Barabarani Precious alionekana kuwa ni mchangamfu sana, alikuwa akizungumza na mimi utadhani tulikuwa ni marafiki wa muda mrefu kumbe siku ile ndiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kuonana. Hahaha! Wanawake bhana ati! Ameniamini kabisa kiasi cha kunipa na lift.
"Hivi ulisema unaishi wapi vile?" aliniuliza hapa tulikuwa tumefika yalipo makutano ya barabara ya Mwenge kwa wakati huo tulikuwa tumeikamata barabara iliyokuwa inaelekea Makumbusho.
"Magomeni sijui," nilijibu huku nikijifanya nimesahau.
"Hee! ni Magomeni au Tandale?" aliniuliza huku akinitazama kwa kujiibaiba.
"Kumbe unajua halafu unanichora," nilimjibu kisha akatabasamu, tabasamu lilelile lililojenga vishomo mashavuni mwake 'Dimpoz', alizidi kuonekana mzuri mno.
"Hivi ulisema unaitwa nani?" aliniuliza tena hapa tulikuwa tumeshafika Bamaga.
"Sijui Dick?"
"Dick au Akili?"
"Yeah! Yote majina yangu hayo ila wengi wanapenda kuniita Dick mapenzi," nilimjibu.
Sikumbuki ni nini kilitokea ila nilishangaa Precious akinitazama kwa mshangao, hakunisemesha chochote alibaki akiwa ameduwaa tu kama sanamu.
"Kuna nini?"nilimuuliza.
"Dick!"
"Naam."
"Ndiyo wewe."
"Kwani unanifahamu?"
"Ndiyo wewe au?"
"Hapana ni wewe."
"Hahaha! Bana acha utani ujue mimi namaanisha?"
"Ndiyo ni mimi."
"Mimi pia ni shabiki yako huwa napenda sana kusomaga machombezo yako," aliniambia kisha akawa kama mtu fulani hivi ambaye hakuwa akiamini kama alikutana na mtu kama mimi.
"Chombezo langu lipi unalipenda sana?" nilimuuliza swali la kichokozi kabisa.
"Yako mengi sana ila kiukweli lile chombezo lako la Chumba cha masaji nililipenda sana yani kila nikilisoma mwili unanisisimka," alinijibu kisha nikacheka kwa makusudi kabisa.
"Mbona unacheka sasa?" aliniuliza, hapa tayari tulikuwa tumeshafika Sinza Palestina, kulikuwa na foleni yakizushi.
"Nilitaka kushangaa yani usisimke?"
"Kwanini?"
"Haya maswali ya kwanini kawaulize wasanii mimi siwezi kulijibu."
"Hahahaha!"
"Unanicheka halafu."
"Hapana."
"Ila?"
"Unaonekana kuwa mchekeshaji sana."
"Sana tu mpaka kitandani mimi ni mchekeshaji balaa."
"Mmh! Huko kitandani vipi?"
"Si nachekesha tu!?"
"Makubwa!"
"Madogo yananafuu."
"Hahahaha! Bhana acha kunichekesha mimi."
"Hahahaha!"
"Unaishi na nani"
"Naishi na jina langu."
"Jina lako?"
"Ndiyo yani naishi peke yangu."
"Wifi?"
"Sina smart phone."
"Nini?"
"Wi-Fi situmiagi."
"Hahahaha! Bhana hujaoa?"
"Bado niponipo kwanza."
"Unasema?"
"Bado nipo nipo sana tu!"
"Mmh!"
"Sasa unaguna nini?"
"Yani umaarufu wako wote huo hujaoa?"
"Wanawake nyie mnazingua."
"Kwanini?"
"Mkipendwa hampendeki."
"Sio kweli."
"Kweli hata wewe unaonekana ndiyo walewale."
"Ah! Wapi sio kweli."
"Nitaamini vipi?" nilimuuliza kisha akacheka kwa aibu, ni hapa ambapo niligundua udhaifu wake. Alikuwa ni msichana mwenye aibu sana, kwake neno hapana halikuzoeleka midomoni mwake, hilo nililifahamu mapema sana na nilipanga kuutumia mpaka akubali kwenda na mimi magetoni.
"Mimi sio muhuni bana," alinijibu hapo tayari tulikuwa tumefika tandale darajani.
"Nitaamini vipi?"
"Wewe niamini tu!"
"Nikuulize kitu?"
"Ndiyo niliulize."
"Hivi unaweza kumuamini mwizi aleyetubu?"
'Hapana."
"Kwanini kwasababu alikuwa ni mwizi."
"Basi na mimi sikuamini."
"Hahaha! Kwahiyo mimi ni mwizi."
"Hilo umesema wewe."
"Unavituko wewe?"
"Kidogo tu! sio sana."
"Niambie."
"Nikikuambia utakubali?"
"Ndiyo."
"Twende kwangu."
"Kwako?"
"Ndiyo."
"Tukafanyaje?"
"Ukapafahamu tu ili hata siku ukitaka nikusimulie hadithi unakuja tu."
"Hahaha! Nitachelewa bhana."
"Huchelewi sekunde ishirini tu! halafu unaondoka zako."
"Sawa sasa hivi saa ngapi?"
"Saa kumi na mbili."
"Halafu giza linaanza kuingia."
"Tutawasha taa," nilijibu, jibu lililomfanya akacheka.
Tulifika Tandale kwa Tumbo kisha tukatafuta sehemu salama ya kuegesha gari, baada ya kuegesha gari sasa safari ya kuelekea magetoni ikaanza. Moyoni nilikuwa nikijiambia 'Leo lazima akafe mtu hawezi kutoka salama."Tafadhali acha Maoni yako au upigie kura
YOU ARE READING
Nifanye Na Mimi Kaka Dick. Na Juma Hiza
RomanceKijana aliye fanikiwa kuwa hodari sana alijitoza katika anasa za dunia......