Habari gani Rafiki, ni wasaa mwingine tena unapoungana nami mwandishi wako Msamiati, katika kuwaletea mkasa wa kuburudisha ndani tamthilia hii ya the second door, na leo tunaenda kuendelea na episode no 10 ya mkasa huu.
“Kichwa kimestack kabisa... au wewe umepata wazo lolote?”Swali hili linaulizwa na Roby, kisha Tarick anajibu kwa kutikisa kichwa huku akisema, “Hapana sijapata jibu tutafanyaje”. Kitendo cha Tarick kumaliza kauli yake hiyo ghafla mlango unasukumwa kisha anaingia Zubery huku akisema, “mimi ninajibu kaka…” Roby anasimama kwa mshutuko na kusema, “Zubery… ! mbona umekuja bila taarifa?” Zubery huku akijiamini, taratibu anawasogelea Roby na tariki wakati akiendelea kusema, “Roby, najua mpo katika wakati mgumu sana kaka yangu, na mimi ninawazo linaloweza kuwatoa katika sintofahamu hii”. Zubery akiwa ametembea mpaka kwenye viti, huku wakitazamana na Roby wanakaachini kwa pamoja, kisha kwa msisitizo Roby anasema, “Zubery…! Nashukuru kwa wazo, lakini ninavyoongea hivi simama urudi nyumbani, na usijaribu tena kuja hapa bila kunipa taarifa.” Tarick anaamua kuingilia mazungumzo haya kwa kusema, “Samahani dokta, sitaki kuingilia matatizo ya kwenye familia yenu, lakini… unahisi tofauti yenu inaweza kuwa muhimu kuliko wazo analotaka kulitoa!?” Baada hoja hiyo ya Tarick kila mmoja anakaa kimya, lakini kwa Roby ukimya wake unakuwa wa tofauti kwani unatokana na shaka kubwa ya kuweka maisha ya Tarick rehani kwa kuamua kumuamini tena Zubery, hata hivyo Roby hataweza kuzungumzia chochote juu ya kosa alilofanya Zubery kwani inaweza kuleta mtafaruku kati ya Zubery na Tarick. Baada ya kimya hicho kifupi Tarick anamalizia kwa kusema, “Wacha tumsikilize, Hata wazo lake likiwa na kasoro linaweza kutupa pa kuanzia” .
Zubery anadakia na kuanza kusema wazo alilokuwa nalo huku wote wakimsikiliza kwa makini, “Tarick anaweza kuendelea kuishi kwa uhuru na amani endapo atabadilisha kila kitu katika uhalisia wake, abadilishe, Jina, Wazazi, Vitambulisho, Pasport na Historia ya maisha yake”. Maneno hayo ya Zubery yanaonesha kudharauliwa na kila mmoja, na kuona kuwa lilikuwa ni wazo la kitoto kabisa. Roby kwa kejeli anasema, “asante kwa wazo unaweza kwenda sasa!”, Tarick anadakia na kusema, “Sikia Zubery, nitakapokamatwa vitambulisho feki havitaweza kunisaidia” Zubery anamkatisha Roby na kumwambia, “Hamjanielewa, Tarick anatakiwa akajipandikize kwenye familia nyingine na kuishi ndani ya familia hiyo kwa kutumia details zote za mtoto ambaye yupo kwenye hiyo familia”. Roby anaonekana kuelewa alichokuwa akifikiria Zubery anamjibu kwa kumwambia, “Ok….. kwa wazo lako, Let Say Tarick anajipandikiza kwenye familia yetu kwa mfano na kutumia ID zako zote, kuanzia jina, historia ya kuzaliwa elimu na kila kitu, then how about you!?” Zubery anajibu Swali hilo kwa kusema, “Nina rafiki yangu ambaye kaka yake mkubwa alizamia south africa miaka kumi iliyopita na mpaka leo hana mawasiliano yoyote na familia yake, Tarick anaweza kujipachika kwa urahisi kwa kujifanya ndio yeye amerudi”.
Roby na Tarick wanafikiria wazo la Zubery na kugundua kuwa lilikuwa ni wazo zuri, lakini lilikuwa gumu kuliingiza kwenye uhalisia. Kwakuwa wameshajadili kwa muda mrefu na sasa umesha kuwa usiku mnene, wanakubaliana kulala ili kesho wajaribu kulifanyia kazi wazo hilo.
Inaingia siku nyingine, Jumapili tulivu leo Tarick ameamka na wazo la kumpigia simu mama yake lakini Roby anamzuia na kumwambia kuwa kitendo cha kuwasiliana na mama kwenye simu kinaweza kutumiwa na askari kugundua mahali alipo, Tarick anaamua kusikiliza ushauri wa Roby. Baada ya hapo, Roby anajiandaa na kuwaaga kuwa kunashughuli za kikazi ambazo lazima akazimalizie weekend hii hivyo atawaacha hapo na kurejea kabla ya saa 8 mchana, Lakini anamwambia Zubery asiondoke mpaka yeye atakaporudi. Mara baada ya Rweyemamu, kugundua kuwa mtu aliyekuwa amempigia simu jana alikuwa na taarifa zinazohusiana na Tunda la moyo wake Brenda, Leo anaamua kusuka mpango kabambe wa kuhakikisha anamnasa mtu huyo na kupata taarifa zote zinazohusiana na Brenda . Rweyemamu anaita timu ya vijana wake, na kuwapa maagizo, kwa umakini na msisitizo mkubwa anasema, “Kuna mshenzi mmoja alinipigia simu jana, kauli yake ya mwisho inaonesha kuwa anataarifa za Brenda, sasa chukueni hii namba fanyeni juu chini mumpate huyu mtu, mnaweza kwenda hata TCRA wakawasaidia, hakikisha mnafanya kadri iwezekanavyo kutumia vizuri taaluma zenu ili kupata hizi taarifa. Jioni nataka jibu ” baada ya Rweyemamu kutoa kauli hiyo na kuwakabidhi kazi hiyo kwa watu wake, anawaaga na kuelekea kwenye ofisi ndogo za bunge kwa ajili ya shughuli zake za kikazi.
YOU ARE READING
The Second Door - Episode 1
RomanceThe second Door ni simulizi yeny mikasa na matukio ya aina yake, Ungana na zaidi ya wasomaji 10,000 wa simulizi hii kupitia jumuia yetu ya WattPad, Mtandao wa JamiiForum na Kurasa yetu ya FaceBook. usikubali kupitwa na mikasa hii ya kusisimua