Mpendwa Rafiki, leo tunaendelea na Episode namba 8 ya Tamthilia hii nzuri kabisa ya The Second Door, Katika Episode ya 7 Tuliishia kuona Roby akiwa amefanikisha zoezi la kumtoa Tarick Gerezani Kwa kumlipia Fine.
Ikiwa ni siku mpya, alfajiri na mapema, Roby akiwa ndio anatoka kuamka anamalizia kujiandaa ili aende kazini huku akiwa na lengo la kwenda kutazama hali ya Brenda pamoja na kufanya utaratibu ikiwezekana leo wamzike Frank, kumbuka tu muda wote huu Roby alikuwa hajamtaarifu Tarick juu ya kifo cha Frank. Wakiwa pamoja Roby na Tarick wanakunywa chai, Tarick anasema, “Nashukuru sana kwa msaada wako dokta”, Roby anatabasamu na kusema,”Usijali ilikuwa ni lazima nimalizie kazi hii kwa nguvu yeyote ile” Baada ya Roby kusema maneno hayo, Tarick anamuuliza Roby, “Lakini dokta leo si ninaweza kurudi nyumbani!?”, Roby ananyamaza kidogo kisha kwa umakini mkubwa anasema, ”Mashtaka yako ni makubwa sana, na tangu jana utoke, hatujajua polisi wapo katika hali gani. Naona ni vema tusubiri kwanza, lakini kwakuwa lengo kubwa ni kumuondoa mama hofu, mchana nitaenda kumfata aje uonane nae”. Tarick anaridhika na ushauri wa Roby na kujibu, “inshalla nahisi hilo litakuwa jambo jema zaidi”. Kimya kifupi kinatawala huku wakiendelea kunywa chai, Roby anaanza kusema, “Tarick! Frank amekupigania sana” Tarick anajibu kauli hiyo kwa kusema, ”Ndio maana ninahamu isiyo kifani ya kumuona ndugu yangu, sijui nitafurahi kiasi gani, kwanini usiwasiliane nae tuone kama anaweza kufika hapa leo!”. Kwambaali sana majonzi yanaanza kuonekana usoni kwa Roby, anajibu kwa upole na uchungu huku akijitahidi sana kuficha hisia zake, anasema, “Tarick! Usihofu tutaonana nae tu, Lakini Nasikitika sana kwamba hatutaweza kuwasiliana nae tena kwa sasa”. Tarick akiwa ndio anamalizia chakula kauli ya mwisho inamfanya moyo wake unashtuka kama mtu mwenye presha anauliza kwa hofu, “Nini kimetokea!?” Roby anajibu,”Katika purukushani za kutetea uhai wako, Frank alipoteza maisha, hatunae tena”. Taarifa hiyo inampa simanzi kubwa sana Tarick na kumfanya aangue kilio. Analia kwa uchungu huku akilaumu kwanini alifikia hatua ya kupoteza uhai wake wakati hukumu yake ilitokana na uzembe wake Mwenyewe.
Huku nyumbani mama yake na Tarick anahaha kumtafuta Frank kwenye simu ili apate taarifa za hukumu ya Tarick kwani alijua kuwa leo lazima angesafirishwa kuelekea Dodoma kwenye hukumu hiyo. Anapiga simu bila kukata tamaa lakini hakuna matumaini yoyote ya kupatikana simu hiyo. Baada ya mama kuitafuta simu ya Frank kwa muda mrefu bila mafanikio, anaamua kujiandaa ili aende kule gerezani kufatilia na kupata taarifa.
Huku kwa Roby mara baada ya Tarick kupewa taarifa za kifo cha Frank na mazingira yaliyopelekea mauti yake, Tarick analia mpaka uso wote unamvimba, analia kiasi kwamba Roby anaanza kuhofia afya yake na kujuta kwanini alimpa taarifa hizo mapema. Lakini haina jinsi, Robi anamuaga Tarick ili kafatilie mipango ya mazishi. Roby akiwa anatoka tu kwenye geti la nyumba yake, zinakuja Difender mbili kwa kasi na kufanya moyo wa Roby udunde kwa nguvu kutokana na hofu. Difender hizo zinakuja na kupita kwa kasi mbele ya nyumba hiyo huku zikipiga ving’ora. Kimoyo moyo Roby anasema “hii ndio ghasia ya kuishi kandokando ya barabara”. Asubuhi hii Roby akiwa ndani ya gari lake anaendesha moja kwa moja mpaka hospitali kisha kabla hajaingia ofisini kwake anaenda kimtizama Brenda na kumjulia hali. Baada ya hapo anaweka mambo yake ya kiofisi sawa kisha anatafuta vijana na kuwapa hela waende wakaandae mazingira ya kuupumzisha mwili wa Frank. Vijana hao wanapokea hela ya kutosha na kwenda kufanya maandalizi yote kwenye makaburi yaliyopo kinondoni.
Mpenzi msomaji Desturi mbaya ya dokta Roby kutofatilia wala kujali kilichokuwa kikiendelea kwenye vyombo mbalimbali vya habari, safari hii inaweza kumgharimu, kwani magazeti yote ya siku hiyo yalikuwa yamepambwa na taarifa ya tukio la kutoweka kwa Tariki kutoka mikononi mwa jeshi la polisi, kwa upande mmoja swala hili linaripotiwa kama kashfa ya uzembe wa hali ya juu kwenye jeshi la polisi, na katika ripoti zingine tukio hili linaelezewa kwa makisio kuwa limefanikiwa kutokana na teknolojia ya hali ya juu inayotumiwa na mitandao wa kigaidi, lakini mwisho wa yote vyombo vyote vya habari vinaripoti, msako wa kihistoria dhidi ya gaidi hilo. Kama ilivyo kawaida magaazeti ya udaku nayo hayakuacha kupiga bao kwenye biashara ya taarifa hizo huku magazeti hayo yakiwa yamepambwa na habari tofauti tofauti, wakati mengine yakiandika “Gaidi la lililohukumiwa kifo laachiliwa kwa fain kwenye kesi ya kuku”. Taarifa zote hizi pamoja na vipindi vyote kwenye maredio kulizungumzia swala hili kwa mitazamo tofautitofauti lakini Roby hakuweza kujua ukubwa wa tukio zima.
YOU ARE READING
The Second Door - Episode 1
RomanceThe second Door ni simulizi yeny mikasa na matukio ya aina yake, Ungana na zaidi ya wasomaji 10,000 wa simulizi hii kupitia jumuia yetu ya WattPad, Mtandao wa JamiiForum na Kurasa yetu ya FaceBook. usikubali kupitwa na mikasa hii ya kusisimua