Sura ya Nne

27 1 0
                                    

Mambo yalipochukua mkondo mpya kwa maisha ya Suzzanna,Fisi wengi waliomwaya mate kwa tamaa,waliikunja mikia yao kwa hofu.
Maisha yake yalikuwa yamegeuka na Suzzie akawa mwanamke gangari,aliyetambulika kwa kuhamasisha waja kuhusu akili afya(Mental health)

Sio tu wanachuo wenzake bali pia mabeberu wahadhiri waliuona umaarufu wake mpya kama kujaribu kucheza patapotea na kaa la moto,hatima ikiwa kuungua viganja vya mikono.

Kampeni hii iliyachukua maisha yake kwa kiwango kikubwa akawa hana wakati tena wa kushughulikia mitego ya majogoo wapanda mitungi.

Daktari Mathangi,kwa ubabe wake wa kufunza anatomia aliona ni vyema kuhimiza mkutano wake na kukifanyia upasuaji kiwiliwili cha Suzzie kuendelea kama ilivyopangwa.

"Tafadhali fika hotelini Sirikwe saa moja jioni bila kuchelewa."
"Nakuonya usiambatane wala kumwarifu mtu yeyote'
"Macho na maskio yangu yapo kila pahali kwa hivyo ukifikria tu,kuniseti nitafahamu" Suzzanna alioupokea ujumbe mfupi katika simu yake aina ya iPhone.

Jambo usilolifahamu ni usiku wa kiza.
Kile ambacho Mathangi hakuwa anafahamu ni kuwa jumbe zake zote pamoja na simu akizokuwa akipiga na kupigiwa zilikuwa zikirekodiwa na majasusi ili kumufumania.

Katika pekuzi pekua zao, majasusi walipata kuyafunua mengi kumuhusu Mathangi na washiriki wenzake wa kanisa la 'nionyeshe uchi nikupe alama'.
Waligundua kuwa Mathangi alikuwa mraibu mkubwa wa filamu za ngono.
Walipigwa na butwaa kupata kuwa alijirekodi katika video akila uroda haramu na wanafunzi,kisha kubadili sura akitumia 'photoshop' na kuwauzia wamiliki wa mitandao ya ngono na kujipatia pesa kugharamia maisha yake ya kifahari.
Pamoja na wenzake, walikuwa na kikundi katika 'whatsup' walichokibatiza,'Mafisi club'
Ni katika kundi ili ambamo walijadiliana na kujipiga vifua kuhusu mawindo yao.
Hapa na ni nakuli ya baadhi ya mazungumzo yao yaliyofichuliwa katika mitandao ya kikundi hicho:
Hakuna siri kati ya watu wawili eti!
Profesa Katunga:Unamuona huyu hapa,haikunichukua muda kumpandisha rinda kichwani!
Makataa: Lo! Wewe bwana umenishinda kwa kasi yako.
Katunga: Hivi daktari hijamtibu mgonjwa yeyote wa alama duni wiki hii?
Mathangi: hahaha,nyinyi mafisi wenzangu mutaivunja rekodi...
                : Nawaonya mukae kitako na      na Suzzie mpaka nimfanyie upasuaji mimi.Baadaye munaweza mukafanya reconstructive surgery.
Makataa: Haha
Katunga:Ila tunakupatia muda wa wiki mbili usipofaulu,nitakupiku barabarani.
Masikitiko yaliyoje kwa wasomi na wanaume wenye watoto wa kike majumbani mwao kushiriki ghasia kama hii?
Ama kweli dunia ilipasuka kitambo twangoja tu,siku ya kiama itumeze na kutuchomea jehanamu.

************************************
"So how has been life my dear?" aliuliza Hafsa baada ya kuchukua nafasi yake na kuketi katika hoteli mojawepo ya Java.
"Life has just been what it should be.. maisha tu!pandashuka za kawaida." alijibu Suzzanna.
Walikuwa wamekutana kujuliana hali .
Suzzanna alitaka kumshirikisha Hafsa katika kampeni yake naye Hafsa akitaka kupanga maojiano naye kwenye kipindi chake cha Runinga.
Hatimaye walikumbatiana na kupeana mikono,ikawa ni hali ya 'nikune nisikokufikia nami kikukune vile vile'.
Muumba humpatia mwanadamu majukumu asiyoyaweza ili kushirikiana na wenzake katika kuyatimiza.
Nani ana uwezo wa kupindua shingo kutazama makalio yake,asiumie ?

SUZANNAWhere stories live. Discover now