Sura ya Kumi na Sita

23 1 0
                                    

Beck kilikuwa kitoto zeruzeru chenye miaka mitano kwa sasa.
Pekuapekua za Jason zilimtuliza kwenye uwanja wa ukoo wake palipopatikana uzeruzeru.
Palikuwapo zeruzeru katika ukoo wa mamake,ingawa kwa nadra sana.
Beck alikuwa moja wepo wa nadra hizo.
Beck ndio alikuwa tayari kaanza kuhudhuria shule ya chekechea.
Mwanzoni, Jason na Maria walimpeleka katika shule moja ya kibinafsi,lakini wakalazimika kumbadilishia shule kwa sababu ya unyanyapaa.
Beck alibadikwa jina la utani,"mzungu",sio tu na vitoto vyenzake,bali na wafanyi kazi pale shuleni.
Beck alilionea jina 'mzungu' fahari,labda kwa kutoelewa katika akili zake changa.
Beck alikuwa anakizungumza kiingereza mapuani.
Jina 'Mzungu' lilimfaa kwa kila njia.
Beck alikuwa na ulimi wa babake, na madaha ya mamake,Maria.
Alikuwa mzungu kwa ustaarabu wake.
Kubandikwa jina 'mzungu' haikuwa sababu ya pekee iliyowafanya Jason na Maria kukata kauli kumbadilishia shule.
Shuleni walimu  walimchukulia Beck kama mtoto mlemavu,licha ya weledi wake katika masomo.
Alikuwa wembe katika mtagusano wake na wenzake pale shuleni.
Beck alikuwa mtoto wa kipekee,'mzungu' pale shuleni.
Akawa kama kunguru mweupe miongoni mwa kunguru weusi.
Ukiwa mbali ungemtambua kwa utofauti wake wa rangi ya ngozi na urefu.
Alikuwa mlingoti kwa watoto wa rika lake.
Maria na Jason walionelea vyema kumpeleka shule iliyokuwa na watoto wa mataifa mbali mbali,wakiwemo zeruzeru.
Walipata shule moja ya kimataifa.
Kiwango cha karo kilikuwa cha juu,lakini kwao,darahimu haikuwa tatizo.
Mifedha waliiweka hadi mvunguni mwa kitanda chao.
Kwao pesa ilikuwa sehemu ya godoro.
Swali ni je,ulaliapo godoro la manoti,usingi huwa wa pono au mang'amung'amu?

Huku walikuwa na hakika kama mauti,kuwa,Beck angepata mazingira mema zaidi,kukulia na pia kusomea.
Jason alipendelea kumpeleka Beck asubuhi na kisha Maria kumchukua jioni kuelekea nyumbani.
Ikiwa wawili,hawakupatikana kwa sababu moja ama ya pili, walimtuma dereva kutekeleza shughuli hizo za uchukuzi.
Beck alikuwa ndiye ulimwengu wao,na dunia yao ilikuwa Beck.
Kila alipokohoa wote walimkimbilia kumjulia hali,kana kwamba walishindana kuonekana shujaa machoni mwa Beck.
Kwa Maria,Beck alikuwa 'kababa',kama alivyopenda kumwita wakati wa kumbembeleza.
Jason alilipinga jambo hili na kudai kuwa ni kumfanya mtoto wa kiume kuwa na 'umama'.
Kumfanya kuwa 'softie',hasikuwe na dhana ya simba dume.
Yote tisa,kumi ikawa,kama vigumu kama kaida,kumtenganisha mtoto wa kiume na mamake,ni kama kujaribu kumpigia mbuzi gita.
Mbuzi hatambui mdundo wala sauti nyororo ya mziki.
Kwa mbuzi,zote  ni ukelele za mee!zisizokuwa na maana yoyote.
Beckham 'Mzungu' aliishi na kusomea uzunguni.
Huku hakuchekwa wala kuonewa huruma.
Alikuwa na bahati kama aliyezaliwa Ijumaa,kwani hakukumbana na matatizo wakumbanayo,zeruzeru waliozaliwa au kukulia vijini.
Vijijini zeruzeru ni mkosi.
Ni ulemavu unaowabidi maskini, malaika wa mungu kulimbikizwa katika shule maalum za walemavu.
Vijijini zeruzeru ni vifaa vya kutumiwa na waganga na wachaei,wenye imani kuwa sehemu fulani fulani,zinaweza kutumiwa katika ushirikina.
Vijijini zeruzeru hawana mafuta maalum au miwani ya kuwakingia miale mikali ya jua.
Vijijini zeruzeru hupata upofu na saratani ya ngozi kutokana na miale ya jua.
Vijijjni zeruzeru huishi maisha ya upweke na kubaki kuwatazama watoto 'wa kawaida' wakicheza, wakabaki kushabikia tu!
Vijijini zeruzeru ni mayai yanayopata majeraha moyoni na usoni kwa nyingi kadhia.

