Precious aliondoka na kuniacha mule chumbani huku nikiendelea kushangaa, nilikuwa siamini kama kweli alikuwa amenipa kiasi kile cha pesa ambazo aliniambia kuwa zilikuwa ni za matumizi madogomadogo.
Hakukuwa na kazi kubwa niliyokuwa naifanya kwake au biashara yoyote kubwa niliyokuwa nikiifanya kiasi kwamba aweze kunilipa kiasi kile cha pesa tena katika siku moja. Kuna watu maofisini wengine ni wasakatonge wanahangaika mitaani usiku na mchana kuitafuta hata japo shilingi elfu moja wanaikosa lakini mimi ndani ya asubuhi moja ile kuamka tu nakumbana na kiasi kile cha pesa ambazo zilikuwa ni kama pongezi kwa shughuli ya usiku kucha niliyokuwa nikiifanya juu ya kifua cha mke wa mtu ambaye alitokea kulewa na penzi langu kiasi cha kuwa chizi kabisa.
Nilichoamua kukifanya kwa wakati ule ni kuchukua Laptop yangu kisha nikaingia mtandaoni Facebook pamoja na Instagram ambapo nikaweza kupost machombezo yangu mawili ambayo yalikuwa yakipendwa sana, yalikuwa yakifuatiliwa sana na idadi kubwa ya watu ambao walionekana kuyapenda kupitiliza, kila siku yalikuwa akinipa mashabiki wapya. Machombezo hayo moja lilikuwa ni CHUMBA CHA MASAJI ambalo nilikuwa nikilipost Facebook na lingine lilikuwa ni NITABAKI NA WEWE TU! ambalo nilikuwa nikilipost Instagram na machombezo yote yalikuwa yakifuatiliwa sana, naweza kusema tangu nilipokuwa nimeanza kazi yangu hii ya uandishi wa machombezo haya ndiyo yalikuwa machombezo bora, machombezo yaliyowahi kunipa umaarufu mkubwa sana hasa katika mitandao ya kijamii, kila kona jina langu la Kaka Dick au Dick Mapenzi lilikuwa likifahamika, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa hanifahamu. Kila siku simu yangu haikuacha kupigiwa na namba ngeni, nilikuwa nikipigiwa sana na namba ngeni mpaka kuna wakati nikaanza kuhisi usumbufu.
“Kaka Dick napenda sana machombezo yako yani pindi niyasomapo huwa nahisi msisimko wa hatari hongera sana,” ilikuwa ni sauti nyororo ambayo ilikuwa ikizungumza kwa upande wa pili mara baada ya kupokea simu, ilikuwa ni namba ngeni kwa wakati huo.
“Asante sana ila hujaniambia unaitwa nani?” nilimuuliza kwa sauti ya utulivu, hapa ni baada ya kugundua kuwa mpigaji wa simu alikuwa ni msichana ambaye alijaaliwa sauti nzuri sana ya kuvutia.
“Oooh, naitwa Helena napenda sana kusoma machombezo yako,” alijitambulisha Helena kwa sauti ya ukarimu.
“Nashukuru kukufahamu.”
“Asante sana Kaka Dick hivi unaishi wapi?”
“Mimi niko Dar.”
“Hata mimi niko Dar wewe uko sehemu gani?”
“Tandale.”
“Wooo, Tandale?”
“Ndiyo kwani vipi?”
“Kumbe ni jirani yangu kabisa mimi mwenyewe niko Tandale.”
“Mimi niko kwa Tumbo na wewe je?”
“Mtogole.”
“Duh! Haya karibu Magetoni.”
“Kwani unaishi geto wewe?”
“Ndiyo.”
“Kwani hauna wazazi?”
“Ninao.”
“Sasa kwanini hauishi nao?”
“Katika maisha kuna kipindi kinafika inabidi mtu ukajitengenezee maisha yako hata ndege nao kuna kipindi kinafikia wanatengena na kila mmoja anaenda kutengeneza kiota chake au na hilo pia mgeni?”
“Hapana ila ni vizuri sana nimependa kwa kuwa umekuwa kijana wa kitofauti sana.”
“Kwanini?”
“Ni vijana wachache sana ambao wanakumbuka kama hayo unayoyazungumza na kuyafanyia kazi.”
“Ni kweli.”
“Nafurahi sana kuzungumza na wewe Dick yani nilikuwa natamani sana siku moja kukusikia japo sauti yako kumbe una sauti nzuri hivyo.”
“Hahahaha! Mbona unanipaka mafuta juu ya shati?”
“Hahahaha! Kweli tena.”
“Hahahaha haya bhana.”
“Baadae.”
“Poa poa,” nilimjibu kisha akakata simu.
