Akiwa amepitiwa na usingizi ndani ya nondo za gereza Tarick anasikia nyayo za mtu zikimsogelea Taratibu. Huku akiwa hoi kutokana na uchovu wa kipigo kizito alichopewa na kikosi cha usalama wa taifa kitengo cha upelelezi Tarick anajivuta taratibu na kugeuka nyuma ili kumtizama mtu aliyekuwa akimsogelea, Baada ya kufumbua macho kwa shida Tariki anamtambua msichana mrembo Brenda akiwa mbele yake, Akiwa mtu mwenye majonzi Brenda anachuhumaa pale alipokuwa Tarick na kudondosha machozi huku miguno ya kilio cha uchungu ikisikika.
Kilio hicho kina mfanya Tarick Kuinua sura yake na kumtizama Brenda. Huku akitoa sauti kwa shida na uchungu Tarick anasema “Naona umeamua kuja kunisanisanifu, na kuibariki safari yangu ya kuelekea akhera……. Mlichokuwa mmedhamilia kimeshatimia nini unataka tena…….! ” maneno hayoo yanampa simanzi nzito Brenda na kumfanya kububujikwa na machozi yanayoambatana na sauti nyepesi ya kilio, Kwa uchungu Brenda anasema,”Please Tarick usiseme hivyo….. I Love You Tarick , and I promise to be With you until the End”. Huku akububujikwakwa na machozi Tariki anamkatisha Brenda na kusema,”What Kind of Love is this?........... Eeh! Nilishakwambia toka mwanzo kwamba ukweli wa mapemzi yako kwangu ni kuachana na mimi, Hatuwezi kulazimisha mapenzi ikiwa hatuendani kwa hali wala Mali. Huu ndio ulikuwa mpango wako Brenda……… Haisaidii kitu kuendelea kunikashifu kuwa unanipenda wakati nimesha hukumiwa kifo……… Haisaidii kitu kiniambia utakuwa na mimi mpaka mwisho wakati nitanyongwa pekeyangu…… Umekuja kunikejeli Brenda……! Mungu awabariki ……” maneno hayo yanazidi kumtia simanzi na kummaliza nguvu kabisa Brenda. Brenda anafuta mchozi na kusema,”Usiseme hivyo Tafadhari,……… ”. Kabla hajanyanyua kinywa kusema kauli yoyote Askari anampa taarifa Brenda kuwa muda umeisha, Huku askari akiwa anamsindikiza Brenda kutoka nje alitoa sauti kwa uchungu akisema’’sitakuacha Tarick……… Sitakuacha peke yako Tarick niamini Tafadhari………”.
Akiwa amedondoka pale chini Tariki alionekana mtu aliye Ghubikwa na mawazo, huku fikra nyingi zikiwaza jinsi atavyo muacha mama yake ambaye katika kipindi hicho alikuwa akimtegemea yeye. Usiku kucha Tarick Hakuweza kupata usingizi, alikuwa mtu aliye jawa na mawazo.
Kesho yake alfajiri Tariki alishtushwa na maji ya baridi yaliyommwagikia na kumpa ukakasi mkubwa kwenye majeraja ya mateso yaliyomjaa mwili mzima.
Kunyanyua sura yake juu ili atizame ni nani iliye kuwa mbele yake, Tarick anamuona Profesa Rweyemam akiwa na wapambe wake, Kwa Dharau na nyodo anasema,”Upumbumbavu wako umekugharimu sana…… Nasikitika sina cha kukusaidia,” Profesa Rweyemam ananyamaza kidogo na kuendelea,”ungetumia weledi wako kidooogo… ungekuokoa usiingie katika dhahma kubwa kiasi hiki mpaka inakugharimu uhai wako”. Maneno hayo yanampa ghadhabu Tarick anajivuta taratibu kwa kutumia nondo za gereza na kusimama, kisha huku akionesha kutokuwa na hofu hata kidogo Tarick anamjibu,”Nilishawahi kukwambia kuwa elimu yako bado haijakutoa kwenye ujinga……… hapa hakuna cha muhimu unachofanya zaidi ya kudhihirisha wasifu wa ujinga na upumbavu wako unadhani pesa na wadhifa wako unaweza kukufanya uishi milele? unajidanganya wewe ...” . Maneno hayo yanamtia hasira Professa Rweyemam Anamkatisha Tarick kwa Ghadhabu, “Shenzi wewe…… hukumu ya kifo imekupendeza… ”. Rweyemamu anaondoka mahali hapo kwa Hasira.
******************************************************************************
Msichana mrembo na aliye umbika kwelikweli Brenda, kitendo cha kuelekea kumpoteza Tarick kilimchanganya kwelikweli, upande wake mapenzi juu ya Tarick yalimzidia kiasi kwamba aliona kuwa asingeweza kabisa kuishi bila ya Tarick. Akiwa ametoka kuamka mrembo huyu anaonekana kuwa bize akitafuta simu ambayo haipatikani. Brenda anaendelea Kupiga Simu hiyo bila kuchoka. Baada ya kuhangaika kwa muda simu hiyo inaita. “Kitendo cha simu hiyo kupekelewa tu Brenda anaangua kilio, anasalimiana na mtu aliempigia simu lakini anashindwa kuzuia hisia zake kwa kuendelea kulia”.
