Naam mpenzi msomaji, Niwakati maridhawa, tunaokwenda kukutana kwa ajili ya kuendelea na Tamthilia yetu ya the Second Door katika sehemu ya 6.
Mara ya mwisho katika Episode Ya 9, tulimuona Frank mapema alfajiri akiwa anawahi kuelekea Unix Network ambako mara ya mwisho alivyoenda alikubaliana nao kuwa angerudi leo kwa lengo la kufanya ukaguzi kama network yao ilikuwa salama kwa ajili ya usafirishaji wa hiyo database. Frank akiwa njiani baada ya kugundua kuwa Jina lake lilikuwa kwenye most wanted list ya polisi, analazimika kuongeza umakini mkubwa kwenye kila hatua anayopiga. Akiwa njiani anahakikisha macho yake hayagongani na ya mtu yoyote, lakini pia sasa hivi anaona ni vyema kuacha kabisa kupita njia zenye msongamano wa watu ikiwa ni pamoja na kutumia usafiri wa uma. Safari ya Frank inampeleka mpaka kwenye ofisi za Unix Network, tofauti na alivyokuja awali safari hii anapokelewa vizuri kama mgeni wa heshima. Frank anafika kwenye chumba cha maengeneer, na kutoa Laptop yake na Kifaa ambacho hakuna mtu ambae aligundua kuwa kilikuwa na kazi gani. Lakini kama unavyojua ingekuwa aibu sana kwa maingeneer wale kuanza kuuliza kuwa kile kilikuwa ni kifaa cha nini. Kilikuwa ni kifaa chenye umbo Fulani hivi la mraba na antenna ndogo, kifaa hiki Frank atakitumia kuhakikisha hakuna mtu yoyote ambae anaweza kugundua nini alikuwa anafanya pale, kilikuwa na uwezo wa kuzuia conection yoyote ambayo pengine ingetumika kutrack(kufatilia) vitu anavyofanya Frank muda ule.
Kama ilivyo kawaida hususan kwenye miji mikubwa kama Dar Es Salaam Taarifa za anatafutwa huwa sio ngeni kwenye kurasa za magaazeti, watu husoma na kwakutumia mazoea huzipuuzia, lakini kutokana na Donge nono la kiasi cha shilling million 5 zilizo tangazwa, zinafanya kila mmoja ajute kwanini hamfahamu huyo mtu anaetafutwa. Zikiwa zimesalia siku tano tu kabla ya hukumu ya Tariki na kundi la magaidi wengine 9 kunyongwa, Rweyemamu mheshimiwa ambaye moyo wake ulishindwa kabisa kupata U-turn ya mahaba dhidi ya mrembo Brenda, baada ya kuset Plan Kabambe ya kutumia jeshi la polisi kumnasa mtu anaemchezea akili na kukinasa kipenzi chake anaamua kuvuta pumzi ili atizame kama mpango huo utazaa matunda, akiwa ametulia Ofisini kwake, anamwita secretary wake na kumwambia, amwandikie Bosko Barua ya likizo ya mwezi mzima ili ashughulikie afya yake vizuri.
Frank Huku akiwa anaamini kabisa kuwa hata pale alipo hapakuwa salama hata kidogo, anaamua kufanya alicho kuwa anafanya chapchap. Akiwa anaendelea kufanya mambo, anaingia Engeneer mmoja akiwa ameshikilia Gazeti la udaku, anasalimia kila mmoja na kukaa sentimita chache kando ya Frank, anakunjua gazeti lake na kuanza kusoma. Akiwa amekunjuwa gazeti hilo, kwenye kurasa ya nyuma kabisa Frank anaona maandishi makubwa yakiwa yanasema Jasusi La kimataifa kutoka Kongo lakimbilia Dar. Gazeti hilo linapamba habari hiyo kwa picha kubwa ya Frank ambayo haina muonekano ang’avu kutokana na waandishi wa gazezi hilo kutumia picha ya paspotsize ambayo ilikuwa imetolea na polisi na kuikuza kisha kuipamba kwa nakshi nakshi za milipuko na maganda ya Risasi. Halikuishia hapo gazeti hilo, habari hiyo inaendelea kwa subtitle zilizokuwa zinasema, Laishi Dar kwa zaidi ya wiki 3. Atakae Likamata Kutajirika. Polisi waapa kulinasa. Gazeti hili linamfanya Frank akose amani, Jasho linamtoka katika jitihada za kufunga funga na kumalizia alichokuwa akifanya.
Mpenzi msomaji, alichokuwa akifanya Frank Ndani ya Kampuni hii ya Unix Telecom haikuwa Kuchunguza Usalama Wa network kama alivyodai Bali ilikuwa ni kupekenyua mwanya wa kupata access na Database za magereza ili afanye mpango wa kuzihack na ikiwezekana uharibifu huo utumike kumsaidia Rafiki yake ama, usaidie kutimiza adhma hiyo. Akiwa anasubiri baadhi ya taarifa zijisevu ili kumalizia shughuli yake, yule jamaa aliekuwa na gaazeti anafikia kurasa moja kabla ya kudondokea kwenye kurasa yenye taarifa ya Frank. Frank anaamua kuomba kipande cha mwisho ili asome. Cha ajabu ni kwamba, moja kwa moja Frank analigeuza gaazeti lile nyuma mbele ili wasione ile taarifa ambayo ilikuwa inamuelezea yeye, kisha anaanza kuzuga kama anaisoma bila kusoma hata herufi moja. Ndani ya wakati huo Frank hakuwa akifahamu kuwa mwenzie alikuwa akiifatilia habari kamili kwenye kurasa ya ndani, Frank anaamua kwenda chooni ili kuweka kipande kile cha gaazeti mbali na eneo hilo. Anauliza choo kiko wapi, anaelekezwa na kutoka kwenda chooni, choo hicho kilikuwa humo humo ndani hatua kadhaa tu ukutoka kwenye chumba cha ofisi ya maengeneer. Kitendo cha Frank kutoka tu, huku akiwa ameacha begi na computer yake, Yule jamaa aliekuwa akisoma gaazeti anasimama mbio mbio pembeni kidogo na kupiga simu kituo cha polisi. Huku chooni Frank akiwa hana hata moja, kumbe ndani ya muda huo General maneger nae alishaliona tangazo la kutafutwa Frank, kisha akawasiliana na askari ili kuhakiki taarifa hizo na jinsi atakavyopata malipo yake halafu akawaelekeza mahali ofisi zao zilipo.
YOU ARE READING
The Second Door - Episode 1
RomanceThe second Door ni simulizi yeny mikasa na matukio ya aina yake, Ungana na zaidi ya wasomaji 10,000 wa simulizi hii kupitia jumuia yetu ya WattPad, Mtandao wa JamiiForum na Kurasa yetu ya FaceBook. usikubali kupitwa na mikasa hii ya kusisimua