Nilianza kucheka mwenyewe maana nilifahamu fika kama ni swala basi alikuwa tayari ameingia kwenye anga za Simba, ilikuwa ni vigumu sana kuweza kutoka salama, ni lazima angeliwa nyama.
Nimewahi kutembea na wasichana wengi sana, nimejaribu kuwasikia sauti zao nyororo tena wengine walikuwa na sauti nzito mbaya lakini sauti ya Helena msichana ambaye alijitambulisha simuni hakika ilikuwa na utofauti mkubwa sana, kuna kitu cha ziada nilihisi kilikuwa kimeongezeka. Moyo wangu ukaanza kutamani penzi hata kabla ya kumuona msichana mwenyewe alikuwa amefananaje, niliishi Tandale kwa muda mrefu sana, nilikuwa nawafahamu baadhi ya wasichana waliyokuwa wakiishi humo, kwa kweli walikuwa wamejaaliwa japo akina Mwajuma Binti Mafujo walikuwepo wengi lakini idadi yao haikuweza kuwafunika wale wasichana wengine wakarimu ambao wangeweza hata kuolewa kabisa.
Nilianza mchezo wangu wa kuchat naye, mchezo ambao katika maisha yangu nilikuwa nikiupenda sana, hii ilitokana na umahiri wangu wa kucheza na maneno katika kupangilia beti zangu ambazo kwa kweli hata kama angekuwa ni msichana mgumu kiasi gani endapo angeweza kunipa nafasi ya kuwasiliana naye kwa njia ya Message (Ujumbe mfupi.) basi ungenihesabia masaa tu! kwani nilikuwa ninauwezo wa kipekee sana katika kumshawishi msichana mpaka abadili mawazo yake.
“Mambo mdada,” nilimtumia ujumbe mfupi hapa ni baada ya kukaa kimya kwa muda wa masaa kadhaa tangu alipoweza kunipigia simu na kama vile nilikuwa nimemtumia ujumbe muda muafaka kabisa mtoto naye akaweza kunijibu bila choyo nikaanza kumchombeza.
“Poa Dick yani nina furaha jamani.”
“Furaha ya nini tena?”
“Kwa kuweza kunitafuta nilijua ungenipotezea.”
“Hahaha! Sio kwa kirahisi kiasi hicho ujue wewe ni sawa na jirani yangu.”
“Hilo nalo neno.”
“Japo halipo kwenye kamusi.”
“Hahahaha! Kumbe unavituko hivi.”
“Ah! Mbona kawaida tu!.”
“Yani natamani nikuone maana si kwa machombezo yale unayoyaandika mmmh! Kweli wifi anafaidi jamani.”
“Wifi tena.”
“Ndiyo.”
“Kwani ulihudhuria kwenye harusi yangu?”
“Hapana.”
“Sasa mbona unanipa mke wa kufikirika?”
“Kwani huna mke?”
“Sina.”
“Ah! Basi mpenzi una mpenzi?”
“Ndiyo ninaye.”
“Anaitwa nani?”
“Chombezo.”
“Hahaha embu kuwa serious bhanaaa.”
“Kweli sasa nikudanganye ili iweje?”
“Inamaana huna mpenzi na umaarufu wote huo?”
“Umaarufu gani?”
“Wa uandishi.”
“Umaarufu na mapenzi ni vitu viwili tofauti kabisa naomba usivichanganye hata kidogo.”
“Kwahiyo huna mpenzi?”
“Ndiyo.”
“Nitaamini vipi?”
“Utaniamini tu!”
“Sawa.”
Nakumbuka nilichat nae muda mrefu sana, nilikuwa nikimchombeza mpaka alikuwa hataki kuacha kuchat, naweza kusema hatukuwa na kikomo katika kuwasiliana kwetu, tulichat sana tena sana tu, mahali tulipochoka tulihamia WhatsApp ambapo huko tuliweza kupigiana kupitia ‘Video Call’ na baada ya hapo tuliweza kutumiana picha mbalimbali.
Helena alikuwa ni msichana ambaye hakuwa na muonekana mzuri sana, alikuwa wakawaida tu! lakini alijaaliwa figa namba nane iliyozidi kumfanya kutamanika. Nilikuwa nimemtamani sana kupitia baadhi ya picha zake alizokuwa amenitumia hata hivyo alikuwa akiishi karibu kabisa na mahali nilipokuwa nikiishi hivyo sikutaka kuwa mwenye papara sana, niliufahamu uchawi wa mambo yale hivyo sikuwa na shaka hata kidogo, niliamini lazima angejileta mwenyewe kwani kwa muda mfupi tu! niliyofahamiana naye tayari alikuwa amejirahisisha kwa kiasi kikubwa.
YOU ARE READING
Nifanye Na Mimi Kaka Dick. Na Juma Hiza
RomanceKijana aliye fanikiwa kuwa hodari sana alijitoza katika anasa za dunia......