Habari gani marafiki? Ni wasaha mwingine murua tunaoungana pamoja katika mkasa wa tamthilia ya kuvutia, si nyingine bali ni Tamthilia ya The second door.
Katika episode namba 8 tuliishia makaburini ambako Tarick na Roby walifika kwa ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya mpendwa wao Frank. Baada ya kutoka eneo lile la mazishi, sasa kwa Roby ilikuwa ni zamu ya kumalizia kibarua cha kumkabidhi Brenda kwa Rweyemamu. Hili halikuonekana kama lilikuwa zoezi kubwa kwa Roby. Roby anamrudisha Tarick nyumbani kisha anaelekea hospitali kwa ajili ya kuangalia utaratibu ambao atautumia kumpeleka Brenda kwa Rweyemamu bila kumsababishia matatizo. Roby akiwa ofisini kwakwe anajaribu kuweka mambo ya kikazi vizuri huku akiplan jinsi ya kumrudisha Brenda kwa Rweyemamu.
Muda wa masaa ya kazi unaisha Roby akiwa anarudi nyumbani anaamua kupitia kwa wakala wa usajili wa namba za simu akiwa na malengo ya kwenda kusajili line atakayoitumia kuwasiliana na Rweyemamu, Roby anafanikiwa kusajili namba kwa utambulisho feki, kisha kutokana na muda kuwa umeenda sana anaamua kurudi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani wakiwa pamoja na Tarick Roby anasema, “Tarick ujue umefanya uamuzi mgumi sana, na laiti ingekuwa hiari yangu ningekusafirisha hata kwa viboko ukaishi nje ya nchi”, Tarick anajibu, “nikweli kabisa unachosema dokta, lakini kunamsukumo mkubwa sana kutoka moyoni mwangu ukinilazimisha niendelee kuishi Tanzaia”. Roby anashusha pumzi na kusema, “ok! Tatizo linakuja, ni jinsi gani tutaficha identity yako” baada ya swali hilo Tarick anajibu, “Naweza hata kutumia ndevu za bandia ili nibadilishe muonekano wangu.” Baada ya Tarick kuongea maneno hayo Roby anatikisa kichwa akiashiria kutokubaliana nae kisha anasema, “Tarick! Utambulisho wako ni muhimu kuliko sura unayoifikiria. Jina lako, umezaliwa wapi, umesomea wapi, wazazi wako, passpot, vitambulisho navitu vingine vyote lazima vikutambue, ukishindwa kuonesha vidhibitisho hivyo kunamambo mawili, pengine sio mtanzania au utajilikana kuwa ni wewe unaetafutwa umeamua kuficha utambulisho wako.” Roby na Tarick wanajadili kwa muda mrefu bila kupata jibu.
Ni siku nyingine tena Asubuhi na mapema mheshimiwa Proffesa Rweyemamu akiwa ofisini kwake anapokea simu kutoka kwa mtu asie mfahamu, simu hiyo anayopokea Rweyemamu inampa taarifa za kumtaka afike kwenye jengo la Haidary Plazza posta kwa ajili ja kuchukua mzigo na taarifa za muhimu. Rweyemamu anauliza maswali mengi na kuhoji sana juu ya wito huo lakini hakuna hata swali moja linalopata jibu. Mwisho simu hiyo inamuelekeza kuhakikisha anafika hapo akiwa peke yake. Kutokana na msisitizo uliooneshwa na simu ile Rweyemamu anaamua kumtuma mfanyakazi wake kwenda kusikiliza wito huo, na kwakuwa hakuwa na uhakika kuwa wito huo ulikuwa unahusiana na nini Rweyemamu anahofia kumtuma peke yake mfanyakazi wake hivyo anaagiza na askari wawili ili wawe wanamfatilia mjumbe huyo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wake.
Mpenzi msomaji wito huu wa ghafla aliokuwa ameupokea Rweyemamu ilikuwa unatoka kwa Roby na ulikuwa na lengo la kumkabidhi Brenda. Bila kujua Rweyemamu anamuelekeza mfanyakazi wake mpaka kwenye sehemu ya juu ya jengo hilo ambako aliambiwa angekutana na mtu anaempigia simu na kumkabidhi vitu alivyo muahidi. Roby kwa kuwa alikuwa hajulikani na mtu aliekuwa akiongea nae kwenye simu anaamua kutumia ujanja wa kumtanguliza eneo la juu kwenye jengo hilo sehemu ambayo inamgahawa, baada ya kuwasiliana na Rweyemamu, na Rweyemamu kumhakikishia kuwa tayari alikuwa amefika eneo hilo, Roby nae anapandisha ili kukutana nae. Kabla hajatokeza, Rweyemamu anawatumia meseji wale askari waliokuwa wakiongozana kwa siri na mtu aliyemtuma na kuwapa namba aliyokuwa akitumia Roby kisha anawaambia waibip ikiita wamkamate, na kumpeleka kituoni kisha wamtaarifu.
Huku nyumbani alikoachwa Tarick, Roby alikuwa amemuagiza Zubery afike nyumbani hapo kwa ajili ya kuchukua Pesa azipeleke kwa mama, maagizo ya pesa hizo Roby alikuwa amemuachia Tarick, Zubery anafika nyumbani kwa Roby na kupokelewa na Tarick, kwakuwa Tarick alikuwa peke yake ndani ya nyumba hiyo Zubery anaamua kukaa kidogo ili kumpa kampani, Tarick. Zubery hakuwa mgeni kabisa ndani ya nyumba hiyo, anaweka movie kisha wanaendelea kutizama na Tarick huku wakipiga story. Baada ya story za hapa na pale walijikuta wakizungumzia kutafutwa kwa Tarick. Tarick haoneshi wasiwasi wowote kwa Zubery kwani aliamini kwa moyo alionao kaka yake sio rahisi Zubery akafanya jambo lolote baya.
YOU ARE READING
The Second Door - Episode 1
RomanceThe second Door ni simulizi yeny mikasa na matukio ya aina yake, Ungana na zaidi ya wasomaji 10,000 wa simulizi hii kupitia jumuia yetu ya WattPad, Mtandao wa JamiiForum na Kurasa yetu ya FaceBook. usikubali kupitwa na mikasa hii ya kusisimua