Majini

25 3 1
                                    

Bila habari ya kilichoningoja nlikodi chumba kimoja karibu na mpiga ramli aliyeaminiwa na wakaazi sikujua kuwa chumba hicho kilikuwa kilinge cha washirikina wenzake.

Nlipomaliza kutandika mkeka wangu sakafuni tayari kujipa nafasi ya kupumzika mlango ulibishwa na akaingia mtu akasimama nyuma yangu kama aliyekuwa na neno fiche lenye uzito.Nliinua kichwa na kumtazama ili nijue nani alieyejaa ujasiri kiasi cha kukuja chumbani mwangu na kusimama nyuma yangu bila hata salamu.

Alikuwa mzee mrefu asili yake kama ya kiarabu ila rangi ya ngozi na nywele zake za kipilipili idhihirisha wazi kuwa alikuwa wa asili ya kidigo.Macho yake yalikolea ukijani kibichi kama zeruzeru na yalionekana kujaa kisirani." Shikamoo mzee habari ya leo?"nlimwamkua. Baada ya kunijibu alinipiga pambaja kama anayenisifia na kusema " tahadhari sana na mji huu umejaa washirikina majini na mazingaombwe yasiyo kifani" aliposema maneno haya aliondoka bila kwaheri na kutokomea kama mvuke nsijue kaelekea kusini au kaskazini.

'Hivi,yule alikuwa nani maana hakujitambulisha na mbona kabeba ujumbe mzito hivyo kwa mtu asiyemfahamu? Mbona hakuniruhusu tufahamiane?'haidhuru nlijilaza chali na kuamua ningeshinda bila kulala maana onyo kama lile halikuwa la kuchezea.

Ilipokaribia saa sita usingizi ulinilemea nikaamua kuiba dakika tano za ubwabwa.Nlipofunga tu macho yangu. Nliskia sauti kamanza watu wanacheza densi  huku wakicheza vinubi vinanda tarumbeta na kuimba kwa sauti za kuongoaongoa.Mziki wenyewe ulikuwa wa asili ya kiLinlin na nliufahamu sana maana babu wakati ule alizoea kuniliwaza nao alipotaka kunipa maneno yake yenye busara.

Mara mlango ulifunguliwa ghafla nami nikafungua macho nipate nafasi ya kumwona mgeni wangu huyu asiyejali saa na majira. Mlangoni alisimama kisura mmoja mweupe mwenye macho yaliouangaza urembo wake ulipitiliza na kuonyesha mahaba yaliyojaa moyoni mwake. Mkononi alibeba tarumbeta iliyometameta kwa miale ya mwezi mkuu.

"We kaka hivi nkuulize?huskii mziki wetu ulivyo mtamu? Jiunge nasi tucheze na twaweza cheza mziki wowote hata isukuti kama ndio chaguo lako." Nlijaribu kufungua kinywa nisipate cha kusema. Mwanamke huyu kajaliwa sauti. Hakuwa bobokaya la kujishaua na kupiga kifua. Alikuwa mwanamke mmoja kati ya wote warembo uwajuwao wewe.

Aliingia ndani akafunga mlango na kusimama pale kando ya mkeka nlioufanya kitanda."Kama umeamua utalala basi nami nitalala hukuhuku ili nikuimbie humuhumu" Makataa yangu yalianguka kwenye skio la kufa. Sikuhitaji mwanamke usiku huu maana Mwembe Tayari kulikua na joto jingi sana na kuongeza na hayo nlikua bado nauguza jeraha la kuchezewa na mtu nliyemwamini kama mpenzi wangu.

Tarumbeta ilimponyoka na kuanguka sakafuni kando yangu. Aliniangalia akatabasamu kisha akaanza kuzidondosha nguo zake. Alipotoa rinda lake refu leupe pe! Sikuweza kustahimili urembo nliouona. Chuchu zake zilisimama kifuani tisti kama makinda wa nyuni asiyejali kupinda kwa mti. Ngozi yake nyeupe nyororo ilinipa hisia za kibogoyo aliyetunukiwa meno.

Alijilaza kando yangu na ngoma ikaanza. Hii haikua ngoma ulioizoea. Ilikua ngoma mpya bikira gari lenyewe bado mpya viti na magurudumu yote hayajakanyaga matope wala injini ya gari hili haikuwa imewagi kubadilishwa oili.lazima ningemtia adabu kisura huyu aliyejinasa kwenye ulimbo wa msonobari asijue una chachu

Tulipomaliza kipindi cha tatu alinyanyuka akavalia kisha akanisihi nisiondoke mjini maana angekuja kunitembelea kila mara wakiwa na ngoma. " Waweza kuniita Mariamu ila si bikira maana ushaninyanganya uteuzi huo" nlipotaka kumjibu binti alikua keshaondoka na mlangu ukajifunga nyuma yake.

Singeweza kulala na jasho lililonitiririka wakati wa soka ile. Nlijitoma msalani kujirashia maji.Nliporudi sikuyaamini macho yangu. Mlango wa chumba changu ulikua umefungwa na kufuli kubwa kuliko taabu zangu na aliyefunga simjui. Nlidhani nimepotea lakini ishara zote zilionyesha ni kwangu.

"Kaka kazi ulioteuliwa kufanya ulimwenguni imekamilika.Tendo ulilofanya la kulala na mwanamke ule wa kizingaombwe ni la kuhuzunisha sana maana iwapo atashika mimba malkia yule wa kiushirikina mtoto atakayezaliwa atakuwa mkandamizaji wa pote peponi na duniani maana ana nguvu na asili mbili. Nlikuonya mchana ila ukayapuuzia mambo yangu. Sasa utagharamia ujeuri wako huo kwa kulea kiumbe hicho kitakacho zaliwa maana Malkia wa peponi huwa hanyonyeshi na wala hashughulikii damu yake hadi ifikapo miaka mitatu ambapo atamkaribisha mwanake kwenye himaya yake ili awe mrithi."

Alinyamaza nikajua ametoweka vile alivyokuja na papo hapo mlango wangu ukafunguka wenyewe kama ambao hukuwa na chochote kilichoubana. Nlihapa kutoingia chumbani kule na hivyo nikangoja machweo pale langoni. Mwezi ulipopishana na jua nliondoka Mwembe Tayari nikiapa kutorudi na kuelekea Unguja

Ipo Siku Where stories live. Discover now