Nilirudi katika chumba changu huku nikiwa mwingi wa furaha, sikutaka kuamini kama nilikuwa nimefanikiwazifi kumnasa Precious katika mtego wangu. Nilijiona kuwa kidume haswaa! hasa kwa msichana mrembo nm yule kumnasa tena bila kutumia nguvu nyingi nikafanikiwa kufanya naye mapenzi. Hakika niliuona kuwa ushindi mkubwa sana. Niliwakumbuka wale wasichana niliyokuwa nawafatilia pale mtaani, kila siku walikuwa wakinipiga kalenda, walijiona kuwa wazuri kama uzuri aliyokuwa nao Kim Kardashian. Loh! Katika macho yangu ya harakaharaka niliwaona kuwa wabaya tu kuanzia sura mpaka yale mambo mengine, kwanza walikuwa wachafu. Kwa muda mfupi niliyokutana na Precious, sikutaka kuamini hata kidogo kama niliweza kumteka kiasi hicho. Nilikitazama kitanda changu mara mbilimbili huku nikiwa siamini kabisa kama dakika chache zilizopita Precious alikuwa amelala miguu juu huku mzee mzima nikijifaidia utamu wa vanila.
"Precious!" nilijisemea kisha nikatabasamu, tabasamu lililonirejesha katika tukio lile lililotokea pale kitandani.
Wakati nikiendelea kuukumbuka ule uchafu niliyoufanya na Precious mara macho yangu yakakutana na pochi ya precious kitandani. Nikakumbuka wakati ule alipokuwa akikurupuka kwa kuhofia kuchelewa kurudi nyumbani, bila shaka ndiyo muda huo ambapo aliisahau pochi yake. Haraka niliichukua na kuifungua, nilikutana na vitambulisho vyake, pamoja na passport. Nilifahamu kuwa vilikuwa ni vitu muhimu sana kwake hata hivyo sikutaka kuwaza sana ni kwa jinsi gani ningeweza kumpata kwani namba yake ya simu aliniachia hivyo sikupata wasiwasi wowote. Wazo la haraka lililonijia kwa wakati ule ni kuamua kumpigia simu na kumwambia kuwa alisahau pochi yake. Kabla sijakubaliana na wazo hilo la kumpigia simu, nilijiwa na wazo la kumtumia ujumbe mfupi na hata pale nilipoichukua simu yangu kwa lengo la kumtumia ujumbe mfupi nilisita. Nilihisi kukosa maneno ya kumwandikia kwani nilijikuta najiwa na maneno mengi kiasi kwamba nikawa sijui ni lipi nimtumie kwa wakati ule.
Akili ya haraka iliyonijia ni kumpigia simu yake. Naam! Hilo halikuwa tatizo hata kidogo kwani ni kitendo cha kumpigia simu na kumwambia kuwa alisahau pochi yake halafu basi huo ndiyo unakuwa mwisho wa mazungumzo.
Niliamua kumpigia simu, hapa nilikuwa nimeketi kwenye kochi nikisubiria simu yangu kupokelewa. Ajabu simu ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Ilikuwa ikiita mpaka ikafikia wakati kwa upande wa pili nikawa naisikia sauti ya mwanamke ikiniambia namba ninayoipiga haipokelewi.
Sikukata tamaa, niliamua kupiga tena lakini hakuna jibu lolote nililokuwa nimeambulia.
"Ina maana hataki usumbufu au?" nilijiuliza lakini kabla sijataka kutafakari jibu niliamua kupiga tena. Safari hii alikuwa akikata.
"Sasa unanikatia unajua nataka kukwambia nini?" nilijikuta nikiwa naiambia simu yangu kwa ghadhabu, sikupendezewa na kitendo kile hata kidogo.
Wakati nikiendelea kuwa katika hali ile mara akanitumia ujumbe mfupi, alikuwa akiniuliza kuwa mimi ni nani? na mimi bila hiyana nikaanza kuchat naye.
"Nani wewe?"
"Nani wewe?"
"Embu nijibu basi halafu samahani nipo na mume wangu na kuna ugomvi kati yetu hivyo usinipigie simu sawa utaniletea matatizo."
