Sura ya Kumi na Tano

18 0 0
                                    

Ilikuwa imepita takriban miaka mitatu baada ya ndoa ya Suzzanna na Bundi kufungika.
Ni ndoa iliyokuwa na panda shuka kama ndoa nyingine yeyote.
Kwa kuwa mke na mumeke walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja, ilikuwa rahisi kwao kutangamana usiku na mchana.
Ili liliyeyusha mitafaruku yoyote ambayo, kwa wakati baada ya wakati ilizuka kati yao.
Walikuwa wafanyikazi wenza, marafiki na pia wapenzi wa dhati.
Ila palikuwapo na kisinyo miyoni yao.
Hawakuwa wamefanikiwa kupata mtoto licha ya kujaribu mara si haba.
Bundi alikuwa mwingi wa matumaini kuwa ingefika siku ambayo,kwa mipangalio yake Maulana,wangepata wana.
Kwa upande wake Suzzanna alikuwa ameanza kusinyika na kufa moyo.
Suzzanna alitamani sana kumshika mtoto wake,kumpepeta,kumbembeleza,kumpa nyonyo na zaidi kuitwa mama wa fulani.
Wanawake wa rika lake tayari walikuwa na wana wakubwa na kila alipowaona wakibeba au kuandamana nao,alisinyika na kulia kimoyomoyo.
"Mungu wangu,nijalie wangu mwana
Nimshike,ninyonyoshe,nimwone mwana
Niingiapo kwangu kiamboni,anikarishe mwana.
Waitwapo kina mama,jina niitwe kwa wangu mwana.
Wakimbiapo walozaa kuhudumia wao wana,nami niwe mbioni kumkuta wangu mwana.
Nakuomba mungu mzawadia wana,unipe wangu wengi wana.
Niijaze dunia,ulivyoagiza Adamu wengi apate wana.
Nipe shubra Maulana,ningojapo wangu wana.
Mimi mwanako mpendwa,niwalee wako wana."
Yalikuwa maombi yake Suzzanna kila siku.

"Subira huvuta kheri sweetie"
"Wakati wake mungu ukifika,tutapata watoto" Bundi alimliwaza mukewe kila aliposongwa na lindi la mawazo kuhusu hali yao.
"Nadhani uko impatient my dear,kuna watu hungoja hadi miaka kumi na..." Alisikika akimpa moyo rafikiye Hafsa.
"After all you have so many kids your helping in your arganization...God has already given you many kids that unalea kwa njia tofauti" aliongezea Hafsa.

Semi hizi zilikuwa na ukweli wake;bidii ya mja haindoi kudura.

Suzzie(alivyoitwa na marafikize)na  Bundi walikuwa wametafuta ushauri wa wataalamu wa uzazi na wakaonekana kuwa dhabiti kabisa katika njia zao za uzazi.
Pengine wasiwasi wake Suzzanna ulikuwa unazindisha ugumu wa kutungwa mimba.
Walikuwa wamejaribu vyakula mbali mbali,wakajaribu nyakati mbali mbali na hata mitindo mbalimbali,ila majaliwa yao hayakuwa yamewafikia.
Kilichobaki ni kuwa wengi wa matumaini na kuendelea kujaribu.
Maombi na imani ikawa lishe ya uhakika ambayo walikula kwa kila mlo.
Uzito wa hali hii ulimzidia Suzzanna kutokana na mtazamo finyu wa jamii kuwa, wakati wote ni mke ambaye huwa na hitilafu pasipolia mtoto kwenye ndoa.
Umbea ulienezwa kuwa pengine, Suzzanna aliavya mimba kisirisiri akiwa msichana na hivyo kuharibu kizazi chake.
Kuna wale waliofikria alikuwa tasa asiyeweza kujifungua,kinyume na matokeo ya uchunguzi na matokeo ya wataalam.
Jambo lilomtia moyo Suzzanna,ni kuwa Bundi na familia yake walimpa matumaini na hawakuwa wepesi kumlimbikizia lawama.

