The Second Door- Episode 7

115 1 5
                                    

Hii ni The second Door Tamthilia inayoelezea mkasa wa kuburudisha, kuelimisha na wakati mwingine kusikitisha kabisa huku mkasa huu wa kipekee ukikuacha na mafunzo mbalimbali katika maisha yetu ya kawaida. Msamiati ndio mwandishi ninaekuletea simulizi hii uipendayo na kwa namna ya kipekee kabisa nikukaribishe katika episode no 7 ya simulizi hii.
Kabla hatujaendelea, kwa dhati kabisa naomba niwatake radhi sana kwa mistake nyingi za uchanganyaji majina zilizokuwa zimejitokeza katika episode iliyopita, lilikuwa ni tatizo lililotokana na kuandika episode ndefu, hivyo ikapelekea nikashindwa kufanya uhariri kwa makini.

Tunaendelea… katika episode ya 6 tuliishia kwa kumuona Robi akishindwa kuwahadaa wale maafisa wa gereza ambalo amefungwa Tarick, kisha aliamua kuondoka na kurudi nyumbani. Leo asubuhi na mapema, Roby akiwa anamalizia kujiandaa kwa ajili ya kuendelea na pilika pilika za kutwa nzima, Roby anapoke simu kutoka hospitali alipokuwa amelazwa Brenda na kuambiwa kulikuwa na taarifa za mgonjwa wake hivyo anaombwa afike hapo mapema. Taarifa hizi zinamshtua kidogo roby akidhani kuwa pengine hali ya Brenda inaweza kuwa imebadilika ghafla au inawezekana amepoteza maisha. Asubuhi hiyo licha ya Roby kupata taarifa za hospitali, Roby anaamua kuziweka kando na kuwahi gerezani ambako leo amedhamiria kumfikia Tarick mapema kabisa hata kabla wafungwa wanaokwenda mahakamani hawajachukuliwa. Roby anatoka nyumbani kwake mapema kabisa akiwa amewahi moja kwa moja kuelekea Gerezani.

Ndani ya siku hiyo, familia ya Brenda inakubaliana kuwa Dada yake aende akakae nyumbani kwa Brenda kwaajili ya usalama wakati wakisubiria siku tano walizokuwa wameahidiwa na Rweyemamu zikamilike. Ikiwa ni siku moja tu tangu atoke kumuona mwanae, mama yake na Tarick anashtushwa na kitendo cha kutokumuona Frank kwa siku mbili sasa, anapata hofu zaidi akifikiria kuwa zimesalia siku 2 tu kabla ya siku kumi ambazo raisi alikuwa amesitisha shughuli zote za magereza. Mama anaumiza kichwa na kuwaza kuwa ni kitu gani anaweza kufanya, ilia pate picha kamili ya maendeleo ya kesi ya kipenzi chake Tarick. Ni kweli kwamba, kutokana na Frank kuwa alimuhakikishia mama huyu kila kitu kitakwenda sawa ingebidi atulie na kusubili matokeo, lakini uchungu wa mwana aujuae mzazi, mbali na matumaini na imani kubwa aliyokuwa nayo juu ya Frank, kimuhemuhe alichokuwa nacho mama huyu hakikuwa cha kawaida.

Gerezani alipofungwa Tarick, Huku maafisa wa zamu gerezani hapo wakiwa wanaendelea kuweka weka mazingira ya ofisi zao vizuri mara anaingia mchungaji, wote wanamshangaa kwani walikuwa hawamjui na haikuwa kawaida ya mchungaji kufika hapo mida kama hiyo, ilikuwa tayari imefikia saa tatu kamili. Maafisa wanaompokea mchungaji huyo wanamsalimia kwa heshima na nidhamu ya hali ya juu, kisha mmoja wao anamuuliza, “Ndio Baba mchungaji, Naomba nikusikilize tafadhali..”, mchungaji yule anajibu kwa sauti ya ukalimu,”Nimempokea mwenzangu leo kuja kufanya maombi kwasababu hali yake ya kiafya sio nzuri” wote wanapatwa na mshtuko na kutazamana. Mpendwa rafiki, Mchungaji huyu wa dharura alikuwa ni Roby, na ameamua kutumia mbinu hii ili kuona kama anaweza kufikisha ujumbe kwa Tariki kabla hajaja kuchukuliwa. Lakini mbinu hii ya Tariki ilikuwa ya kukurupuka kwani hakuwa akijua hata taarifa moja kuhusiana na Mchungaji aliekuwa akienda pale gerezani kufanya maombi.

