi aliyewapa habari hii akikabidhiwa jukumu la kuiba picha zile kisha, naye akafanya wanguwangu na kupigia 999 kufika katika makazi ya akina John.

Mwezi mmoja baadaye Abdul na mwenzake aliyejitambulisha kama Degrada walishindwa kustahimili mateso na kutoboa siri zote.Katega na askari yule msaliti pamoja na wote katika mviringo wao wa uhalifu walishikwa na kufikishwa mahakamani.

“Mmepatikana na hatia ya  ukiukaji wa sheria kama umiliki silaha bila idhini na mauaji ya kikatili.Hivyo basi korti hii imeamua kuwa Katega kushiriki kifungo cha maisha pamoja na washtakiwa wawili waliopatikana na silaha.Wengine watahukumiwa kifungo cha miaka arubaini kila mmoja.”

Hadasa alilia alipoona baba na kakake wakisukumwa hadi kwenye karadinga kwenda kutumikia vifungo vyao.Alitaka kusema nao lakini hakuweza.John alikaa naye na kumpa pole na morali kuwa alifanya jambo la busara.
Miaka miwili baadaye,John na Hadasa wakafunga pingu za maisha!.

KARATA YA MAHABAWhere stories live. Discover now