"Wala mimi sikukuoa huje uwe mtambo wa kutengenezea watoto"
"Hata tusipopata watoto,bado mapenzi yangu ni yale yale" Bundi alimwambia mara kwa mara.

Suzzanna alimwamini munuwe, lakini yale alikuwa ameyaona katika sinema za Kinigeria,zilimtia wasiwasi.
Mama mkwe kumsinikiza mwanawe kuoa mke wa pili kumpa mjukuu.
Katika tamaduni za kiafrika,wajukuu ni fahari kwa babu na nyanya,hasa katika miaka yao ya kutua jua.
Wazaziwe wa Bundi walikuwa wacha mungu na hawakuwahi kumsinikiza Suzzanna kwa vyovyote vile kuwapa wajukuu.

**********************************
Maria alijifungua kitoto kivulana,kieupe pepepe!
Ilikuwa furaha isiyo kifani kwake na Jason kukikaribisha kitoto chao duniani.
Kitoto ambacho bila shaka kingewaunganisha zaidi na kuotesha mapenzi yao.
Kama ilivyotarajiwa mitandao ya kijamii ilijazana habari na picha za majio ya Beckham.
Umbea pia ulitawala kuhusu sababu tofautitofauti za Beck kuwa mweupe, licha ya Maria na Jason kutokuwa weupe.
Kuna waliosema Jason alichezwa,kuna waliofanya uchunguzi katika koo za Maria na Jason kutambulisha uwepo wa uweupe,kuna waliosingizia kuwa Maria alikuwa ametumia tembe za ulimbwende kwa muda mrefu na kuleta hali hiyo.
Kenda,yote kumi,visababu tofauti tofauti,vilivyomtia Jason tumbo joto kutaka kuwa kama kweli Beck alikuwa mtoto wake.
Licha ya haya,Jason alikuwa tayari kumkumbatia mwanawe na kumpa mapenzi kama baba.
Jason alipanga kufanya uchunguzi wa 'DNA' bila kumhusisha Maria.
Ilikuwa muhimu kwake kufanya uchunguzi bila kuzua mfarakano wowote na Maria.
Jason pia alitafta huduma za mchunguzi wa kibinafsi ili kupepekua na kufahamu kama Maria alikuwa na uhusiano mwingine,huku akimpatia kisogo.
Uchunguzi wote ulileta matokeo yaliyofanana;Beck alikuwa mtoto halisi wa Jason.
Tashwishi ikamtoka na akavalia njuga za kumtunza mwana katika miguu yake yote miwili.

Nafuu ikamvaa na kukolesha zaidi uaminifu wake kwa Maria.
Lililobaki,likawa kutafta sababu za kisayansi kuhusu Weupe wa Beck.
Uchunguzi ambao kwake aliuona kuwa usiokuwa na maana yoyote,isipokuwa kama ungemletea Beck matatizo ya kiafya.
Palikuwa na haja ya kubaini kama Beck alikuwa Zeruzeru au Chotara.
Katika uchunguzi huu Jason alikusudia kumhusisha Maria.
Uzeruzeru au uchotara uliwezekana kutokea kwenye koo zote mbili.

**********************************
Chris kwa sasa alikuwa ashakuwa jogoo la uzunguni.
Labda kwa mihemuko ya kuweza kupandisha bendera, alijihusisha na mahusiano ya kuholelahole.
Mahusiano yaliyosababisha kutengana kwake na Rosata.
Chris alikuwa ameambukizwa ugonjwa wa uzunguni na kupata mtoto nje ya ndoa.
Ndoa yake na Rosata ilikuwa ya 'kuja tukae'.
Ndoa isiyo cheti chochote kudhibitisha uwepo wake.
Chris alikusudia kupata cheti kwani sheria iliwahitaji walioishi pamoja kama mke na mume kufanya hivyo baada ya miaka miwili.
Msukosuko wa ndoa yake uliwayumbisha kabla ya hayo kutimia.
Wakakubaliana kutengana kwa muda licha ya Rosata kuwa mjamzito.
Habari kuwa Chris alikuwa na 'baby mama' tena mzungu zilimpiga kama radi.
Aliona kuwa Chris alikuwa amemsaliti licha yake kusimama naye kidete wakati wa upungufu wake.
Alimuona Chris kama nyoka aliyemlelea kwake na kisha nyoka kumgeukia na kumuuma kisiginoni.
Ahsante ya punda ilikuwa mateke.
Kasumba za kizungu zilikuwa zimemkwama Chris akilini,asione alilolifanya kama sababu tosha ya kuwatenganisha.

