The Second Door - Episide 3

223 1 0
                                    

Mpendwa Rafiki, Namshukuru mola kwa kuweza kunijalia Afya njema, nimatumaini yakungu kuwa nawewe ni mzima wa Afya. Ni weekend safi kabisa, siku ya jumamosi ya tarehe 17 kwenye mwezi huu wa 5. Kama kawaida tunaendelea na simulizi ya Tamthilia yetu nzuri kabisa, Tamthilia ya The Second Door, na leo nawaletea Episode namba 3 ya simulizi hii.

Katika Episode ya 2 tuliweza kushuhudia jinsi ambavyo jitihada za Frank kujaribu kukata rufaa kwenye kesi ya Tarick zikigongeshwa mwamba na mtu ambae frank hakuweza kumjua ni nani, japokuwa alishahisi kuwa kunauwezekano mkubwa kwamba kunamtu ambae alikwamisha mpango huo kwa makusudi. Tukio hili zima bado linakuwa kizungumkuti kwa Frank, kwani mtu ambae angemwambia pa kuanzia alikua ni Brenda ambae mpaka hivi sasa hatma ya uhai wake ipo mikononi kwa mwenyezi mungu.

Frank anaondoka katika mazingira ya pale mahakamani na anaamua kuelekea Gerezani ambako Tarick Amefungwa, Kumbe ndani ya muda huo bila ya kufanya makosa Profesa Rweyemamu tayari alikuwa ameshafanya mpango, ikapelekwa list maalumu ya baadhi ya wafungwa ambao wamefungiwa ruhusa ya kutembelewa na mtu yoyote zaidi ya maafisa usalama. Bila kujua hilo,Safari ya Frank Inampeleka mpaka gerezani, Baada ya kufatilia Taratibu za kumuona mtu wake, maafisa waliokuwa zamu muda huo wanatizama Details za mfungwa husika, kisha wanampa taarifa frank kuwa kwa bahati mbaya mfungwa huyo yupo kwenye list ya wafungwa maalum ambao hawaruhusiwi kuonana na mtu yoyote, mpaka uandike barua ya maombi kwa Jenerali Devid Mwamkonge, halafu uandike barua nyingine ya utambulisho ipelekwe kwa mh profesa Rweyemamu. Kusikia jina la Rweyemamu, Frank anatoa tabasamu lake ambalo linataka kuwa kama tabasamu la dharau, lakini ndio maumbile yake yalivyo. Anatabasamu kwa kupinda mdomo pembeni hivi kisha anawaaga wale maofisa na kuondoka akiwaacha wameduwaa.

Kinachowashangaza zaidi maofisa hao kwanza kuona jinsi mtu ambae ndugu yake yupo kifungoni, akiwa hana taharuki ya kutaka kumuona, hasa baada ya kuzuiliwa kufanya hivyo. Rweyemamu akiwa ofisini kwake majira ja mchana, unakaribia kabisa muda wa chakula cha mchana. Yupo kwenye kikao kifupi na baadhi ya watu wake. Kikao hiki kilikuwa kikihusiana na mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa mwili wa Brenda unapatikana kwa njia yoyote ile, kumbuka wao waliamini kuwa Brenda alikuwa ameshapoteza maisha, hivyo kati ya maadhimio ya kikao hicho kifupi ilikua ni kuupata mwili wa Brenda, pili kumpata mtu alieuiba dakika chache baada ya tukio, pamoja na kumfungulia mashtaka mtu huyo.

Wanamaliza kikao na kila mtu anatawanyika. Inapita kama dakika moja hivi huku Profesa Rweyemamu, akiwa anawekaweka sawa madocument yake, mara anaingia mgeni ghafla, Rweyemamu anainua macho ghafla, na kugongana uso kwa uso na mgeni huyo, Kwa mstuko Rweyemamu anasema, ”Samba!?” mgeni huyo ambae alikua ni Frank anamjibu, “Suppries……!” Rweyemamu anaendelea kwa kusema, “Umefikaje Ofisini kwangu bila Taarifa!?” Frank huku akiongea Taratibu na kwa uhuru anajibu, “Sikufikiria kufanya hivyo, au unahisi ingesaidia kunizuia kufika hapa?” Frank anatikisa kichwa kuonesha kukataa kisha anaendelea, “ilikua lazima nionane na wewe by anyhow”, Frank akiwa anazungumza maneno hayo, Rweyemamu ana sogeza mkono wake taratibu kwenye button ya alam huku akiuliza, “Ok unataka nikusaidie nini?” Frank anamtizama kwa dharau kisha anamjibu, “Kitu cha kwanza, simamisha zoezi lako la kuita Walinzi”. Baada ya kuambiwa hivyo Rweyemamu anato mkono wake Taratibu karibu na batan Ya Alam, Frank anaendelea kwa kusema, “Halafu nisikilize kwa makini”.

Muda wote huo Rweyemamu alikua amekaa chini, Sasa Frank nae anakaa chini taratibu huku akisema. “Ni zaidi ya miaka 20 imepita, tangu mzee Edward Rosta Rweyemamu baba yako alipo muua mama yangu ili apite kwenye uchaguzi.” Baada ya sentensi hiyo frank ananyamaza kidogo Bila kuonekana na Rweyemamu anabandika kifaa kidogo kama kifungo cha koti amabacho kitaalamu kinaitwa DMR(Dynamic Micro Recording), kisha anamkazia macho Rweyemamu na kuongea kwa sauti ya chini na msisitizo,”Unakumbuka kuwa mimi na dada yangu tulibaki yatima………… tukavunjiwa nyumba yetu ya urithi, ili kupisha ujenzi wa bomba la maji……….” Mpenzi msomaji sijui nitumie maneno gani kukueleza hali aliyokuwanayo profesa Rweyemamu kipindi Frank anamwambiaa maneno hayo, lakini kwa kifupi alilowa mpakaaaaaa ……….,. Frank anaendelea, “na Fidia Mpaka leo Hatujalipwa…………. Najua hujui nini kiliedelea………, Kale kadada kangu kiliko kadogo kipindikile kalishatangulia mbele za haki, kabla ya mimi kuacha shule na kuwa mtoto wa mitaani ” Frank anakaa kimya kidogo na kuendelea, “Sasa sijaja kulipa kisasi kwa mauaji yaliyofanywa na baba yako, wala sikuja hapa kudai fidia ya nyumba yetu mlioibomoa miaka 20 iliopita, nimekuja kukupa onyo moja tu! ……………. Ukimwaga damu ya mtu yoyote asiekuwa na hatia……… Utaioga.”

The Second Door - Episode 1Hikayelerin yaşadığı yer. Şimdi keşfedin