Beck alizaliwa mjini.
Mjini zeruzeru ni 'wazungu'.
Wazungu waliokubalika na jamii iliyohamasishwa na somi.
Mjini zeruzeru ni watu.
Mjini zeruzeru husoma na hawana hofu ya kukatwa vidole kupelekewa waganga na warogi.
Mjini zeruzeru ni mawakili,wanasiasa na madaktari.
Mjini kuna mashirika ya kuwatetea na kuwalinda zeruzeru.
Zeruzeru kama jogoo la mjini,kijijini hawatambi.
Zeruzeru ni binadamu kasoro rangi ya ngozi.

**********************************
Kwa Suzzanna kuliwaka moto.
Subira ilikuwa ndio mwanzo imemtoka.
Licha ya kutumia kila mbinu,mtoto ,kwake,aliadimika kama shilingi ya kenya.
Bundi bado alikuwa mwenye matumaini siku yao ingefika.
Suzzanna alikuwa amekonda hadi kukondeana kutokana na sinikizo la mawazo.
Jamii haikuwa imemkubali mama bila mtoto.
Kumwita mwanamke asiyejaliwa mtoto,tasa;ni kosa la kijinai mbele zake Maulana.
Utasa ni ukosefu wa uwezo wa kuzaa.
Kuzalisha au kuzaa ni uwezo wa kuiotesha mbegu na kuwa mumea.
Mbegu hii inaweza kuwa wazo,kazi au hata mwana.
Kwa hivyo kumwita asiyejaliwa kupata mwana,tasa,ni kasumba finyu na iliyopotoka.
Utasa wa mja upo katika matunda ya bidii zake.
Neno 'tasa' lilimkosesha Suzzanna usingizi.
Kila alikopita alihisi mbingu zikimkejeli na kumsomea kuwa yeye alikuwa tasa.
Wambea wakambandika tope na kumwita 'Suzzana Tasa'.
Suzzanna alisononeka kwa kuiona familia yake haikukamilika.
Alijilimbikizia lawama za 'utasa',lawama ambazo pengine alimbebea mumewe.
Mwanamke ni kama ardhi ipokeayo mbegu na kisha kuiotesha.
Labda mbegu za Bundi zilikuwa hafifu,zisizoweza kuota.

