Sura ya Nane

18 1 0
                                    

Mathangi alipofahamu kuwa majasusi walikuwa karibu kumufumania,alichana mbuga kwa mara nyingine na kuelekea Sudan Kusini ambako kwa wakati huu alianzisha zahanati katika mji wa Yebei.
Ni mji ulioko eneo ambalo ni gumu kufika, yakawa maficho mazuri kwake.
Akiwa Uganda makachero walianza kumfuata mara tu alipowasiliana na familia yake kwa mbinu ya rununu.
Alikuwa akitumia simu za marafikize au wafanyikazi wake ili kufunika sura yake halali.

Yebei ni eneo ambalo mitandao ya simu ni hafifu na kuna matumizi makubwa ya simu zinazotumia sateliti.
Simu za aina hii ni vigumu kufuatiliwa kuliko simu za kawaida.
Yebei pia ni mji uliomilikiwa na mibabe wa kivita, hivyo kwa kutoa mulungula,ulinzi wake ulikuwa thabiti.
Huduma za afya zilikuwa afifu katika nchi nzima na kupelekea zahanati yake kufurika wagonjwa furi furi,kutibiwa ndwele za aina mbalimbali.
Kulikuwa visa vingi vya utapia mlo miongoni mwa watoto,vikifuatiwa kwa karibu na vidonda vya kupigwa risasi.
Wagonjwa wengi walikuwa ni chumo kubwa kwa Mathangi.
Baada ya muda,aliweza kushikamana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kupanua zahanati yake kuwahudumia wagonjwa zaidi.
Aliwaajiri madaktari wengine na pia wahudumu mbalimbali.
Ni pale alipopatana na Zuhuria, daktari kutoka Uganda Magharibi,mwenye upole wa kobe na tabasamu la kumfanya Askofu wa Kikatoliki kuisaliti imani yake.
Kama wasemavyo wenye ,'Mapenzi ni kama jeraha utosini,hayafichiki'
Haikuchukuwa muda mrefu kabla ya mbegu ya mahaba kumea kati ya Mathangi na Zuhuria.
Yakawa mapenzi kati ya mtu na bosi wake.
Yalianza kwa chekacheka katika harakati na kupitana pitana pale kazini.
Ikafuatia mitagusana na busu za kujifichia ofisini.
Kujamiana  haraharaka kukashika moto nyuma ya pazia kule zahanatini.
Waliwahi kufumaniwa kwenye chumba cha kufanyiwa upasuaji na daktari mwenzao.
Ilikuwa si aibu ni fedhea.
Mwishowe wakati ilishindikana kuyaficha mapenzi yao,wakayaweka kandamnasi na kuanza kuishi pamoja.
Mathangi akawa ameoa mke wa pili kule Sudani Kusini.
Kwa kuwa fedha zilikuwa nyingi wakati ule,aliweza kuwakimu familia yake alioasi na kuwacha nyumbani.
Alitumia watu wengine kuwasiliana na kutuma pesa kwa familia hii ya kwanza.
Hakuwafafanulia aidha wanawe ama mkewe alikokuwa akiishi au kuwafichulia kuwa alikuwa na mke wa pili.

Mathangi na Zuhuria walijaliwa watoto wawili.
Wakawa familia kamilifu isiyo na bugudha yoyote.
Maisha yakawa raha msaterehe.
Ila kwake Mathangi, mpango wake wa kwenda ughaibuni hakuwa ameusitiza.
Ni safari aliyoidhamiria kwa udi na uvumba.
Alidhamiria kuwalea watoto wake, wawili,wafikie miaka ya kubaleghe,kisha kusingizia kwenda kwa masomo ya juu.
Hakuwa na shaka kwani angemwachia Zuhuria, biashara yao ya zahanati kuiendeleza.
Alikusudia,mara tu akitulia na kukita mizizi ughaibuni,kuwachukua familia yake ya Kenya na kuishi nao.
Kwa Zuhuria angewacha kilio na kwa Bi.Mathangi alikusudia kicheko.
Alitumahi pindi muda ulivyosonga, makachero wangechoka kumuandama na kuifunga faili yake.
Kama ingebidi angetumia hongo kuregeza kamba ya sheria.
Chungu alikuwa amekiinjika tayari kuipika mipango yake.

