Sura ya Sita

30 2 0
                                    

Maria alipotemwa kutoka shule ya  Pingoni alijiunga na shule dogo kijijini,shule ya Mkiritini ambayo haikuwa shule ya bweni.
Baada ya matukio yaliojiri kule Pingoni,wazaziwe waliafiki kumpeleka kijijini kwa nyanyake,wakikusudia kumtenga na anasa za mjini.
Kwao waliiona kama shule ya kumrekebishia tabia.
Huku mashambani angefundishwa uwajibikaji na nyanyake na pengine mkondo wa maisha yake ungenusurika usimwelekeze motoni.
Maria alipinga kauli hii ya wazazi wake kwa mbinu na namna zote alizoweza.
Aliwahi kutorokea kwa rakiye kwa majuma mawili,ili kuwashurutusha wazazi wake kulegeza kamba.
Ila,juhudi zake ziliambulia patupu mithili ya kumfundisha kuku jinsi ya kutafuna kabla ya kumeza.
Babake,Mubabe alitumia idara ya ujasusi kumfichua alikotorokea,ila akamwacha kujibarizi kwa wiki mbili, angalau hasira zimtue.
Mubabe alikuwa mzee mwenye msimamo dhabiti sio tu kwa siasa bali katika maamuzi yake yote maishani.
Filosofia hii ulimfanya kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa na biashara kule nchini mwake.

Maria alielekea shuleni Mkiritini akiwa shingo upande na kufura kama kaimati.

"Ewe mamangu,nakuomba kuyachuchukulia mambo haya kwa urahisi na kama yatakayokufaidi wewe." mamake mzazi alimrai.
Maria aliyatia maskio yake nta,na kuigiza ububu,akawa hambiliki hasemezeki.
Akajimwaya safakuni na kubaki kununa ja kitoto cha chekechea.
"Deal with this..I can't" Mubabe alisema huku akishika tama na kutokomea zake.
Kibarua cha bembelezabembeleza mwana,akamwachia bibiye.
"Ee mwanangu, nakuomba utulize roho!"
"Kwa nyanyako sio jela!Tutakuwa twaja kukuona na pia kuwasiliana kila siku."
"Hii si shule ya kulala,kwa hivyo utakuwa huru kuliko ulivyokuwa kule Pingoni!"
"Shusha roho mwanangu usimzidishie babako presha!
"Ama wataka kumua babako?" Bi.Mubabe alitumia mbinu zote kumshawishi bintiye

"La mama!Siwezi nikamua babangu, Siwezi...naomba samahani kwa ujeuri wangu.. nitaenda..na naihidi kurekebisha tabia" Maria alisema huku akipiga magoti mbele ya mamake.
Macho yake yaliloa machozi.
"Sawa mama..inuka..ebu inuka" Mama mzazi alimsaidia mwanawe kusimama na kisha kumkumbatia.
Waliketi kwenye kochi na kupiga gumzo huku wakicheka.

Bi.Mubabe alikuwa na kohozi lililomkaba kooni na alihitaji kulitema.
Je Maria angemsamehe?

"Kwa niaba ya babako, nakuomba msamaha Maria,nakiri ni kosa letu kukutelekeza lililokufanya ukawa ulivyo"
"Babako alishughulika na siasa nami nikashughulika na biashara tusipate wakati wa kukulea na kuwa naye"
"Tukakuachia yaya na telivisheni kukulea" Bi.Mubabe alisema kwa sauti ya masikitiko.
"Laiti ningalijua..ningalijua kuwa mifedha tuliotafuta usiku na mchana,haingechukua majukumu  yetu kwako kama wazazi." Machozi yalimtoka na kutengeneza njia mbili mashavini.
Maria alimuegemea mamake na kumpapasa mgongoni angalau kumtuliza.
"Nakuahidi binti yangu,sitokuwachilia tena na nitakuwa nawe katika safari hii." Mama mzazi majuto yalikwama kooni.
"Ni sawa mama,ulilolifanya pia lilikuwa la muhimu,kuhakikisha sikukosa chochote nilichokihitaji.....lakini nilikumiss mum" Maria alijiunga na mamake katika karamu ya machozi.
Kutokea hapo wote wawili walizungumziana kwa kupanguzana machozi na kufuta kamasi.
"Nafurahi kuskia ukiniomba msamaha na nakupenda mum"
"Nawenda sana mukiwa na dad" walikumbatiana na kulia hadi kupata lepe la usingizi.

Bi.Mubabe alikata kauli kuandamana na Maria hadi kijijini na kubakia huko kwa muda ili kuwa karibu na bintiye.
Jumatatu iliyofuatia,mama na bintiye walijifunga kibwebwe cha kuelekea kijijini Mkiritini, tayari kuyakumbatia maisha mapya na matulivu,ya mashambani.
Kinyume na mjini, Mkiritini kulijaa miti na visima vya maji safi.
Kwake Bi.Mubabe ilikuwa kama kuzifuatilia nyayo za utotoni kwani huku huku ndiko alikozaliwa.
Baada ya kupakia kila walichohitaji,walisimama kando ya gari la prado,jeusi tititi! tayari kuliabiria kwenye  safari yao.
"Hakikisha,hukosi kumeza dawa zako! Nitakuwa nakupigia kuhakikisha unazitumia."
"Nimempa Zipora masharti kuhakisha hutakosa lolote wakati ambao sitakuwepo" Mke alimwakikishia mume huku wakisimama bako kwa bako.
"It can never be the same without you han!but nitajaribu" Mubabe alimuaga mkewe.
Zipora alikuwa kijakazi wao waliyemwajiri akiwa msichana mdogo na sasa alikuwa mama wa makamo.
Ni Zippy aliyekuwa ametwikwa jukumu la kuwa mama na baba wa kambo kwa Maria,wazazi wakiwa 'too busy chasing money'.
Safari ya kwenda kijijini iling'oa nanga,binti na mamake wakawa na mengi ya kuzungumza safarini.

SUZANNAWhere stories live. Discover now