Sura ya kumi na mbili

112 4 0
                                    


Nakumbuka yalikuwa ni majira ya saa tisa kasoro, nilitoka katika chumba changu na sasa ilikuwa ni safari ya kuelekea maeno ya Kinondoni lilipokuwa duka la Evadia msichana ambaye nilipanga kutoka naye kimapenzi. Nilikumbuka kumtumia ujumbe mfupi WhatsApp kumfahamisha kuwa nilikuwa naenda kwenye duka lake.
"Ndiyo nakuja Dada Eva."
"Sawa haina shida ukifika utaniambia."
"Haya," nilimjibu kama mtu fulani ambaye nilikuwa mshamba, nilifahamu kuwa hata Evadia naye alinidharau kwani kila ujumbe ambao nilikuwa nikimtumia alionekana kuudharau na kunijibu kama mtu ambaye alikuwa akilazimishwa kujibu.
SONGA NAYO......
Kutoka Tandale mahali nilipokuwa nikiishi mpaka lilipokuwepo duka la Evadia maeneo ya Kinondoni hapakuwa na umbali mkubwa sana, niliweza kufika na kwa wakati huo nilikuwa nje ya duka moja kubwa lililoonekana kuwa na kila aina ya nguo za kisasa. Lilikuwa ni duka la nguo za kiume pamoja na za watoto.
Nilikuwa nikilitazama katika namna ya kutamani kila kitu, sikutaka kuingia ndani kwa wakati ule niliamua kumpigia simu, haikuchukua sekunde nyingi tangu simu yake ilipokuwa inaita kisha alipokea.
"Hallo,"alisema huku akionekana kuwa bize.
"Naam!."
"Nani?"
"Umenisahau mara hii tena?"
"Ooh! Nani Majaliwa sijui?"
"Ndiyo."
"Umefika?"
"Ndiyo."
"Uko wapi?"
"Niko hapa nje."
"Ingia basi ndani."
"Hapana njoo tu kwa hapa nje."
"Ok sawa nakuja basi."
"Sawa," nilijibu kisha nikakata simu, nilikuwa nikimsubiria Evadia ambaye aliniambia kuwa muda mfupi alikuwa akinifuata. Nilijitathmini ile suruali ya kadeti iliyokuwa imenikaa vyema huku juu nikiwa nimevalia T-Shert aina ya Manga pamoja na kikoti cha kizushi ambacho niliamua kukivaa kwa lengo la kumechisha na kofia aina ya pama niliyokuwa nimeivaa, ilikuwa na rangi ya kijivu. Nilionekana kuwa wa kisasa zaidi hasa ukizingatia mahali nilipokuwepo palikuwa ni pa kijanja pia, kila kona nilikuwa nimezungukwa na maduka ya nguo.
Wakati nilipokuwa nikiendelea kujitathmini mara simu yangu ikawa inaita, nilipoangalia nililiona jina la Eva likisomeka. Haraka niliyatupa macho yangu kwenye langu kuu la duka lake ili niweze kumuangalia. Nilimuona akiwa katika wakati wa kuweweseka hakujua ni wapi mtu huyo aliyekuwa akimpigia simu alipo. Nililifahamu hilo na hivyo sikutaka kuipokea, niliamua kuikata kwa makusudi kitendo ambacho kilimuudhu sana, nilimuona akitokwa na mfyonzo kisha akawa kama anayetaka kurudi ndani.
"Eva!" nilimuita lakini kutokana na ile kofia aina ya pama niliyokuwa nimeivaa hakuweza kuiona vizuri sura yangu kwa wakati ule. Alikuwa akinitazama tu bila kusema lolote kwa wakati ule.
"Eva!" nilimuita tena safari hii nilikuwa nikipiga hatua kumfuata pale alipokuwa amesimama, alikuwa amesimama karibia na mlango wa duka lile.
"Unaniita mimi?" aliniuliza huku akijinyooshea kidole.
"Ndiyo."
"Unasemaje?"
"Umenisahau?"
"Nikukumbuke kwani we....." kabla hajamaliza kusema sentensi yake niliamua kuitoka ile kofia na sasa aliweza kupata wasaa wa kunitazama kwa uzuri kabisa. Hakutaka kuamini macho yake kwa kile alichokuwa anakishukudia, kuniona kwa wakati tena katika duka lake hakika hakutaka kuamini kabisa.
"Dick ni wewe?" aliniuliza kisha akafyatuka kutoka pale alipokuwa amesimama na kuja kunikumbatia kumbato ambalo kiukweli lilinifanya nihisi kitu cha tofauti mwilini mwangu. Evadia alikuwa na joto la kipekee sana. Harufu yake ya manukato aliyokuwa akinukia yalizidi kunifanya niwaze mambo mengi sana mengine ambayo hata hayajulikani.
"Dick," aliniita kipindi tulipokuwa tumekumbatiana.
"Niambie," nilimwambia huku nikimpigapiga kwa utulivu mgongoni.
"Siamini kama nimekuona tena."
"Amini sasa ndiyo umeshaniona," nilimwambia kisha akajitoa katika lile kumbato halafu kazi iliyokuwa imebakia ni kuanza kunitazama. Alikuwa akinitazama mpaka kuna kipindi nilianza kuona aibu.
"Mbona unanitazama hivyo."
"Siamini."
"Huamininini sasa?"
"Kama ningekuona tena."
"Hahahaha."
"Mbona unacheka sasa."
"Kwani wewe ulikuwa unamfuata nani sasa huku nje?"
"Kuna mjinga mmoja kaniambia nije kumchukua sasa natoka simuoni mpaka ameniudhi yani kama sio huyo mtu nadhani hata nisingekuona."
"Hahaha! Mshukuru sasa."
"Nimshukuru nani?"
"Huyo mtu ambaye amekufanya utoke nje."
"Hahaha na kweli?"
"Dick."
"Niambie Mrembo."
"Yani hata sijui nianzie wapi kwanza hii sio sehemu nzuri kwa ajili ya mazungumzo embu kama hutojali twende sehemu hivi tukakae ili tuongee mawili matatu."
"Na dukani je?"
"Kuna msichana nimemuajiri yeye ndiye anayenisaidia hivyo usijali."
"Sawa."
"Nisubiri basi ili nimuage."
"Usijali," nilimjibu kisha akaingia ndani na baada ya dakika kadhaa aliweza kutoka. Tuliongozana mpaka sehemu ya maegesho ya magari, aliniambia niingie katika moja ya gari aina ya Harrier kisha na yeye akaingia akawasha gari tukaondoka eneo lile. Safari yetu fupi ilikwenda kuishia katika moja ya Restaurant moja ambayo ilikuwa maeneo Mwananyamala na hapo tulikwenda kwa nia moja tu! ya mazungumzo.
Mpaka kufikia kwa wakati ule sikuwa nimemwambia ukweli kuwa mimi ndiye niliyekuwa nimempigia simu, niliamua kumficha huku nikiwa na maana yangu ya msingi.

Tafadhali toa maoni au upige kura.

Maoni yenu Kuhusu sura hii?

Shukrani za dhati wapenzi wasomaji kwa hiki kitabu kimekua cha nne katika kutengo cha mapenzi

#4- Romance

Nifanye Na Mimi Kaka Dick.  Na Juma Hiza    Where stories live. Discover now