Upande wa pili, Mh Profesa Rweyemamu, baada ya kutoa ahadi ya kumpata Brenda akiwa hai, huku akiwa na malengo ya kujisafishia nyota kwa wakwe, lakini pia akiwa na nia ya dhati ya kutaka kulitia mikononi tunda na kipenzi cha moyo wake Brenda, safari hii anaamua kutumia jitihada binafsi bila kuwashirikisha wafanyakazi wake ambao alikuwa akiwatumia kila siku, wala kushirikisha polisi. Rweyemamu anaingia makubaliano ya kuidhamini kampuni ya ulinzi, ili iweze kuwasaka na walio muweka Brenda mafichoni na kumrudisha msichana huyo mikononi mwake akiwa mzima. Kampuni hiyo iliyokuwa imesajiliwa kama kampuni ya ulinzi ilikuwa ikimilikiwa na afisa mstaafu wa jeshi la kujenga taifa. Rweyemamu akiwa kwenye mazungumzo, licha ya kuzungumza mengi na viongozi wa juu wa hiyo kampuni, hakusahau kuwaeleza juu ya mtu anaemchezesha kindumbwendumbwe, akiwa anaelezea hayo anasema, ”Nina nguvu kubwa sana kwenye jeshi zima la polisi, ila nimeamua kutumia kampuni binafsi kumtafuta huyu binti kwasababu kubwa moja, mtu aliemuweka kizuizini sio mtu wa kawaida”, akiwa anazungumza maneno hayo huku viongozi hao wakimsikiliza kwa makini anaendelea kwa kusema, “Yupo imara sana, na kwa jitihada nilizozifanya kwa kutumia jeshi la polisi, ingekuwa tayari nimesha mtia mikononi ila……mmm mmm mmm huyo mtu ni hatari” Rweyemamu anaongea maneno hayo kwa msisitizo mkubwa lakini viongozi wa kampuni hiyo wakionesha kutojali hata kidogo wanasema, ”Proffesa, ndani ya kampuni yetu tumejipanga kuliko kawaida, tunaweza kupambana na uhalifu wa aina yoyote ile, Hata kama huyo jamaa anaweza kupigana kama marehemu bruce, tuna kikosi maalimu kinaitwa Blockline Ninjas kikiongozwa na Don-Ju ninja wa kikorea, moto wa kuotea mbali yaani hakuna kinachoshindikana”. Kusikia maneno hayo Rweyemamu anatikisa kichwa na kuongea taratibu akisema, “Sikumaanisha hivyo, Huyo mtu hajui hata ngumi inavyokunjwa…” kabla Rweyemamu hajaendelea mmoja anamkatisha na kumuuliza, ”Kumbe kitu gani cha kumuhofia!?” Rweyemamu anajibu swali hilo haraka haraka kwa kusema, ”Anafikiria kama Computer! Na amini usiamini wakati mwingine anatumia uchawi, ninauhakika kabisa atakuwa anatumia ushirikina, unapo mtaiti kabisa ili umkamate anaweza kuporonyokea hata kwenye ukuta”. Bila kujua kuwa Frank Tayari alikuwa ameshaaga dunia Rweyemamu anaendelea kuwatahadharisha viongozi wa kampuni hiyo juu yake.

Mpenzi msomaji, katika hatua nyingine Rweyemamu anaendeleza mfululizo wa makosa kwani sasa anajiandaa kutumia nguvu kubwa zaidi akidhani anaenda kupambana na Frank, kumbe Brenda alikuwa mikononi mwa dokta Roby.