"Kwahiyo nishike lipi hapo?"
(Kimya) hakujibu lolote.
Mpaka kufikia hapo nilishaelewa nini kilichokuwa kinaendelea, Precious alikuwa ni mke wa mtu. Tukio la kuchelewa kurudi nyumbani bila shaka ndilo lilikuwa sababu kuu ya kutokea ugomvi kati yake na mume wake japo sikuwa nimepata picha halisi lakini kupitia mawazo yangu niliweza kuunda tukio zima lililokuwa limetokea wakati ule alipokuwa akirudi nyumbani.
Kichwani nilitengeneza tukio kuwa Precious alikuwa ndiyo ameshafika nyumbani kwake kisha anamkuta mume wake akiwa katika muonekano wa hasira.
"Umetoka wapi?" anauliza mume wake huku akimtazama Precious ambaye anaonekana kuwa katika muonekano wa uwoga.
"Ni....ni..ni....." anajibu Precious kwa kujiumauma kisha mume wake anafyatuka na kuja kumnasa kibao kikali ambacho kinamfanya aanze kulia kwa sauti huku akiomba msamaha.
"Nauliza umetoka wapi?"
"Nisamehe mume wangu nimechelewa foleni."
"Foleni?"
"Ndiyo mume wangu."
"Foleni gani hiyo na mbona kila siku unawahi kurudi kwanini leo uchelewe?" anauliza mume wake kisha anaanza kumpiga.
Nilimaliza kutengeneza tukio hilo kichwani mwangu kisha nikaanza kujiuliza maswali, ni kwa jinsi gani Precious alikuwa akimjibu mume wake. Kwa kweli sikutaka kushindwa kubaini lolote lile ambalo lilikuwa linaendana na ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea. Niliamua kukitumia kipaji changu cha uandishi kuanza kuunda matukio mengi mengi kisha nikaanza kuyafanyia kazi.
Akili yangu ikanituma nimpigie simu Precious kwa wakati ule japo hapo mwanzo alinitumia ujumbe mfupi na kuniambia kuwa nisimpigie simu kwani alikuwa katika mgogoro na mwanaume ambaye alidai kuwa ni mume wake. Niliamu kupiga simu na haikuchukua muda iliwezakupokelewa.
"Wewe ni nani unayempigia mke wangu usiku huu?" iliuliza sauti nzito ya kiume upande wa pili, nilifahamu kuwa alikuwa ni mume wake Precious, sikuwa na hofu hata kidogo nikatabasamu huku kichwani nikimuandalia jibu takatifu ambalo bila shaka lilikuwa linakwenda kummaliza.
"Mimi," nilimjibu kwa kujiamini.
"Nakuuliza wewe ni nani unayepiga simu ya mke wangu usiku?"
"Mimi ni mwizi."
"Mwizi?"
"Ndiyo mimi ni mwizi ambaye nimemuibia mkeo pochi yake lakini nimeona sio vizuri kwa nilichokifanya hivyo nataka nimrudishie," nilimwambia maneno ambayo kwa kweli nilijitungia tu! akilini lakini nilishangazwa na kile ambacho alinijibu yule mwanaume. Aliniamini kuwa mimi ni mwizi kweli na aliniambia anajuta kwa kumpiga mke wake kwani alihisi anamdanganya kuwa alikuwa ameibiwa. Nilijihisi kucheka lakini kimoyomoyo nilijikaza, nikakata simu kwa makusudi ili nizidi kumuweka katika wakati wa maswali. Nilifahamu fika ni lazima angeweza kunitafuta kwani pochi ilikuwa na vitu muhimu sana. Naam! Ilikuwa kama nilivyokuwa nawaza na ni hapa ambapo nilizidi kuuonyoesha udick wangu katika kucheza mchezo ambao baadae ulizidi kumfanya Precious anione kuwa 'genious' mtu Fulani hivi ambaye nilikuwa na akili nyingi ambaye aliniganda kama ruba.Tafadhali acha Maoni yako au upigie kura
YOU ARE READING
Nifanye Na Mimi Kaka Dick. Na Juma Hiza
RomanceKijana aliye fanikiwa kuwa hodari sana alijitoza katika anasa za dunia......