Nilizidi kuwa katika wakati wa mawazo sana, muda wote nilikuwa nikimfikiria Evadia msichana mrembo ambaye alitokea kuuteka moyo wangu, nilichokuwa nakitamani kwake ni kuona siku moja anakuwa wangu kisha naufahamu na utamu wake.
Niliporudi nyumbani kwangu, usiku wa siku hiyo hakukuwa na kazi nyingine zaidi ya kumfikiria Evadia tu, nilizidi kujilaumu sana kwa kushindwa kumpata katika Maisha yangu.
“Haiwezekani,” nilijisemea kisha nikapiga ngumi kwenye godoro kwa ghadhabu.
Niliamua kuichukua simu yangu na kisha nikaingia kwenye kitabu cha kuhifadhi majina, nilikuwa nikijaribu kupitia jina moja baada ya lingine huku nikiyafuta yale majina ambayo nilikuwa siwasiliani nayo kabisa. Ni katika zoezi hili fupi ambapo niliweza kukutana na jina la Mick. Mick alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana, alikuwa ni mtu ambaye niliweza kusaidiana naye mambo mengi sana, ulipokuwa unauzungumzia urafiki wa kweli wa kufa na kuzikana basi usingeacha kuuzungumzia urafiki wangu na Mick. Tulifanana mambo mengi sana ila tofauti yetu ilikuwa ni moja tu. Mimi nilikuwa ni mwandishi wa Machombezo lakini yeye hakuwa mwandishi wa kitu chochote. Nakumbuka nilikuwa nikimsaidia mambo mengi sana, hasa lilipokuwa linakuja suala la wanawake waliokuwa wakimtesa niliweza kulichukua tatizo lake na kumsaidia. Nilipoliona jina lake kwa wakati ule nilishtuka sana kwani zilikuwa zimepita siku nyingi bila kuzungumza naye lolote. Sikutaka kupoteza muda, niliamua kumpigia simu kwa wakati ule, simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Safari hii nikaamua kumtumia ujumbe mfupi lakini haikuchukua dakika aliweza kunijibu.
“Mambo vipi?”
“Poa mshikaji wangu niambie.”
“Aisee mbona umekausha hivyo?”
“Mambo mengi ndugu yangu.”
“Nakupigia simu hupokei au uko na shemeji nini?”
“Hahahaha nilijua tu utasema hivyo.”
“Ulijua nini?”
“Niko peke yangu bhana.”
“Ok uko wapi sasa hivi?”
“Nyumbani.”
“Wapi?”
“Kwani wewe unajua nakaa wapi?”
“Tegeta.”
“Ndiyo.”
“Hivi wewe utakuwa lini?”
“Hahaha! Kwanini?”
“Yani umri huo uliyokuwa nao bado tu unaendelea kula ugali wa baba yako.”
“Hahaha nini wewe maisha kujipanga.”
“Ohoo shauri yako.”
“Niambie.”
“Dah! Ndugu yangu kuna mtoto ananichanganya sana akili yangu.”
“Yupi tena huyo maana wewe kila siku huishiwi na vioja.”
“Hahahaha! Mtoto mmoja wa kishua yani anapenda kusoma chombezo zangu lakini kila nikitupia ndoano anachomoa.”
“Hahaha! Sasa utafanyaje?”
“Lakini lazima nimpate tu!.”
“Sawa nakuaminia.”
“Poa.”
Nilichokuwa nimepanga kumfanyia Evadia kwa wakati ule ni kuhack akaunti yake ya WhatsApp pamoja na Facebook. Niliamua kumfanyia mchezo huo kwa makusudi kabisa kwani niliamini udhaifu wake ulikuwa katika mitandao. Alikuwa akipenda sana kuchat, kusoma hadithi pamoja na kuperuzi mambo mbalimbali katika mitandao hii.
Sikuacha kuchat naye kupitia ile namba yangu ambayo alikuwa akinifahamu kwa jina la Majaliwa Majuni, niliendelea kumtumia ujumbe mfupi wa kumchombeza huku kila siku akionekana kunipuuzia. Kuna muda alikuwa akinitukana na kuniambia kuwa alikuwa haitaji usumbufu kabisa. Hilo halikunifanya niache kumsumbua, nilizidi kumtumia ujumbe mfupi mpaka pale siku nilipoamua kuzihack akaunti zake na kila kitu alichokuwa anakifanya nilikuwa nikikiona, kuna kipindi nilikuwa nikibadilisha ‘Profile’ yake WhatsApp na kuweka picha ya bibi kizee bila ya yeye kufahamu lolote.
“Mambo mrembo?” nilimtumia ujumbe mfupi siku moja majira ya asubuhi kwa namba yangu ambayo alikuwa akiifahamu, hapa ilikuwa ni baada ya kuzihack akaunti zake.
“Poa Dick niambie.”
“Niko poa sema umenichunia sana.”
“Hamna bhana ubize tu ndugu yangu.”
“Sawa ila vipi lakini uko fresh?”
“Niko poa ila sio sana.”
“Vipi unaumwa?”
“Hapana?”
“Nini tatizo.”
“Kuna mtu amezihack akaunti zangu yani ananifanya mpaka nakosa furaha kabisa.”
“Sasa hilo ndilo linalokuumiza.”
“Ndiyo.”
“Mbona ni tatizo dogo sana.”
“Unaweza kulitatua?”
“Ndiyo kwani wewe uko wapi?”
“Niko hapa dukani.”
“Njoo basi nyumbani kama utaweza maana hapa kuna kazi nazifanya.”
“Hivi ulisema ni wapi tena?”
“Tandale kwa Tumbo.”
“Mmh! Kwahiyo nije?”
“Ndiyo mbona unaguna sasa.”
“Hamna! Kwahiyo nikifika hapo Tandale kwa Tumbo nikwambie.”
“Ndiyo ukifika niambie nitakufuata.”
“Sawa nakuja,”alinijibu kisha nikaanza kuandaa maziloongira ya chumba changu vyema kwa ajili ya mapambano, sikutaka siku ile ipite hivihivi bila kuufahamu utamu wake.Nje kutaendelea aje?
Shukrani za dhati wapenzi wasomaji kwa hiki kitabu kimekua cha kwanza katka kitengo cha mapenzi
#1-ROMANCE
YOU ARE READING
Nifanye Na Mimi Kaka Dick. Na Juma Hiza
RomanceKijana aliye fanikiwa kuwa hodari sana alijitoza katika anasa za dunia......