Maamuzi

18 3 0
                                    

Tuliingia kwenye hoteli moja la kifahari kisha madam akaitisha menu.watu wote waliokuwa humo walikuwa nadhifu na wenye vyeo vyao.walionekana kuwa wenye raha na tabasamu.

Nlikuwa nimeanza kuzubaa kabla ya kurudishwa ulimwenguni na mrembo huyu aliyenileta.'utakula nini kaka?' Nlimwambia kisha nikarudi kwenye ulimwengu wa ruiya uliojaa ulimbwende wa aina yake.

Baada ya kinywaji aliagiza chakula ambayo nliibugia kwa pupa.Nlipomaliza alianza kunisaili nami sikuwa na budi ila kumjibu bila kuficha.Mrembo huyu alitoa miwani yake ya jua ambayo wakati wote huu aliificha kwenye begi lake.Aliivaa kisha akaniambia nimepata mwokozi.

Nlitabasamu kisha nikamwambia mimi nlikua nimetosheka na kuwa kijana wa mitaani na sikuwa na hamu ya kuwa mlimwengu tena.Alianza kulia ghafla kisha akasimama.Sikuwa na jingine nlianza kujawa na mawazo nliporudi ulimwenguni nlikuwa pekeyangu.Nlitoka polepole na kuelekea majalaani nlipojitupa na kulala bila kufikiria chochote.

Siku iliyofuata alikuja tena yule binti.Nlijaribu kumkanya ila hakukuwa na jingine alikataa katakata kuniskiza na ikabidi nimfuate.Tulikwenda kwenye mkahawa mwingine na huku kulikuwa na watu wachache na wote walionekana kutokuwa na furaha.

Alifululiza hadi kwa mhudumu na kumwongelesha kwa muda kisha akarudi kwangu na kunielekeza kwa kiti kilichokuwa mbali na wanunuzi wengine.Muuzaji alikuja na vinywaji vyetu kisha akaondoka.Yule binti akatabasamu kisha akanielekeza macho yake yaliyoregea kwa njia ya mapenzi.Mbona wahuzunika ilhali nina pesa ya kutosha kutupa furaha maishani?,

Nlijifanya kutosikia ila hakujirudia alitabasamu kisha akanibusu! Nlifunga macho ghafla na kuendelea kuunyonya ulimi wake uliojaa asali nikamsogelea kabisa kisha tukawa tumekumbatiana. Akafurahi kabisa nami nikajawa na hamu ya kuendelea kumwamilia na kumpa raha aliyohitaji.

Ipo Siku Where stories live. Discover now