Nilitumia dakika chache kutoka Sinza mpaka Tandale kwa Tumbo nilipokuwa naishi, hata hivyo niliweza kuchukua usafiri wa bodaboda ambao uliweza kunifikisha kwa haraka zaidi.
Kichwani mwangu hakukuwa na kitu nilichokuwa nakifikiria zaidi ya Evadia msicha nilijikuta natokea kumkumbuka sana. Moyo wangu ulihisi kitu cha tofauti sana. Nilipoingia katika chumba changu kitu cha kwanza kabisa nilichokifanya ni kuanza kuitafuta suruali ambayo niliivaa siku ile ambayo niliweza kwenda nayo Mlimani City, niliamini kwa asilimia zote kuwa 'business card' ilikuwemo katika mfuko moja wapo. Nilianza kutafuta kwa utulivu na hatimaye niliweza kuipata, niliizamisha mikono yangu ndani ya mifuko yake, naam! Ilikuwa kama matarajio yangu, niliikuta 'business card'. Niliichukua na kuanza kuisoma kwa umakini wa hali ya juu.
Evadia alikuwa akimiliki duka kubwa la nguo lililokuwa likijulikana kwa jina la 'Eva Fashion Wear' lilikuwa ni duka kubwa lililokuwepo Kinondoni. Sikutaka kujali jina la duka wala ule urembo uliyokuwepo katika ile 'business card' kitu nilichokuwa nakiangalia ni namba za simu. Sikutaka kupoteza muda haraka niliitoa simu yangu na kuanza kunakili namba za simu za Evadia, moyoni nilikuwa nashahuku ya kutaka kuwasiliana naye. Nilipohakikisha zimetimia namba kumi nilizisave kabisa, nakumbuka nilimsave kwa jina la 'Eva' ikiwa ni kifupi cha jina lake halisi.
Akili ilinituma nimpigie lakini nilisita, nilihisi kutojipanga kwa mazungumzo yetu. Nilichoamua kukifanya ni kuingia upande wa WhatsApp na kuanza kumuangalia kama alikuwa online, hakuwa online kwa wakati huo lakini nilipotazama muda aliyotoka hayakuwa yamepita masaa mawili tangu alipotoka.
Alikuwa ameweka picha ya kikatuni ambacho kilikuwa kikionekana kuwa na furaha lakini nilipoangalia upande wa 'status' yake alikuwa ameandika maneno ambayo kwa kweli yalinifanya nicheke mwenyewe kama mwendawazimu baada ya kuyasoma, alikuwa ameandika maneno yaliyosomeka "Utamu wa kaka Dick." Kisha akayasindikiza kwa kuweka kimdoli kilichokuwa kina macho ya kopa.
Mpaka kufikia wakati huo nilijiona kuwa mshindi tayari yani kama ni mbuzi basi alikuwa amefia kwa muuza supu. Wakati nilipokuwa nikiendelea kumuangalia ghafla! Nilimuona akirudi online. Sikutaka kupoteza muda niliamua kumtumia ujumbe mfupi, nakumbuka sikuwa nimeweka picha yoyote kwenye 'profile' yangu hivyo ilikuwa ni ngumu sana kunifahamu.
"Mambo mrembo."
"Nani mwenzangu."
"Pokea kwanza salamu halafu ndiyo uniulize kuwa mimi nani?"
"Okey poa, nani wewe?"
"Vipi kwani kuna ubaya wowote hata usiponifahamu?"
"Unajua sikuelewi embu jitambulishe halafu sema shida yako."
"Naitwa Majaliwa Majuni."
"Majaliwa?"
"Ndiyo."
"Wa wapi?"
"Nipo Dar."
"Dar sehemu gani?"
"Mbagala ila kwa sasa niko hapa Mwenge."
"Mbagala?"
"Ndiyo."
"Nikusaidie nini?"
"Wewe ndiyo Evadia?"
"Yes ndiyo mimi nikusaidie nini?"
"Nimeona matangazo ya nguo zako mitandaoni sijui naweza kupata huduma na mimi?"
"Yeah! Unaweza kupata ni pesa zako tu."
"Ok unapatikana sehemu gani?"
"Duka langu lipo Kinondoni wewe ukifika tu hapo nitafute nitakuja kukuchukua."
"Nitashukuru dada yangu."
"Poa."
Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa chatting zetu, nilikuwa nimechart naye lakini mpaka kufikia wakati ule hakuwa amenifahamu kabisa, alionekana kuwa na dharau kiasi fulani lakini sikutaka kujali sana, nilichokuwa nimepanga kwa wakati huo ni kwenda kukutana naye hukohuko kwenye duka lake la nguo, niliamini pindi ambapo angeweza kuniona hakika asingeweza kuamini macho yake, nililifahamu hilo kutokana na umaarufu wangu wa kuandika machombezo mitandaoni, nilikuwa nikipendwa sana, kila mwanamke alikuwa akitamani kuniona hii ilisababishwa na kipaji changu. Machombezo yangu yalikuwa yakiwasisimua sana watu, nilikuwa nikipokea jumbe mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa hadithi waliyokuwa wakiyafatilia machombezo yangu, walikuwa wakinilalamikia kwa kuwaumiza kila siku na machombezo yangu.
****
Niliamua kwenda kuoga kisha nikajiandaa vyema tayari kwa safari ya kwenda kukutana na Evadia ambaye kwa wakati ule alikuwa akinifahamu kwa jina la Majaliwa Majuni, niliamua kumdanganya jina langu kwa makusudi kabisa kwani kama ningeweza kumtajia jina langu halisi nadhani hata leo hii ninapokusimulia chombezo hili kamwe lisingeweza kukuvutia kwani ungeshafahamu kila kitu ambacho kilikuwa kinakwenda kutokea. Nakumbuka yalikuwa ni majira ya saa tisa kasoro, nilitoka katika chumba changu na sasa ilikuwa ni safari ya kuelekea maeno ya Kinondoni lilipokuwa duka la Evadia msichana ambaye nilipanga kutoka naye kimapenzi. Nilikumbuka kumtumia ujumbe mfupi WhatsApp kumfahamisha kuwa nilikuwa naenda kwenye duka lake.
"Ndiyo nakuja Dada Eva."
"Sawa haina shida ukifika utaniambia."
"Haya," nilimjibu kama mtu fulani ambaye nilikuwa mshamba, nilifahamu kuwa hata Evadia naye alinidharau kwani kila ujumbe ambao nilikuwa nikimtumia alionekana kuudharau na kunijibu kama mtu ambaye alikuwa akilazimishwa kujibu.Maoni ya sura hii.
Imekua ya Kumi katika kutengo ya mapenzi
#10 Romance
YOU ARE READING
Nifanye Na Mimi Kaka Dick. Na Juma Hiza
RomanceKijana aliye fanikiwa kuwa hodari sana alijitoza katika anasa za dunia......