Sura ya kwanza

213 13 3
                                    


Nilikutana naye Mlimani City supermarket. Alionekana kuwa msichana mrembo sana, kuanzia sura yake ya kuvutia, umbo la namba nane, chuchu saa sita yani alikuwa ni mrembo kwelikweli. Kwa mara ya kwanza nilipomtazama nilijikuta nikitamani kuwa naye kimapenzi, akili yangu ikanituma nimfuate na kumwambia kile nilichokuwa nakitamani lakini moyo wangu ulisita, sikutakiwa kukurupuka kufanya hivyo.
Alionekana kuwa makini kufanya 'shopping' lakini hilo halikunitisha hata kidogo nilichoamua kukifanya ni kuanza kujongea kuelekea pale alipokuwepo huku kimoyomoyo nikijisemea 'liwalo na liwe'.
"Mambo," nilimsalimia huku nikilitengeneza tabasamu pana.
"Safi," alinijibu huku akionekana kuwa bize kuchagua bidhaa aliyokuwa akiitafuta.
"Unaonekana kuwa bize sana vipi naweza kukusaidia?"
"Hapana asante."
"Asante maana yake nini?"
"Nashukuru kwa msaada wako."
"Ok vipi naweza kukufahamu kwa jina?" nilimuuliza huku nikijifanya kama ninayetafuta kitu fulani hivi kwa kuzuga.
"Kwani kuna ulazima wa kulifahamu jina langu?" alinijibu kwa kuniuliza swali lililonifanya nimuone kuwa msichana wa matawi ya juu sana. Alikuwa hapendi mambo ya uswazi uswazi sijui kila mtu unayekutana naye unaanzisha urafiki naye mara sijui unakutana na mtu unaanza kumchekea chekea kwake haikuwa hivyo, alikuwa ni msichana fulani hivi wa gharama, wazungu wanapenda kumuita "Expensive Girl."
"Sio lazima kulifahamu lakini kama hutojali ningependa kulifahamu?"
"Wewe kaka vipi, hivi utafahamu wangapi wanaoingia supermarket hii au wewe ni mwizi nini?"
"Ndio mimi ni mwizi nataka kuliiba jina lako," nilimjibu kwa kutania na kumfanya atokwe na kicheko cha bila kukitegemea.
"Wewe kaka umetumwa?"
"Ndiyo nimetumwa na moyo wangu nikuulize kuwa unaitwa nani?"
"Sitaki."
Mpaka kufikia hapo nilikuwa nimeshafahamu kuwa alikuwa ni msichana wa aina gani, alikuwa ni miongoni mwa wale wasichana ambao wanapenda kubembelezwa, yani wao kila kitu ni kubembelezwa tu. Nilikwisha lifahamu hilo na sikutaka kulifanyia kazi niliamua kuendelea kumsumbua mpaka pale uvumilivu ulipomshinda.
"Haya naitwa Evadia," alijitambulisha huku akionekana kuchoshwa na usumbufu wangu.
"Nafurahi kukufahamu," nilimwambia kisha nikampa mkono lakini hakuupokea, aliupuuzia. Hilo halikwa tatizo kabisa, niliendelea na usumbufu wangu.
'Naitwa Dickson lakini wengi wanapenda kuniita 'Dick mapenzi'," nilijitambulisha kisha nikaanza kuondoka eneo lile kimtego.
Sikumbuki ni nini kilitokea lakini nilishangazwa na mshangao uliomkumba Evadia mara baada ya kumtajia jina langu. Alinitazama mara mbilimbili kisha akawa kama mtu ambaye haamini kile alichokuwa akikishuhudia kwa macho yake. Alilirudia kuliita jina langu halafu akanitazama usoni, safari hii ule ubize aliokuwa nao ulimuisha, akanitazama tena huku akiwa haamini kabisa kukutana na mimi mahali pale.