Dokta Roby akiwa pale gerezani Maafisa wote wanapigwa na butwaa kusikia kuwa amekaimu nafasi ya mchungaji aliekuwa akifika gerezani hapo kwa ajili ya kuombea wafungwa. Dokta Roby bila ya kujua kuwa, mchungaji huyo alikuwa akifika hapo sikumbili tu za week ambazo zilikuwa ni jumatatu na alhamisi yeye aliendelea kuwaondoa hofu wale askari kwa kusema, ”Hakuna shida… kwasababu nimejiandaa kufanya sala kwa wafungwa wawili watatu tu…”. Kauli, vitendo na maneno ya dokta Roby hatimae vinawafanya askari washindwe kabisa kumwamini, hivyo ili kuondoa ghasia askari mmoja anamwambia kama dharura kama hiyo imetokea basi ni vyema makao makuu ya kanisa waandike Barua kwa mkuu wa gereza, kwaajili ya kutoa taarifa. Kichwa kinamgonga dokta Roby akijuta kukosa maarifa ya kumfikishia Tarick ule ujumbe. Akiwa hana jinsi anawaaga na kuanza kutoka eneo hilo, mara anamsikia askari mmoja akisema, “Bonge kaondoka na gari iliyopeleka wafungwa mahakamani kisutu, nimemuagiza atakuja na karatasi zingine….” Maneno hayo yanamstua Roby, anaganda kidogo huku akiwaza. Kumbe Roby hakujua kuwa gari inayochukuwa wafungwa huwa inafika hapo saa 2 kamili. Na ndani ya muda huo Tayari ilikuwa imefika hapo na kuondoka. Baada ya kugundua hilo Roby anajipiga kichwa kwa hasira, anawaza mpaka anafikiria kuwa afadhari Frank andekuwepo muda huu tayari angekuwa ametoa wazo nini cha kufanya, anajidharau na kujiona mjinga.

Dokta Roby anakosa cha kufanya ila kabla hajaamua kukata tamaa kabisa anaamua kwenda kumalizia kazi yake mahakamani kujaribu kufatilia ni nani waliemchukuwa kwa jina ambalo Frank alikuwa amelibadilisha taarifa na za Tariki. Roby anaondoka na kuelekea moja kwa moja Kwenye mahakama ya kisutu, anafika eneo na kuamua kukaa kwa nje kidogo ilifikirie nini alitakiwa kuuliza au kusema mahakamani hapo. Akiwa hapo nje, kutoka ndani Roby anamsikia Hakimu ndani ya mahakama akisema. “Baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi uliotolewa na wananchi mbali mbali, mahakama hii imejiridhisha na kukukuta na mashitaka sugu ya wizi wa mifugo midogo midogo ya majumbani, hususan ni kuku na Bata. Hivyo kwanza mahakama hii inakupa Ndugu Lucas Shehiza onyo la kuacha tabia hiyo mara moja, pia inakupa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela au fine ya kiasi cha shilingi laki tano”. Jina la Lucas Shehiza linalotajwa kwenye hukumu hiyo linamfanya Roby asimame na kuingia ndani yajengo la mahakama.

Ndani ya kipindi hicho, proffesa Rweyemamu alikuwa amefika gerezani kwaajili ya shughuli za kikazi, kama kawaida yake anaamua kwenda kumdhihaki adui yake Tarick. Kufika katika Eneo alilokuwa amefungwa Tarick, Rweyemamu anashtuka kuona eneo hilo halina mtu, anaita askari aliekuwa karibu yake na kumuuliza, “Kaamishiwa wapi huyu!? ” yule askari anajibu kwa nidhamu, “Ni siku yake ya mahakamani mheshimiwa, amechukuliwa asubuhi”. Rweyemamu ana uliza kwa mshangao, ”What!”. Rweyemamu anakimbia mpaka ofisi kubwa ya utawala, anafika na kuwauliza, ”mfungwa wa chemba no 216 yupo wapi” dada mmoja anatizama kwenye computer na kujibu, “ni siku ya kesi yake leo amechukuliwa na watu wa mahakama.” Reyemamu anakunja mdomo kwa hasira na kusema, “Acheni upumbavu, chumba namba 216, ni Tarick abdul Gaidi aliehukumiwa kifo, mmempeleka kusikiliza kesi gani?”, Askari mwingine wa kiume anajibu, ”Samahani mheshimiwa, chumba namba 216 hakuwa Tarick Abdul bali ni Lucas Shehiza” Rweyemamu anasogea kwa kasi mbele ya ile kompyuta na kuoneshwa jina na picha, Rweyemamu anakuna kichwa kwa hasira na kusema, ”Nani kaliweka hili jina hapa? Mwenye hii picha ni Tarick Abdull !, nani kaweka hili jina la Lucas Hapa!? Mnacheza na Dolla!?” yule kaka anajibu na kusema, “Mheshimiwa… Database ya Profile za wafungwa inasimamiwa na Wizara sisi hatuna access kabisa wala uwezo wa kufanya mabadiliko yoyote”. Frank anaganda ghafla na kuduwaa, kisha anasema taratibu kwa sauti ya upole na utulivu, “Toa taarifa wamzuie huyo mtu sasa hivi wasithubutu hata kumshusha kwenye gari”. Rweyemamu anawaacha wale maafisa magereza wakihaha kupiga simu ili kutoa taarifa za kumzuia Tarick, Kisha yeye anaondoka kwa kasi kuelekea mahakamani ili kuwahi isije ikafanyika mistake Tarick akaachiwa au akawatoroka.

