The Second Door- Episode 5

162 3 0
                                    

Habari gani marafiki namshukuru mwenyezi mungu kwa kuweza kuniweka salama mpaka wakati huu, Lakini pia kwa kutuwezesha kufikia Episode ya nane kwenye Tamthilia hii.

Kwenye episode namba nne tuliweza kuona jaribio la Frank na dokta Roby kuwatoroka Makachero waliokuwa wametumwa na Rweyemamu, na tukaishia mahali ambapo jaribio hilo liliingia dosari kwa gari waliyokuwa wakitumia kutorokea ambayo ilikuwa ya dokta Roby Kuishiwa mafuta.

Baada ya wakina Frank kugundua kuwa gari yao imeishiwa mafuta, kila mmoja anaonekana kuingiwa na hofu hususan Zuberi mdogo wake na dokta Roby, Frank anatizama nyuma kwambali anawaona wale makachero wakija kwa kasi, Frank anamtizama Roby na kumuuliza, “mafuta yaliyobaki yanaweza kutufikisha umbali gani ?” Roby anajibu, “kama mita 300 tu! Tutafanyaje?” umbali ambao Roby ameusema ni sawa na urefu wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu, Frank anasema, ”simamisha gari”, Roby anastushwa na kauri hiyo, huku akiwa mtu mwenye hofu anauliza kwa mshangao, “Unasemaje!” Kisha anacheka kwa kejeli,”Hee heee, Jinsi tulivyo watoroka, wakitushika hapa, tutaenda kupata fahamu gerezani huku kila mmoja wetu, akiwa kapoteza lita mbili za Damu”, Frank anaongeza msisitizo kwa kusema, “sikia Roby Tukisimamisha gari wenyewe inamaanisha tutakuwa na Plan nyingine ya nini cha kufanya, na tusipofanya hivyo litaishiwa mafuta na kusimama lenyewe, then tutashikwa kiulaini kabisa”. Wakati Frank anamaliza kuzungumza hayo, Zubery ana dakia na kusema, ”nimepata wazo!” kauli ya Zubery inafanya kila mmoja amsikilize kwa makini, Zubery anasema,“Simamisha Gari, kisha Nyinyi mshuke na kukimbia”, Robi anamkatisha na kusema,”Halafu wewe na Brenda?” Zubery anajibu, “Simple! Mimi nitaangalia tension yao, kama wakishuka na kuwafukuza nyinyi sisi tutakua salama” Roby anahoji, “na what if wasipo tufata sisi wakaja kwenye Gari?“. Zubery anaonesha kukwama, Frank ananyanyua mdomo kujibu, Gari inazima Ghafla, Frank anaghairi kile alichataka kusema kisha anauliza,”yamekata?” Zubery anajibu, “hapana mafuta hayajaisha imezima tu, nyinyi shukeni…….” Frank na Roby wanatizamana kisha Frank anasema, “Tushuke” Roby anamtazama Zubery na kumwambia, Be Carefull”. Roby anataka kushuka Frank anamvuta na kumwambia apite kwenye siti za nyuma kisha ajifanye kama mgonjwa ajitundike kitambaa ambao walikua nacho kutoka Kule hosteli, Frank akapita na kutokea mlango wa Dereva, kisha kwa kasi anazunguka na kumshika Roby ambae nae anatembea kama mgonjwa aliezidiwa kisha wanaingia kwenye mitaa. Huku nyuma wanamuacha Zubery akiwa ameinama chini kabisa. Wanapo potea tu ndani ya nyumba za watu wanazindua marathon.

Mpenzi msomaji mbinu hiyo ya Frank inafanikiwa kwani wale makachero wana shuka kwenye gari yao kwa kasi na kuanza kuwafukuza kwa kupita njia tofauti tofauti kwa lengo la kuwazunguka. Makachero wanaonesha kuwa hawana wasi wasi kwani waliamini kuwa mmoja wao kati ya wale waliokuwa wakiwakimbiza alikuwa mgonjwa, hivyo hawawezi kufika mbali na watawashika bila shida.

Askari saba kati ya wale nane walio kuwa ndani ya gari wanaungana kuwafukuza na kumuacha mmoja akiwa eneo lile. Zubery anachungulia na kumuona yule askari mmoja, yule askari anakusogea kwenye lile gari taratibu mara simu yake inaita, anapokea simu na kuanza kuongea, aliekuwa akimpigia askari huyo alikuwa ni shangingi mmoja aliekuwa akimtoa njia kuu askari huyo, hivyo askari huyo analegea ghafla na mawazo ya kikazi zaidi yanabadilika na kuwa mawazo ya kimahaba.

Zubery huku akijua kuwa ni wazi kabisa kwamba akimaliza kuongea na simu askari huyo atamfata, anatumia muda huo kukaa kwenye Stering. Wale askari waliokuwa wakimkimbiza frank na Roby wanachanganywa na vichochoro vya uswahilini na kujikuta wakizunguka hapo hapo. Lugano anamwambia Bosko arudi ili akakague gari waliyoiacha, wakati wao wakiwa wanaendelea kuwasaka, huku mmoja wao akisema, “Yule mwanamke bado mgonjwa anachechemea kabisa, hawajaenda mbali watakuwa wapo eneo hili hili”. Wanazungumza maneno hayo,kumbe Frank na Roby walikuwa wamejibana ndani ya maliwato ambayo uswailini inajulikana kwa jina maarufu la PasportSize, wakati huyo askari akizungumza maneno hayo, kwa sauti ya chini Frank ansema,”akili zenu mbovu ndio zinachechemea”. Huku kwa Zubery anaingia kwenye mtihani mpya kwani gari ambayo aliamini ingewaka kutokana na jinsi alivyoizoea sasa inamgomea kuwaka. Na kitendo cha kupiga stata kinamfanya yule jamaa aliekuwa akizungumza na simu ashtuke kuwa kwenye hiyo gari bado kunamtu.

The Second Door - Episode 1Donde viven las historias. Descúbrelo ahora