Labda nikuambie kitu ndugu msomaji, nilikuwa na jina kubwa sana mitandaoni, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa ni mtumiaji wa mtandao wa Istagram au facebook halafu akawa halifahamu jina langu. Wengi walikuwa wakinifahamu sana kutokana na hadithi zangu aina ya chombezo nilizokuwa nikiziandika katika mitandao hiyo, nilikuwa nikiongoza kwa kuwa na wafuatiliaji wengi wa machombezo nilizokuwa napost.
"Dick!" aliniita kwa mshango.
"Naam!" nilimuitikia halafu nikamgeukia, alizidi kunishangaa sana.
"Ni wewe?"
"Yeah! Ndiye," nilimjibu huku nikimrudia, safari hii nilijifanya kubadilika kidogo, sikutaka anielewe kwa haraka kuwa nilikuwa ni binadamu wa aina gani.
"Kwani unanifahamu?" nilimuuliza huku nikijifanya sifahamu lolote.
"Ndiyo nafuatilia sana simulizi zako mitandaoni yani kila siku nilikuwa natamani siku moja nikuone maana sio kwa simulizi zile za mapenzi unazotunga," aliniambia kisha akaja na kunikumbatia kyumbato ambalo lilinifanya nijione tayari nimeshang'oa mtoto.
"Siamini jomoni," aliniambia kwa kisauti fulani hivi kama kile cha watoto wadogo.
"Hahahaha sasa huamini nini?" nilimuambia.
"Yani kukutana na wewe kwangu ni bahati kubwa sana."
"Usijali," nilimwambia kisha nikajitoa katika kumbato.
Evadia hakutaka kuamini kama alikutana na mtu kama mimi ambaye nilikuwa nikisifika sana, wasichana wengi walikuwa wakitamani kuniona 'live' lakini lilikuwa ni jambo gumu sana kutokana na ubize niliyokuwa nao nilishindwa kukutana nao, mazungumzo mengi yaliishi kwenye simu, nilikuwa nikichat na wasichana wengi sana na kila mmoja alikuwa akionyesha kunipenda, hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana wote ambao walijilengesha mtegoni sikuweza kuwaacha nilihakikisha nawapa dozi. Alichoamua kukifanya Evadia ni kuitoa simu yake aina ya Iphone 6 yenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania kisha akaanza kupiga selfie na mimi.
Nilichokuwa nakiwaza kwa wakati huo ni kwa jinsi gani ningeweza kumpata Evadia ambaye alikuwa amenivutia sana, nilimtamani sana kiasi kwamba mtarimbo wangu ukashindwa kuvumilia mwisho ukajikuta umesimama dede.
"Unajisikiaje?" nilimuuliza huku nikimtazama, alionekana kuwa mwenye furaha sana.
"Najisikia vizuri sana."
"Nipe namba yako," nilimwambia kisha akaingiza mkono katika pochi yake, akatoka na 'business card' halafu akanipa.
"Utanitafuta."
"Muda gani?"
"Muda wowote kuwa huru Dick," aliniambia.
Nilichoamua kukifanya ni kuondoka eneo lile, sikutaka kuendelea kubaki kwani nilikuwa nazidi kujiumiza tu, mtarimbo wangu uligoma kushuka, kila nilipokuwa nikimuangalia Evadia ndiyo kwanza ulizidi kusimama dede.
"Acha mi niondoke," nilimwambia.
"Unaenda wapi?
"Kuna sehemu natakiwa kwenda."
"Kwahiyo umeghairi kufanya shopping?"
"Hapana nitafanya nikirudi," nilimuambia kisha nikaanza kuondoka, Evadia alizidi kunitazama sana, nililifahamu hilo pale nilipoamua kugeuka na kumuangalia, alikuwa akinitazama muda wote.

Tafadhali acha Maoni yako au upigie kura .

Nifanye Na Mimi Kaka Dick.  Na Juma Hiza    Where stories live. Discover now