*********************************
Suzzanna kwa sasa, alikuwa keshahitimu chuoni na alikuwa katika mazoezi yake katika hospitali ya rufaa iliyokuwa imeshikamana na chuo chenyewe.
Alidhamiria kuzamia kwenye matibabu ya kijinsia.
Ni katika idara hii alikokuwa akiyafanya mazoezi yake ya mwisho,kabla ya kupewa cheti cha kuwa daktari kamilifu.
Pamoja na matibabu, shirika lao la kuendeleza afya ya kiakili lilikuwa limeshamiri.
Bundi alikuwa kwenye mwaka wake wa mwisho kusomea saikolojia.
Bundi alikuwa tayari kapata ajira pale hospitalini kama mshauri wa kisaikolojia.
Visa walivyokumbana navyo kuhusu dhuluma kwa kina mama na watoto viliwashusha mioyo.
Kulikuwa na visa vingi vya kunajisiwa,kulawitiwa na majereha kutokana na fujo za ndoa.
Cha kusikitiza zaidi,wadhulumu walikuwa ni watu waliojulikana na kuaminiwa na wadhulumiwa.
Wengi wa wanyama hawa kasoro mashetani, walikuwa ni ndugu na jamaa kwa wadhulumiwa.
Suzzanna na Bundi walikusudia kuanzisha elimu kwa shule zote za msingi kuhamasisha watoto wakiwa wachanga jinsi ya kugundua hatari na kujiepusha na mazingara yaliowaweka hatarini.
Kwa kushirikiana na Hafsa na washika dao wengine,tayari walikuwa wameanzisha kampeni ya kuisindikiza wizara ya elimu kuratibu  na kuyaweka mafunzo haya kakita mtaala rasmi wa elimu nchini.
Yalikuwa maoni na imani yao kuwa kuwapa watoto ufahamu kuhusu mahusiano ya kimapenzi,kungewawezesha kuwa na nafasi bora zaidi kujikinga.
Idadi ya visa vya mimba za mapema zingepungua kwa idadi kubwa.
Kutokana na tafiti zao, ilikuwa kisa cha mbuni kukificha kichwa chake mchangani,kwa baadhi ya wadao na wazazi kupinga mafunzo ya masomo ya kijinsia shuleni huku wakiwaacha watoto kupata masomo yayo hayo kutoka kwa watu wanaowapotosha.
Wengi wa walimu hawa badia ndio huwadhulumu watoto hawa wanapogudua sitofahamu yao.
Maendeleo ya tekinolojia pia yamewezesha kupitia kwa mitandao, watoto kuweza kuwa hatarini zaidi kupotoshwa na watu wenye kusudi mbaya.
Kwao walionelea bora kumkunja samaki angali mbichi na kinga ni bora kuliko tiba.
Yalikuwa matumaini yao kuwa ombi lao lingekubaliwa.
Mgema alikuwa amependekeza kuunda katuni ambazo kwazo,ujumbe huu ungepitishwa kwa watoto kama njia burudani.
Kupitia kwa kamputi yake ya kopyuta na tekinolojia, alikusudia kutoa huduma hii kufanikisha mpango huu.

Mgema baada ya kufanya kazi kwa muda wa miaka kumi, alianzisha kampuni yake ya komputa na tekinolojia.
Ni kampuni iliyonawiri na kuwaajiri vijana wengi chipukizi wahadisi wa sayansi ya tarakrishi.
Pamoja na huduma nyinginezo, kampuni hii ilijishughulisha na uundaji wa katuni kwa lugha ya kiingireza, kiswahili na lugha nyinginezo za makabila tofauti tofauti.
Ulikuwa uvumbuzi wa kipekee ulioyavutia makampuni mbalimbali kufanyia matangazo ya kibiashara.
Mgema alikuwa bado anatumia madawa kupunguza makali ya maradhi yake ya UKIMWI.
Ni katika hospitali alikoenda Mgema, kliniki ya kuhudumia wagonjwa wa UKIMWI,alipopata na mhudumu kwa jina Flora.
Flora alivutiwa na uchangamfu na ucheshi wake.
Walifunga pingu za maisha na kujaliwa kupata mtoto mumoja.
Wakawa kielelezo cha kupigiwa mfano kuonyesha kuwa iliwezekana kwa wagonjwa wa UKIMWI kuishi maisha ya kawaida na hata kupata watoto kwa njia salama bila kuwaambukiza virusi.
Flora alikuwa haishi na virusi na alikusudia kuupiga vita ukiritimba ulioambatinishwa na ndwele hili.
Uchesi na uchangamfu wa Mgema ulimwezesha kuwavutia vijana kwa jinsi alivyoimudu lugha ya sheng.
Akawa anashirikishwa na Suzzanna katika mihadhara, hasa iliyohusu swala nyeti la ushoga na usagaji.
Ni tamaduni potovu zilizoigwa kutoka kwa watu waasi wa dini na maumbile ya mungu.
Ni kinyume na tamaduni za kiafrika.
Mbona Waafrika tuwe watu wa kuiga tamaduni za watu wengine?
Mbona wao wasiige tamaduni za Waafrika?
Ni kasumba za kikoloni zilizowateka Waafrika akili na kuwafanya kudharau tamaduni zao na kuchukulia kuwa;'cha mgeni ni bora kuliko cha mwenyeji'
Katika mazungumzo yake Mgema alipenda kutoa mfano wa vifaa vya kielekitoniki ambavyo huwa na matundu ya kike na kiume ili viweze kushikanishwa na kufanya kazi ilivyostahili.
Kiume hakiwezi kuingiana na kifaa kingine chenye tundu la kiume.
Ni maumbile na ni mpango wa mungu.
Mbona wadamu kujaribu kuasi mantiki ya mfumo huu wa kimaumbile?
Ufahamu ni silaha kali.
Kwa kuwahamasisha vijana kuhusu mambo haya ni kuwapa silaha kuweza kufanya maamuzi ya busara maishani.
Mchelea mwana kulia, hatimaye hulia yeye.

SUZANNAWhere stories live. Discover now