The Second Door - Episode 11

103 0 0
                                    

Baada ya pilika pilika na purukushani za weekend, tunaingia katika siku mpya, ikiwa ni jumapili tulivu waumini wa madhehebu ya kikristo wakiwa kwenye movement za hapa na pale kuelekea kwenye nyumba za ibada na wengine ambao jana walikesha kwenye maeneo tofauti tofauti ya kujirusha, wakiwa bado na uchovu unaotokana na starehe za usiku kucha. Bila kusahau waliojaribu kufanya majaribio hatari kama Tarick, yeye asubuhi ya leo anaamka huku sehemu ya juu ya jicho ikiwa imechimbika kabisa. Kwa mara ya kwanza anaonana na robi, asubuhi hii Roby anastaajabu kuona jeraha kubwa kiasi kile usoni kwa Tarick wakati jana alimuacha akiwa mzima. “Imekuwaje Tarick!?” Tarick anajibu, “ilikuwa usiku wakati naenda kujisaidia nikajigonga mlangoni” Roby anasogea ili kumuangalia kwa karibu na kugundua kuwa lile jeraha lilikuwa kubwa. Kabla ya kufanya chochote dokta Roby itabidi amshone na kumpa matibabu.

Baada ya kumaliza kushughulikia lile jeraha wanakunywa chai huku huku wakitazama cd ambayo Roby alikuwa ameichukuwa jana kwa Grace. Leo walikuwa na makubaliano kuwa Zubery angekuja na Details zote ambazo Tarick inabidi azitumie. Kwajinsi walivyopanga, ilibidi Tarick aanze maisha hayo mapya kuanzia jumanne, japokuwa hili lilikuwa jaribio la hatari kabisa na jaribio ambalo lingeweza kumkamatisha Tarick kiulaini, lakini kwasasa ndio njia pekee ambayo endapo ikifanikiwa basi Tarick ataendelea kuishi bila shida kama watu wengine. CD wanayotizama muda huu ni ndefu sana, hivyo Roby anamwambia Tarick aendelee kuitazama ili yeye aende akamalizie kibarua cha kumrejesha Brender kwa Rweyemamu.

Zubery nae akiwa amedhamiria kabisa kumuuza Tarick, lakini safari hii akitumia umakini mkubwa ili asije kuingia kwenye matatizo kama yaliyomkuta kwa Frank, leo amefanikiwa kupata mawasiliano ya secretary ofisi ya kamanda mkuu kanda maalum ya dar es salaam, wanapanga kukutana kwaajili ya mazungumzo yasiyokuwa ya kiofisi ili watizame ni jinsi gani wanaweza kushirikiana kutengeneza pesa kupitia biashara hiyo ya kumuuza Tarick. Wanafanikiwa kukutana, kisha yule secretary anamhakikishia zubery kuwa dili hilo linaweza kumuingizia zaidi ya shilingi milioni themanini bila wasi wasi wowote kwani mpaka muda huu serikali inapoteza mamilioni ya pesa kila kukicha kwaajili ya kulisaka gaidi hilo lililoponyoka kutoka kwenye hukumu ya kifo. Mazungumzo hayo yanafana, hatma yake wanaishia kwa kukubaliana kuwa Huyu secretary ataenda kuzungumza na jenerali mwamkonge ili kujua kama jeshi la polisi litakuwa tayari kutoa Shillingi million 100 kwa mtu atakae fanikisha kukamatwa kwa gaidi hilo. Mazungumzo hayo yanamalizika huku secretary akimuahidi Zubery kuwa, kama kweli anauhakika anaweza kufanikisha zoezi la kukamatwa kwa mhalifu huyo basi hizo pesa zisingekuwa tatizo kabisa kutolewa, kwani kunahofu kubwa kuwa kitendo cha gaidi hilo kuingia uraiani kunaweza kupelekea tukio la mauaji makubwa zaidi kuliko yale yaliyofanywa arusha.

Tukirejea kwa dokta Roby, yeye anaenda mpaka hospitali na kumchukuwa Brenda kisha kwa kutumia line nyingine kabisa anampigia Rweyemamu na kusema, “Kishoka naongea.. Tunaweza kufanya makubaliano?” Rweyemamu kusikia swali hilo anadharau na kukata simu. Lakini ndani ya sekunde chache anashtuka na kugundua kuwa ile ilikuwa ni sauti aliyo zungumza nayo mara ya mwisho, Rweyemamu anaamua kumpigia simu swaiba wake kamanda mwamkonge na kumpa taarifa, mwamkonge unaunganisha simu hiyo kwenye mtandao wa polisi na kuwapa oda ya kufatilia mazungumzo yote, kisha anamwambia Rweyemamu apige simu ya huyo mtu bila kukata simu yake. Rweyemamu anafanya hivyo. Wakati Roby akiwaza kitu cha kufanya mara simu yake inaita, anaipokea kisha Rweyemamu anamwambia, “samahani, naomba nikufahamu kisha uniambie ulikuwa unahitaji makubaliano gani na mimi”, Roby anajibu, “Sina shida ya kufahamiana na wewe ila nataka kufahamu tu kama makubaliano ninayotaka yanaweza kukufaa” Rweyemamu anasema, “Ok, sema nakusikiliza…” bila kujua kuwa mazungumzo yao yalikuwa yakifatiliwa kwa makini na makao makuu ya jeshi la polisi, Roby anasema, “Kama utafanya kila nitakachokuelekeza, leo unampata Brenda, ukifanya kinyume ukajaribu kuleta ujanja wowote, utampata akiwa robo yake, na sehemu inayobaki hautaiona maisha yako yote” Roby anaamua kumtisha Rweyemamu ili asijaribu kushirikisha polisi kama alivyofanya awali, Roby anaendelea, “Kama unamtaka akiwa hai, fanya kama tutakavyokubaliana, ila kama kichwa chake ndio muhimu zaidi kwako jaribu kunizunguka” Rweyemamu anaanza kuogopa maneno ya Roby na kuhisi kuwa akifanya masikhara anaweza kupoteza uhai wa mpenzi wake, Rweyemamu anamkatisha Roby na kusema, “Nipo tayari kufata makubaliano yoyote tafadhari naomba nimpate akiwa mzima… hata kama unahitaji kiasi chochote cha pesa nipo tayari kukupatia” Roby anasikiliza kwa makini na kumwambia, “Hakuna kunizunguka!” kauli hiyo inamfanya Rweyemamu ajibu kwa kutetereka, “Naapa sitakuzunguka!” Roby nae bado hajiamini kabisa kwenye tukio analoenda kulifanya anasisitiza kwa kusema, “No trick no Game!” Rweyemamu kitete kinamzidi anaamua kumwambia Roby asubiri kwanza, kisha anakata simu ya generali mwamkonge na kusababisha kukatika kwa mawasiliano yaliyokuwa yakiunganisha mazungumzo hayo na makao makuu ya polisi. Baada ya hapo Rweyemamu anasema, ”Sikia kishoka, I real need that girl alive” Baada ya Rweyemamu kuzungumza kauli hiyo, Roby hakutaka kuendelea na mazungumzo yoyote moja kwamoja anamwambia, “tukutane kwenye ufukwe wa msasani saa tisa kamili hakikisha unakuja peke yako utanikuta mbele ya soko la samaki”.

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Jun 13, 2014 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

The Second Door - Episode 1Where stories live. Discover now