Mzee alipoaga kila mtu alirejea kazini mwake mimi nikashika langu zizini.Wanakijiji wakapungua na mwishowe wakaacha kutupa Makiwa.Kila mja alionekana kunihurumia kichinichini ila hakuna aliyekuwa na ushupavu na ari ya kuniambia hali halisi ya maneno.
Nlienda chumbani mwangu usiku mmoja nikapata chumba kimekorogeka vitu vimerushwa kila mahali hakukaliki.Sikujua kabisa maana ya kilichotendeka na hamna aliyekua tayari kunipa maelezo nijue kilichokua kinatafutwa kwenye msako huo.
Asiye na mwana kawaida hueleka jiwe.Miye sikuwa na wazazi na wale walonilea walishaaga sasa ilibidi niwache kazi ya kulisha mifugo wa marehemu na kuenda zangu.Nliishika njia ya Mathlai na kulipita Kasri la Binti Sultani ila sikuwaimwona kwa uso lakini alikua akisifiwa sana baina ya wanakijiji.Siku hii ilikua ya bahati sana maana nliposonga mbele nlikutana na kundi lake la wapiga debe.Waliniskuma wakaniangusha mtaroni.Na magari yao ya farasi yakaendelea mwendo.
Akakuja Nyuma farasi mmoja mweupe amembeba mwanamke mrefu aliyebeba upanga.Aliponikaribia akapiga nduru kisha akasimamisha farasi lake akapiga firimbi akashuka akanielekea.Singeweza kuuvumilia urembo wake.Alikua na maziwa yaliyojijaza na chuchu zake kujichora vyema kifuani.Meno meupe kama mla theluji na uso mpana uliojaa tabasamu ya uzazi.Roho yangu haingekataa kugonga mbio.Ulikua urembo uliokamilika.
Kijana waendapi na watokapi? aliniuliza.Naenda mjini wazazi wangu walezi wameaga dunia na sasa inabidi nitafute riziki.Nlimjibu.Aliniangalia kwa kina akayaangalia majeraha yangu kisha akachangamka.Kijana utanifuata uishi kwangu nitakutunza hadi upone ndipo uondoke uende kutafuta riziki yako mimi ni Binti Mathlai Shemz.
Hima hima nikaandamana naye hadi kwake chumbani ambapo nlikutana na vijana wawili wenye umri wa makamu tu wakiwa wametulia wakiitumbulia runinga macho.Hawa ni waume zangu alisema binti Mathlai Shemz.Hawa ndio ninao watafutia riziki na ukiwa mmoja wa hii familia utawaamkua mjuane na uanze kujifunza kifaransa.
YOU ARE READING
Ipo Siku
HumorWosia wa babu yangu ukitimia naapa nitakua mtu asiye na kiburi.Naapa kutimiza yote aliyoninongonezea na ninaapa kuitunza aila yangu bila kiburi wala dharau. Maana natumai IPO SIKU.