"C'mon babe,it's not a big deal!"
"It's not like I'm leaving you"
"The baby can't be thrown away!"
"Ni makosa nakubali nilikukosea lakini" Chris alimsihi Rosata huku akirusharusha mikono mithili ya wale waimbaji wa mziki wa kufokafoka.

"Hold it on there"
"Hebu kwanza jisikize"
"Wewe huoni kuwa umeivunja imani yangu kwako?"
"Umeuvunja uaminifu wangu kwako?"
"Chris how could you...how could you do this to me?..to us?" Rosata alisema huku machozi yakimchezacheza machoni.
"I need a break, nahitaji kuwa peke yangu ili kuyatafakari haya yote"
Baada ya mabishano makali, Rosata alikusanya kila kilichokuwa chake na kuhamia kwa rafikiye, mfanyikazi mwenza.
Chris alisimama kwenye mlingoti wa lango kuu la nyumba yake na kumtazama Rosata akitokomea zake.
Alijihisi kama jibwa lililoponyokwa na fupa kinywani na kulitazama likibingiria hadi kuzama kwenye kidimbwi chini ya mlima.

"Nafikria hungetoka,je kutaendaje ikiwa huyo baby mama akipata mwanya na kuhamia kwa Chris?" Alimnasihi rafiki yake, Philomena, mara tu Rosata alipotua kwenye jumba lake.
"Right now,mimi sijali,I just need a break.I can't even stand him,sitaki hata kumuona!" Rosata alifoka huku akichimbia uso wake katika viganja vyake,kana kwamba alijaribu kuifuta picha ya Chris akilini mwake.
Kwa upande wake, Chris alimpigia simu rafiki yake,Japeth,na kumsimulia masaibu yaliyokuwa yamempiku.
Kwa wakati huu alikuwa amevubugia mvinyo aina ya 'John Walker' na kutapakaa chumbani,chupa kwa mkono mmoja na simu kwa mkono wa pili.
"Easy man,it's not like the earth has stopped spinning!Am joining you in a few." Japeth alikuwa na uwezo wa kufanyia utani hali yoyote; nzuri au mbaya.

"Men you still breathing?" Japeth alimtania Chris muda tu baada ya kuwasili,huku akiwekelea sikio lake kwenye kifua cha Chris.
"What's up my nigga!You crying because of a babe?"
Kwa wakati huu Chris alikuwa ameketi sakafuni kichwa kikiegemea kochi.
Japeth alikuwa Mumarekani Mweusi aliyejaa madaha na utani.
"That's trouble outa your life bro!Cheer up let's drink to this!" Alimnyanyua Chris na kwa mara ya kwanza, tabasamu ikaonekana mdomoni mwake.
Japeth alikuwa mtangazaji wa kibiashara na pia mchekeshaji mtajika.
Chris akimtarajia sana kumchangamsha kila wakati alipojihisi chini.
"What's wrong with these babes men?"
" There are 3 babes to one men!"
"Where do they expect them to go men?" Japeth alisema huku wakiangua kicheko na kupiganisha chupa walizokuwa kila mmoja ameshikilia mkononi.
"You know what?one babe leaves,go getcha the two lost!" Waliangua kicheko huku wakianza kudensi kufuatilia midundo ya reggae iliyokuwa kuwa ikipenyeza pembeni.







SUZANNAWhere stories live. Discover now