Roby nae pale mahakamani baada ya kuingia ndani anagundua kuwa yule aliekuwa akisomewa hukumu alikuwa ni Tarick. Mpenzi msomaji hapa mpango wa marehemu Frank ulikuwa umefanikiwa kwa asilimia mia moja. Kwani timu ya askari iliyokuwa ikizungukia magereza na kuchukua wafungwa wa kuwapeleka mahakamani ilifika pale gerezani na kumchukua Tariki kwa kufananisha picha yake na namba ya kizimba alichokuwa amefungwa. Mara ya kwanza wakiwa ndio wanaenda kumtoa gerezani Tarick alijua kuwa safari ya kuelekea isanga Dodoma ndio ilikuwa imewadia, lakini kitendo cha kushushwa Kisutu Tarick aliona ni mauzauza tu na hakuwa na nafasi ya kuzungumza chochote mpaka anasomewa hukumu ya wizi wa kuku. Kitendo cha hakimu kuuliza tu kama kuna ndugu yake yoyote atakae mlipia fine, Roby anajitokeza, kisha anaongozana na askari kwenye ofisi za Mahakama kwa ajili ya kufanya malipo ya fine hiyo. Muda wote huu Tarick alikuwa akiduwaa bila kuzungumza chochote, huku akiwa haelewi wala haamini kinachoendelea, anakuwa kama simu iliyopoteza network, nimtu ambae anahisi yupo ndotoni ndani ya gereza. Inamchukua dk 7 tu Roby kufanya malipo yote, kisha bila kuchelewa anampakia Tarick kwenye gari na kupotea nae maeneo hayo.

Wakiwa njiani, Roby anamwambia Tarick, “Pole Tarick… Hawatakuona tena”, Tarick anajibu, ”Ahsante nashukuru… Lakini.. wewe ni nani!? Na nini kinaendelea!?” Roby akiwa anaendesha gari kwa kasi anasema, “Utafahamu kila kitu tufike nyumbani” tariki anasema, “Naomba nipeleke kwa mama yangu, anione kama nipo nje ya gereza” Roby anamwambia tarick, “Sio salama, na pamoja kuwa uponje ya gereza haupo huru”. Huku wakiendelea kuzungumza maneno yasiyokuwa na uelekeo maalum wanajikuta wamefika nyumbani kwa Roby. Roby anamuandalia maji Tarick na kumwambia akaoge kisha abadilishe nguo. Tariki anaoga vizuri kisha dokta Roby anaanza kushughulikia majeraha na maumivu mbali mbali aliyokuwa nayo, huku akisema, “Tarik karibu sana jisikie upo nyumbani”, Tarick anaitikia, “Inshallah, Wewe ni nani na imekuwaje mpaka mimi niko hapa!” Roby anajibu, ”Ndugu yako Frank ndie aliyekusaidia” Tarick kusikia kauli hiyo anamkatisha Roby na kuuliza,”Yupo wapi Frank!?” Roby anasita kidogo na kuonesha kuwa hakutarajia swali kama hilo, kisha anajibu, ”Utamuona… Pole sana mwili wako unaonesha umeteseka. Na hivi…. ni nini kinachoendelea kati yako na Brenda?” Frank anajibu swali hilo kwa kusema, “Ni mwanamke shetani sana, yeye ndie iliefanya mipango yote mpaka mimi kutiwa hatiani na kuhukumiwa, Ni msichana ambae alijifanya ananipenda sana, siku zote nilimkatalia kabisa kuwa na mahusiano nae kwasababu nilikuwa nikifahamu uhusiano wake na Mheshimiwa mmoja hivi.., baadae alinipa tenda ya kuwa mpiga picha wake kwenye shughuli zake za uwanamitindo akajenga mahusiano ya karibu sana na mimi, na mipango yake ilipotimia akaniomba nimsindikize Arusha huko ndiko wakanibambika hiyo kesi”. Roby anasema, “Pole sana Tarick. Mungu amesaidia umefanikiwa kutoka, Sasa kimebaki kibarua kimoja cha kufanya wasikuone tena. Frank aliniambia nikusaidie kutoroka kabisa nje ya Tanzania ili usikamatwe, ninajamaa zangu wapo Botswana nimezungumza nao itabidi keshokutwa tufanye mpango wa safari ukafanye maisha yako huko”.
Kule Mahakamani Baada ya Rweyemamu kufika na kukuta Tarick akiwa ameachiwa na mahakama kwa fine ya laki tano. Bila kuchelewa Rweyemamu anatoa taarifa kwa viongozi wote wa vyombo vya ulinzi na usalama, na taarifa hizo zinamfikia mpaka waziri wa ulinzi. Maramoja waziri huyo anaitisha kikao dharura kitakacho jumuisha viongozi wote wa taasisi za ulinzi na usalama.
Roby baada kumpa huduma ya kwanza Tarick na kumuacha huku akimwambia asijaribu kutoka kabisa hata iweje. Roby anatoka nyumbani kwake kukimbilia hospitali, ili akafahamu nini kilichokuwa kimejiri juu ya hali ya Brenda. Anafika mpaka hospitali lakini kwa bahati nzuri kunakuwa hakuna taarifa mpya ila madaktari waliokuwa wakimshughulikia Brenda wanamwambia kuwa ubongo wa Brenda ulikuwa na mabaki ya kemikali za sumu, ambazo kwa teknolojia yetu hatuwezi kuzisafisha hivyo ili aweze kurudisha akili yake kama awali inabidi asafirishwe kwenda kumalizia matibabu yake nje. Hili linakuwa zoezi lisilowezekana kabisa kwa Roby kwani kitendo cha kujaribu kufanya hivyo, kinaweza kumfanya akakamatwa na Brenda kisha akaingia kwenye matatizo makubwa, kutokana na mawazo haya Roby anaamua kufanya mpango wa kumrudisha Brenda kwa Rweyemamu.

