Kuibiwa

44 5 0
                                    

Joka lenye urefu wa futi sita na upana wa inchi kama nne lilijikwangura mbele yangu kama wafanyavyo paka wa kijijini wamwonapo mwenye nyumba kaleta kitoweo cha nyama.Joka jeusi lenye macho ya kuchina china na kichwa kipana kama kiganja cha Abunuwasi.

Nlishindwa kupumua kutokana na uoga ulionikumba ghafla.Nliinua mkono kuchukua ufito uliokuwapo sakafuni ili nilifukuze joka hili ila lilishinda likinisogelea.Nlitaka kupiga ukwenzi mkali ila mdomo wangu ulizibika na kufungwa kama uliotiwa gundi ya kushonea viatu.

Nikaanza kusikia nasaha ya guru wa kiswahili Ustadh Wallah bin Wallah kwenye maskio yangu.Hapo nikajua mwisho wangu umefika.Nikakumbuka marehemu babu yangu akisema usiogope jitu lolote maana majitu mengine yana miili mikubwa kuliko fikra na akili zao.

Nikasimama tisti bila kutingisika nikachukua mkoba wangu nliokua nimejitengezea kutoka kwa ngozi ya ngombe aliyechinjwa wakati wa sherehe za tohara yangu nkiwa umri wa miaka karibu nane hivi.Nikaushika vema kisha nikaufululiza kichwani mwa joka hili mara tatu bila kusimama kujipa muda wa kupumua.

Joka liligaragara kisha likaegeuka na baada ya kuinua kichwa chake juu kabisa likakiangusha kichwa chake na kutulia tuli.Bila wasiwasi nikaokota kiboko chenye urefu usiozidi futi tatu nikalipinduapindua na ...........Niligutuka nlikokua nimelala.Ilikua jinamizi kumbe.Ilikua ndoto iliyonipa wasiwasi kwa muda. Nlipoamua kujipanguza umande uliokuwa umeniganda kutokana na kulala nyasini kwa usiku wote,nligundua sikua na viatu na mkoba wangu pia ulikua umenyakuliwa bila mimi kujua ni nani na mbona.

Kwenye mkoba ule kulikua na kile kitabu chekundu nlichopewa na Babu yangu na mbali na hicho vyeti vyangu vya kuhitimu na vitambulisho vyote vilikuwamo mkobani.Nisemeje.Kuna nini kinachoendelea nifanyeje?nitaambia nini ulimwengu?

Kuketi chini na kulia hakungesuluhisha jambo lolote niliamua kujiendea zangu safarini nijifiche mjini labda nitaweza kupata msamaria anisaidie kuviunda vyeti vyangu upya .Nlipiga miayo kutokana na njaa na pia kukata tamaa ila nlijipa moyo na kuendelea kutembea kuelekea mjini nisiko kujua

Siku ya nyani kufa aghalabu miti yote huteleza.Nliposonga hatua chache toka nlipokua nkizubaa mbeleni nlikutana na jambo linalozifanya nywele zangu za kisogo kusimama tisti hadi wa leo.Joka lenye urefu wa futi saba na upana wa inchi karibu kumi alikua anajivuruta na kuinua kichwa akinielekea......Kilichofuata sikijui hadi leo hii.Nlipojikuta kwenye hali yangu nlikua hosipitali iliyojaa vitanda vyenye malazi meupe.Sikuweza kukumbuka chochote hadi nlipoelezewa kuwa nlikutwa porini nkiwa nakabiliwa na chatu ndipo wasamaria wema wakanileta huku

Ipo Siku Where stories live. Discover now