Sura ya Tatu

25 1 0
                                    

Bundi alopoingia jijini aliyaanza maisha mapya yenye shughuli za mchwa na changamoto  kimasomo.
Mazingara mapya ya kuwa huru,tena mjini yalimpiga dafrau akajipata amejiingiza katika uraibu wa pombe na kushiriki ngono za kikoinange.

Nazi yake ilimuozea kutokana na idadi kubwa ya wanaidara wahadisi, walevi,aliosoma nao;kisingizio kikiwa, masomo  mazito na magumu,yalioitaji kubumbuwaza akili mara kwa mara.

Walikuwa wanaanza kwa mvinyo wa nifungulie,hasa mwanzoni mwa muhula,na kumalizia kwa vifurushi na vikebe,wiki chache baadaye.
Ufunguzi wa muhula,mifuko yao ilijazana ngwenje kutoka kwa wazazi au mkopo wa serikali, uliobatizwa 'chacha'.
Pesa zilipokatika, waliingilia vileo vya bei rahisi na hata vile vya kienyeji;mathalan chang'aa.

Mgema alikuwa rafiki na mwanachumba wa Bundi,waliyesomea shule moja ya upili,hivyo kuwa rahisi kwao kufuma urafiki kule chuoni
Mgema alikuwa nazi mbovu iliyomwaribu Bundi.

"Kuna chaguo mbili,aidha pombe iingie ndani yangu au mimi niingie ndani yake!There is no other option" alipenda kusema sema kila akilewa chakali.

Ni kijana aliyetoka familia kwasi, hivyo pesa hazikuwa tatizo kwake.
Pengine tatizo lingekuwa jinsi ya kuzitumia.

Yote yalianza ile siku ya 'freshers night'.Siku iliyokuwa ya kwanza kwa Bundi kubugia mvinyo.
Ukawa mwanzo wa starehe ya miaka miwili iliyogeuka na kuwa karaha kwake.

Ni siku pia aliyoimpokonya  ubikira wake na kunadhifu ahadi yake kwa Suzzanna.
Ngoma ya kibongo ya mwanamziki maarufu,Diamond kutoka studio za Wasafi productions ilikuwa inaporomoshwa.
"Nataka kulewa.. lewa ..nataka kulewa..lewa."
Umati wote,akiwemo Bundi walikuwa walirusharusha mikono na miguu,vichwa kwa viuno;kila mmoja kwa styli  yake.
Wasiotunukiwa viuno walichezesha matumbo,vifua na wengine vichwa vyao.
Bundi tayari alikuwa kesha lewa na kila akitazama aliona viwiliwili.

"Am a very intelligent guy!.."  alijisemesha huku akipepesuka,nusra kuiramba sakafu kichalichali.
Kwa bahati nzuri alimkamata Peni asianguke.
Hapo ndipo lilianza gumzo na kudensi pamoja kwa wawili hao mpaka Chee!
Peni alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho akisomea ualimu.
Alikuwa maarufu kule chuoni kwa kuwatega 'fresha' na kuwafyonza hela zote,hasa wale walionekana butu kama Bundi.
"Baby am afraid of sleeping alone tonight,my roommate is not around.." alimsihi Bundi.
"Let's go..kwa.. kwani iko nini!" alisema Bundi bila kujitambua alichokisema.
Walishikana bega kwa bega na kuelekea chumbani mwa Peni.
Chovyachovya ya vyungu vya asali kati ya Bundi na Peni ikawa imeanza rasmi.
Peni alitumia ujuzi wake na ukosefu wa tajriba wa Bundi,kumpeleka safari yake ya kwanza.Safari isiyokuwa na mwisho na iliyomwacha Bundi na uchu wa kuikamilisha kila walipopatana.

Ikawa kila jioni wanavugia pombe na kuishia kitandani kuicheza lele hadi machweo.

Urafiki wao haramu, ulikatikatika ghafla wakati hela zilipompa  Bundi talaka.Akawa mvinyo hamununulii tena.
Pamoja na kufilisika,Bundi aliachwa akiuguza ugonjwa wa kisonono,ambao nusra upooze uume wake.
Umuhimu wa Bundi kwa Peni ulikuwa umemalizika,akawa kambi la miwa liloisha utamu na kufanywa mboleo.
"My fren if you can't buy me bia,songa ukisonganga" ndio kwakheri aliyopewa mwana wa Nyeri baada ya kuishiwa na hela.

***********************************
"Mgema akisifiwa.... sorry Bundi akisifiwa...." Mgema alimkejeli Bundi kutokana na masaibu yaliyompata.
"Am the only one who can swim in River Chania without clothes and nothing will happen to me.." alijivuna kama kawaida yake akilewa.
"Why did you go mining oil instead of fresh waters?" Aliangua kicheko hadi michirizi ya machozi kumdodoka njia mbilimbili na kuishia kinywani.
Bundi kwa fedhea alinyamaza ji! huku masikitiko yakimvaa kama kanzu Ijumaa.
Habari juu ya 'kuungua' kwake ilienea na kuenezwa kwa upesi kama moto wa majani makavu  wakati wa kiangazi.
Alitamani dunia imumeze mzimamzima asionekane tena milele.

SUZANNAWhere stories live. Discover now