Baada ya pilika pilika hizo Robi anaamua kumalizia siku yake kwa kwenda kumtoa mdogo wake polisi. Ndani ya gari akiwa anamrudisha nyumbani Roby hakutaka kuongea nae chochote, lakini Zubery anasema, ”Roby naomba unisamee Bro, nakuahidi hili halita jirudia tena, Nipeleke kwa Frank nikamuombe radhi”, Roby huku bado akiwa na hasira na machozi yakimlenga anasema, ”Na hilo ndio litakuhukumu mtu ambae ungemuomba samahani ameshakufa”, Zubery kwa mshangao anasema, “Frank Amekufa!?” Mshutuko huo unamfanya Roby amjibu kwa ghdhabu, “Mnafki mkubwa wewe, wakati unamuitia polisi wenye masiraha kiasi kile ulitegemea nini?”. Mazungumzo hayo yanaendelea, na mpaka wanafika nyumbani kunakuwa hakuna maelewano njia nzima.
Baada ya kumrudisha Mpaka nyumbani, Roby anarudi kwake kwaajili ya kujiandaa na mazishi ya Frank.

Hatimae Tarick Amefaulu kutoka Gerezani, Vitengo vyote vya ulinzi na usalama vinakutana kwa dharura ili kujua ni jinsi gani wataweza kulitia gaidi hilo nguvuni mapema iwezekanavyo kabla hata halijasababisha Athari zozote wala halijatoka nje ya mipaka ya nchi. Roby anataka kumrudisha Brenda kwa Rweyemamu na kumtorosha Tarick mbali kabisa nje ya nchi. Je Huu ndio mwisho wa hisia kali za kimapenzi za Brenda dhidi ya Tarick, Bado ni kizungumkuti kikubwa usikose kufatilia Episode namba 8 ya tamthilia hii ya the Second Door.

Kwa kumalizia, niseme tu kuwa kuna vitu viwili vinavyoniumiza kichwa, Sijui idadi ya watu wanaofatilia tamthilia hii, I real want to know my readers, lakini pia nataka kujua ni kiasi gani tamthilia hii inawavutia na jinsi gani mnaithamini fanya nijue, unaweza kufanya yote haya kwa kuchangia hata 500 tu kupitia namba ninazotoa, yaani katika watu 8000+ wanaosoma hakuna aliyechangia hata 200 tu!? Kama Tamthilia haivutii coment hapa chini, mimi nitafanyia kazi kila comment kama nilivyofanya tangu awali, na kama itaendelea hivi kufikia episode 8 nitaisimamisha Tamthilia hii na kuanza nyingine nzuri zaidi itakayo wafurahisha. Tukutane kwenye episode no8.

Kwa wasomaji wa wattpad namba za kutumia mchango wako ni

TIGO:0712494761

VODA:0754955566

The Second Door - Episode 1Where stories live. Discover now