Samahani kwa kupotea sasa nipo. Bi kazi zilikua mingi Zaidi
Karibu kwa sura ya kumi na Saba
“Evadia,” nilimuita huku nikimuinua uso wake taratibu aliyokuwa ameuelekezea chini na sasa tulikuwa tukitazamana uso kwa uso, macho yake ya huba aliyokuwa akinitazama yalinifanya nizidi kuingiwa na jinamizi la mapenzi.
“Abee,” aliitika kwa sauti nyororo ya huba.
“Naomba unisamehe,” nilimwambia kisha nikaishika mikono yake halafu nikawa kama naipapasa, aliwahi kuitoka kisha akavuta pumzi nzito kwa pupa na kuichaia.
“Nikusamehe nini?” aliniuliza.
“Najua nimekosea sana wala hayakuwa matarajio yako mpaka umeamua kufanya mapenzi na mimi, ni shetani tu! alinipitia,” nilimwambia huku nimtazama, alionekana kuwa na mawazo sana, kabla sijamruhusu aseme lolote kwa wakati ule niliwahi kumuuliza.
“Mbona una mawazo?”
“Hapana siwazi.”
“Unaonekana una mawazo sana.”
“Hapana niko sawa.”
“Kweli?”
“Ndiyo wala usijali.”
“Basi niambie kitu.”
“Nikwambie kuhusu nini?”
“Dah!”
Nilifahamu fika mpaka kufikia wakati ule nilikuwa nimemkosea sana, nilimfanyia kitu ambacho hakutegemea kufanyiwa. Nilikuwa nikijilaumu nafsi kwa kitendo kile nilichokuwa nimekifanya hata hivyo nilikuwa nimeshachelewa kwani hata nilivyokuwa nazidi kujilaumu wala lawama hizo hazikuweza kusaidia lolote lile.
“Dick,” aliniita.
“Niambie Evadia.”
“Hiki ulichonifanyia ndicho ulichoniitia kwako?”
“Hapana.”
“Sasa kwanini umeamua kunifanyia hivyo?”
“Ni ibilisi alinipitia.”
“Ibilisi!”
“Ndiyo.”
“Sawa,” alinijibu kisha akaamka pale kitandani na kuanza kuvaa nguo zake, nilipomtazama usoni alionekana kuchukizwa mno na kitendo ambacho nilikuwa nimemfanyia.
“Nisamehe,” nilimwambia lakini hakuweza kusema lolote lile, alizidi kuzivaa nguo zake na sasa alikuwa tayari amemaliza.
“Dick nashukuru sana,” aliniambia kisha akatoka nje, nilijaribu kumzuia kadri niwezavyo lakini haikuweza kusaidia lolote lile, aliamua kuondoka kwa ghadhabu.
Nilibaki mule chumbani kwangu huku nikijutia kwa kitendo nilichokuwa nimekifanya, ni kweli nilikuwa nina wasichana wengi sana ambao walikuwa wakinipenda sana tena lilipokuja suala la kufanya mapenzi nilikuwa situmii nguvu hata kidogo, walikuwa wakitamani kufanya mapenzi na mimi. Kitendo nilichokuwa nimekifanya kwa Evadia kilikuwa ni kitendo cha kikatili ambacho kwa kweli kiliniumiza sana, sikuwahi kuwaza kuwa kuna siku itatokea nitaweza kugombana na msichana huyo ambaye alikuwa ni mmoja wa mashabiki wangu waliyokuwa wakiyapenda sana machombezo yangu, kuna kipindi alikuwa akiniambia kuwa alikuwa akikesha usiku mzima kwa ajili ya kusoma chombezo zangu zilizokuwa zikimsisimua mpaka akawa anajichafua mwenyewe bila kutarajia.
“Aaaghhhh!” niling’aka kisha nikapiga ngumi kwenye godoro, nilikuwa katika wakati wa majuto.
Niliamini nilikuwa tayari nimeshampoteza Evadia katika maisha yangu, katika maisha ya simulizi na chombezo ambazo nilikuwa nikiziandika, niliamini sikutakiwa kumuona tena Evadia msichana ambaye kwa kweli alikuwa na uzuri wa kipekee sana na laiti kama ungepata bahati ya kukutana naye naamini ungeyasahili maneno yangu kwa kukubali kuwa alikuwa ni mzuri haswaa.
Sikutaka kuendelea kujilaumu pale kitandani, niliamua kumpigia simu lakini hakuwa akipokea, niliendelea kumpigia na mwisho alikuwa akinikatia. Nilizidi kuwa katika wakati wa mawazo sana hasa baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimemkosea sana Evadia.
Nilimpigia simu Mick yule rafiki yangu mkubwa sana ambaye nilikuwa nikisaidiana naye mambo mengi na mara baada ya kumpigia aliweza kupokea.
“Niambie mzee wa totoz,” aliniambia mara baada ya kupokea.
“Ndugu yangu we acha tu!”
“Niache nini sasa?”
“Yule mtoto ameingia kingi mwenyewe.”
“Duh! We noma kaka kwahiyo umeshajilia vya utamu.”
“Nadhani unanifahamu vizuri huwa sicheleweshagi lakini kuna tatizo.”
“Tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Nimefanya naye mapenzi kwa kumlazimisha.”
“Kivipi?”
“Hakuwa amepanga kufanya mapenzi na mimi.”
“Kwahiyo alikuja magetoni kuimba taarabu au?”
“Hapana kuna mchezo nilimchezea.”
“Mchezo gani?”
“Nilizihack akaunti zake na niliamua kutumia njia hii ili aweze kuja geto kwa lengo la kumtatulia tatizo lake na kweli aliweza kuja.”
“Kwahiyo kumtatulia tatizo ukamtatua kweli.”
“Dah! Mtoto kaniona mimi sio kabisa ameondoka lakini anaonekana kukasirishwa sana na kitendo nilichokuwa nimemfanyia.”
“Dah!”
“We acha tu ndugu yangu.”
“Sema Dick wewe sio wa kulilia wanawake kwani huyo mmoja akiondoka kuna nini, utakuwa umepungukiwa na nini wakati kila siku wanawake wanazidi kujigonga kwako.”
“Tatizo sio hilo.”
“Tatizo sio hilo ni nini sasa?”
“Hivi umemuona au unazungumza tu.”
“Wazuri wangapi bhana umekutana nao?”
“Mick baadae.”
“Hahaha! Haya bhana naona mtoto amekuchanganya,” aliniambia na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu kwenye simu.
Nilizidi kuwa katika wakati wa mawazo sana, sikuwa najua nilitakiwa kufanya nini kwa wakati huo ili niweze kumrudisha Evadia katika hali yake ya usawa aliyokuwa nayo mwanzo, nilikuwa nimemkosea tena nilikuwa nimemkosea kikubwa sana.
Wakati nikiendelea kuwaza na kuwazua ghafla! Ukaingia ujumbe kwenye simu yangu, haraka niliufungua, ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Precious na alikuwa ameniandikia hivi;
“Mbona umenibadilikia ghafla! Jamani Dick, hutaki kuwasiliana na mimi tena wala hutaki kunijulia hali kabisa au kwa kuwa umeshanijua mwili wangu? Ok basi mimi nilikuwa nakujulia hali. Mchana mwema nakupenda sana.”Nje kutaendelea aje,?
Maoni ya sura hii.
Imekua ya Kumi katika kutengo ya mapenzi
#10 Romance
YOU ARE READING
Nifanye Na Mimi Kaka Dick. Na Juma Hiza
Lãng mạnKijana aliye fanikiwa kuwa hodari sana alijitoza katika anasa za dunia......