Kiserema

103 5 0
                                    

Jua lililokua likielekea machweo lilipenyeza kwenye kuta za chumba cha Mzee Maweo ambaye alikua amejilaza kitandani akingoja kufa.Kando yake palisimama watu watatu wanaume waliokuwa wanalandana kwa kimo ila mmoja wao alikua mweusi mnene mwenye tumbo lililoonekana kuguza kitanda cha mlalahoi huyu

Kwa umbali Lulu ambaye ndiye msichana wa kipekee wa Mzee Maweo alionekana akijongelea chumbani.Alibeba sinia iliyojaa dawa chakula na vinywaji aina ya Tusker Cider hawakua wachochole kiasi cha kutosherehekea na kileo hicho maarufu.Alipoingia chumbani mzee alimwita akamnongonezea sikioni.

Lulu mwanamke aliyeumbwa siku ya saba alikua mhandisi wa kampuni moja ya ujenzi ila babake alikataa kabisa kukubali amjengee chumba.Pesa hazikua shida kwake ila alikua na roho nyepesi ya kupenda iliyomfanya kuumizwa sana na wanaume wengi.

Macho yake yaling'ara akinielekea kama aliyekua na jambo la ajabu au furaha.Alikitegua kiuno chake kwa mwendo wa twiga akinikaribia.Mimi na ndugu yangu Mosi hatukuwa wa familia ya Maweo.Tuliishi kuambiwa wazazi wetu walisafiri watarudi siku moja.Wazazi wetu hawakufariki ila hakuna anayewakumbuka na hamna hata picha moja iliyowahi kuonyeshwa kwetu ili tuwajue.

Kwangu kwa Mzee Maweo ndipo nilipaita nyumbani na kwa ukarimu wake aliweza kuniskuma nisome hadi kidato cha sita.Ndugu yangu Mosi alikua ashamaliza Uanadiplomasia kutoka chuo kikuu cha Msafara na alikua akihangaika mjini akitafuta kazi.

Lulu alinikaribia akatabasamu,Huyu mtoto alikua na midomo ambayo ilishabahiana sana na ya Mamake Bi Sukari Kero.Mamake aliishi mbali na nyumbani baada ya baba yangu ambaye alikua mwanawe wa kwanza aliokuja naye kwenye ndoa ya Maweo kupotelea hewani asitambulike aliko na hapakufanywa hata mazishi ya kuzika mgomba.Aliponiangalia machoni ile nyota iliyong'aa machoni pake ikapotea akanipa ujumbe kwamba nlikua nkiitwa na Babu yangu Mzee Maweo.

Nlitembea haraka nkiruka maua na mawe yaliyokua yameangikwa kuitenga njia na bustani ya babu iliyokuwa imetunzwa na kuchanua miwaridi miekundu na mieupe.
Aliponiona nimefika chumbani aliagiza Ponde Ziwa na Mto waondoke ili aninong'onezee.Waliheshimu na kutoka.Aliniambia nipige magoti na baada ya kuniombea (Mzee Maweo alikua mcha mungu na mshiriki wa kanisa kuu la katholiki)Alianza kuongea kwa lugha tata ambayo nlichukua muda kuishika.Na baada ya kumaliza wosia wake babu alichukua kitabu chekundu na kukikunja vyema kisha akaniambia nikitunze kitabu hicho ni muhimu sana kwangu.
Alipomaliza alimwita lulu kisha akamwambia."Hekima amekaribia umri tosha wa kuoa.Najua itakushangaza lakini nataka siku ikifika muoane kwenye harusi kubwa." "Lakini baba huyu ni mwanangu siwezi olewa na yeye."Ndipo mzee alipofunguka na kuufichua ukweli kuhusu mimi na ndugu yangu.Ukweli ambao siwezi kukutajia bila idhini ya wahariri.Alipomaliza akatutemea mate kisha akajilaza vyema Akafa.

Ipo Siku Where stories live. Discover now