Penzi

30 3 0
                                    

Joto la mwezi wa sita lilikua limeanza huku kila mlalaheri akijiskia kwa kunywa sharubati zilizotiwa kwenye jokovu na walalahoi kununa maana hawakua na lolote la kuwapoza koo.
Mimi sikua na langu hivyo sikua na daraja lolote.sikua mlalahoi sikua mlalaheri,nlikua nipo tu.Nliamua kuteremka toka majalalani nlipokua nmeyaweka makao nikafululiza hadi kwa chumba nlichokua nimekitazamia kwa muda nkiwa na tumaini kuwa hapo ningesaidika.
Ndipo nlikutana na yeye.Mwanamke mwenye ngozi ya rangi ya maji ya kunde na macho yanayopendeza kwa mvuto wa aina yake.uso laini na kiuno kilichoambatana sawa na rinda alilovaa.Hadi leo sitambui vipi nliweza kumwongelesha ila kwa kweli aliumbwa akaumbika.Chuchu za maziwa yake zilisimama tisti kuonyesha gari lenyewe injini bado haikua imeenda maili kadhaa.
Aliniamkua kunigutusha kutoka kwenye lepe la mawazo ya njaa.Vipi kaka waelekea wapi?mbona wakaa kuwa na mawazo hadi dereva wengine karibu wakubonde.Aisee picha kama hili nliliona kwenye sinema tu na zipo sinema ambazo bado hazikua na wanawake wenye urembo huu.
Nlimwangalia machoni na kumwambia la hasha dada mimi ni mpita njia tu.sina mawazo ila nipo kwenye ulingo usiokuwa na refa na mpira.Alitabasamu kisha akamiambia pita upande huu mwingine nkufungulie nataka sana tuwe marafiki tuongee tuondoe tashwishi ndipo utanipa ukweli wako.
Nlikubali na kujirusha kwenye kiti cha upande wa kushoto.Gari lenyewe lililua safi sana hata kuwepo kwangu kule kulileta uchafu.Nlimkumbuka mwandishi wa novela ambayo nliipenda sana son of a beggar. Nlikumbuka jinsi msimulizi alivyojikuta amebarikiwa na mpenzi nikatabasamu ila huyu hakuwa mpenzi alikua tu raia mwema aliyeninusuru toka jua kali kwa kunibeba kwenye gari lake hili

Ipo Siku Where stories live. Discover now