"Fanya hivi Suzzie,jaribu kupata mtoto na mwanaume mwingine uone kama utafaulu!" sauti ya kishetani ilimpita mawazoni.
"La!la!la! Bundi ndiye wangu niliyemgoja kwa miaka mingi"
"Siwezi kumsaliti"
"What if he finds out"
"Na je,mtoto akitukia kufanana na mume wa kupanga,itakuwaje" sauti ya kimungu ilimkabili shetani aliyekita mizizi akilini mwake.
Sauti mbili zilizopingana akilini mwake zilimfanya Suzzanna kuhisi kizunguzungu.
Hali ilikuwa imezorota hadi kumlazimu kutumia tembe za kuvutia usingizi ili kuwahi usingizi.
"C'mon Suzzie,you can't beat yourself like this"
"Your are a doctor and you know the long term effect of this!"Bundi alimtuliza mkewe huku akimpapasa mabegani.
"Mpenzi wangu,familia ni mimi na wewe,tunatosha!Hatuwezi kumkosoa mungu.Akionelea vyema, na kwa wakati wake,atatupatia watoto." Bundi alisema.
"Tunaweza pia tukaadopt mtoto ikibidi!"
"Jipe moyo Suzzanna, ndiposa wakati ukifika uwe katika hali nzuri kisaikolojia na kiafya"
"Haya ni mawimbi yatapita tu!" Bundi alisema akiwa mwingi wa matumaini.
"Nakuskia mume wangu, lakini ni miaka kumi na...." Suzzanna alisikitika huku machozi yakimtoka na kulowesha kifua cha mumewe.
"Psss! Tosha sasa,ni wakati wa kuandaa chajio na nitakwandalia kile chako favourite!" Bundi alimwacha Suzzanna kwa tabasamu na kuelekea zake jikoni.
Kila alipokuwa na mumewe, mawazo yalimtulia.
Bundi alikuwa kiumbe mwenye imani na matumaini ya ajabu.
Ila alipokuwa pekee alisononeka moyoni.
Kuna waliomshauri kutafta msaada kutoka mahali mbalimbali.
Suzzanna aliwahi kunong'onezewa kuhusu nabii mmoja aliyeahidiwa maombi yake yangempatia suluhu.
Pamoja na kulipia kiasi kikubwa cha pesa,nabii mtapeli,alitaka kujamiana naye,eti kumfungua njia ya uzazi.
Suzzanna alidinda na kukaidi nabii ibilisi.
Yalimpita mawazoni, idadi ya wanawake waliotapeliwa na kuchafuliwa na nabii huyu,katika kiu chao cha kusikia kilio cha mwana,majumbani mwao.
Ni wazo lililochemsha hamaki zake.
Hamaki za jinsi manabii matapeli huwateka wanawake wanaopitia nyikani,kujinufaisha.
Shetani ni mtu?

Suzzanna alifikria kumshtaki, lakini akaogopa fedhea iliyoambatana na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuchapisha habari za kesi hiyo.
Wenye blogi hungojea matukio tata kama hayo,huyachapisha,huku wakiongezea chumvi na rojorojo.
Lengo lao likiwa kuwavutia wasomaji na hatimaye matangazo ya kibiashara.

Kuna wakati Suzzanna akikaa kitako na  kubebwa na mawazo yake na kurudishwa katika ile densi aliyoisakata na Jason,siku ya harusi yake na Bundi.
Alijaa shauku ya kutaka kuhisi yale mawimbi ya hisia nzito yaliomfagia,akitaka kujua yangempeleka hadi wapi, hatimaye.

"I would love to be in his hands again..kuna safari...ningeikamilisha?"
"Na je nikijaribu kupata mtoto na Jason.." Suzzanna alijiwazia huku akichezwa na tabasamu la kishetani mdomoni.
"Rishwa!.. Shetani ashindwe!What am I even imagining?" Alijikanya na kujichuna mkononi.

Ibilisi mkubwa zaidi ni mawazo ya mwanadamu.
Mara nyingi, vitendo vibaya huanza kwa mawazo mabaya.
Kabla ya kitendo,kuna kupanga.
Mpango ya fikrani.
Shetani ni kisingizio tu!
Dini iliwapa waja kisingizio cha kujifichia,waamuapo kuyatenda mabaya.
Shujaa mkubwa ni binadamu aliyeyamudu mafikra yake.
Binadamu mwenye uwezo wa kuyawaza mazuri wakati wote.
Mtu kama huyo hufuatwa na mema asilani.

SUZANNATempat cerita menjadi hidup. Temukan sekarang