“Brender Stop crying…… ujue unanipa hofu, kwani kunatatizo gani? ” maneno hayo yanasikika kutoka kwenye simu. Brenda anaonekana kujikaza kisha anajibu,”Tarick is going to Die….. Tarick amehukumiwa kifo Frank…… plea…… nahit ___ nahitaji msaada wako please”. Maneno ya Brenda yanampa mstuko Frank “Mbona sikuelewi Wewe! Kwani nini kimetokea? Tarick amehukumiwa kifo na nani!? Na amefanya kosa gani hasa?”. Maswali hayo ndio yanasababisha Brenda ashindwe kabisa kuongea na kuishia kulia kwenye simu.
Aliyepigiwa simu na Brenda ni rafiki kipenzi wa Tarick, kwa msisitizo wa maneno ya Kiswahili nikisema rafiki wa damu au rafiki wa kufa na kuzikana naweza kuwa nimeelezea kwa ufasaha zaidi uhusiano baina ya Tarick na Frank, maarufu kama samba jina ambalo alipewa kutokana na ujasiri mkubwa na umakini wa hali ya juu aliokuwa nao wakati wa ukuaji wake, vijana hawa wawili waiishi kama ndugu pekee, undugu ulioletwa na urafiki mkubwa baina yao, hivyo kauli tata zilizohusisha kifo cha Tariki, Zinatikisa fikra za Frank kwa namna ya kipekee kabisa.
Frank yeye alibahatika kupata ajira kwenye moja kati ya makampuni mashuhuri ya mawasiliano nchini south Africa inayojulikana kama Vox Telecom. Frank alikua ameajiliwa kama Technical Engeneer kwenye kitengo maalum cha kupambana na Aina mbalimbali za wizi unaotumia mtandao. Taarifa hizo tata kutoka kwa Brenda zinamfanya Frank apige simu ya Tarick Bila mafanikio, Bila kukata tama ya kutaka kujua kinachoendelea Frank anaamua kumpigia Mama yake na Tarick.
Baada ya salamu mama nae akionekana mwenye huzuni kubwa anajikaza na kumuelezea Frank kilichotokea. “Frank mwanangu Tarick mwenzio amehukumiwa kunyongwa… wanasema yeye alihusika kwenye mlipuko uliotokea Arusha mwezi juni mwaka jana, walimkamata akiwa hotelini na Yule binti Brenda huko huko Arusha, na…… na……”. Sauti ya mama inafifia ghafla kwenye simu na kukatika kabisa, Mapigo ya Mama yanaenda mbio kisha anadondoka na kupoteza Fahamu.
Ukimya wa mama unamstua Frank, anaita kwa hofu na mstuko “mama……… Haloooo, Halo ….. Mamaaaa”. Frank anaamua kukata simu. Mahali alipokua anazungumza na simu nikatika eneo la mapumziko la kampuni yao, Frank anatoka kwa kasi mpaka kwa bosi wake aliekuwa akisimamia kitengo chao, kisha huku akionekana kuwa mtu mwenye presha anasema,”Lodrick ! inabidi nisafiri kuelekea Tanzania Leo”, kwa mshango bosi wake anamuuliza,”Vipi mbona hivyo………! Kuna nini?”. Frank anamtizama na kumjibu,”Lazima niondoke kunamatatizo”. Bosi wake anasema,”Lakini huu sio utaratibu frank, hebu tuliza akili, then andika barua ya kuomba ruhusa”. Frank anamtizama kwa umakini mkubwa bosi wake kisha anamjibu,”sihitaji kumuomba ruhusa mtu yoyote, ila hii inatosha kuwa taarifa ya safari yangu”. Bosi anaonesha kuhamaki na kumsihi Frank,”Lakini Frank…… Subiri tuone ni jinsi gani tutashirikiana na wewe kwenye tatizo lako…”, Huku akigeuza na kuondoka Frank anajibu,”Nashukuru…… Nikihitaji msaada nitawasiliana na wewe”
Nini Frank anafikiria, Je Kuna Msaada wowote anaweza kutoa kuzuia hukumu halali ya mahakama na hatimae kumsevu Rafikiyake?.
Usikose kufatilia Sehemu ya pili ya Tamthilia hii ya Kusisimua inayokujia kwa jina la The second Door. Pia unaweza kuungana na wasomaji wengine wa simulizi hii kupitia ukurasa wetu face book
www.facebook.com/EAstoryforeveryone
YOU ARE READING
The Second Door - Episode 1
RomanceThe second Door ni simulizi yeny mikasa na matukio ya aina yake, Ungana na zaidi ya wasomaji 10,000 wa simulizi hii kupitia jumuia yetu ya WattPad, Mtandao wa JamiiForum na Kurasa yetu ya FaceBook. usikubali kupitwa na mikasa hii ya kusisimua