Usalama Bandia

4 2 0
                                    

Nlirejea na bi Agnes nyumbani kwake na kuona mabadiliko tele. Chupa za pombe na vileo vingine vilitapakaa kote. Hapakuwa na alama yoyote ya chakula kumaanisha alikua tu anabugia pombe na kubonda mali bila ya haja ya kuishi tena. Nlimhurumia sana ila sikua na cha kusema isipokuwa kumwomba radhi na kuapa kurekebika.

Tulianza usafi na baadaye tukaenda duka kuu kununua vyakula na matunda. Agnes alikuwa amejawa na furaha tele na kila walokutana naye alikuwa na mtazamo mpya wa bi huyu aliyekuwa kajiachilia. Tulirejea nyumbani usiku mkuu na kuandaa chajio ama tuseme kiamsha kinywa na kujitupa kitandani.

Nliogopa kumgusa maana nlikuwa nimekawia kabla nionane naye,usiku huo tulilala tu kama kaka na dada mtu. Asubuhi ilipowadia alinisihi niandamane naye kumwona rafiki yake mcheza sinema aitwaye Rose. Kwa binti huyu hapakuwa mbali ila aliheshimu sana watu wanaoendesha magari kwa hivyo ilibidi tutumie Volks wagon jipya alilokuwa ameninunulia kile kipindi nikiwa bado napambanya na kujaribu kunionyesha penzi.

Rose alikuwa mwanamke mwenye kiuno cha nyigu na mapaja yaliyojaa tele na matuta ya kutamanika. Uso wake mweupe ulionyesha ishara za kukomaa kumaanisha kweli wauza mafuta walikuwa wamefanya kazi ya kumremba mwanamke huyu. Alitukaribisha kwake na baada ya salamu akaingia jikoni na kumpa kijakazi amri ya kuanza mapishi. Sikupenda kula sana ila chakula alichokiandaa mpishi yule kilikua na haiba na mvuto wa aina yake.

Tulipomaliza kula ndipo mazungumzo yakang'oa nanga. Kila wakati Agnes alinitambulisha kwa huyu mwanamke kama rafiki yake tu na hatukuwa na uhusiano wowote wa ziada. Jambo hili lilinitia wasiwasi na kunikumbusha nijikaze nijitoe kwenye ulimbo huu ulioninasa na kunipa usalama bandia.

Baada ya muda mfupi wa mazungumzo kisura huyu alikubali kunipa ajira kwenye kampuni ya babake ya kununua na kuuza magari yaliyokuwa yanaagizwa kutoka ngambo. Alinishauri niwe mwepesi wakuelewa na nisichelewe kazini na kila nipatapo shida nimwambie Agnes.

Yote hayo yalikuwa kama muujiza kwangu. Yaani ukiwa na hela hauhitaji karatasi vyeti wala barua zozote,kupata kazi. Nlimshukuru sana naye akaonekana kuwa kafurahia uamuzi wake. Laiti ningalijua yalokuwa yananingoja...

Nlifika kazini Jay and family motors jumatatu saa moja asubuhi na kuwahi ofisini mwangu. Kwa kuwa sikuwa nimehitimu nlihitaji sana usaidizi wa tarishi na karani. Wote hao walikuwepo ila walikuwa na mengi ya kushughulikia hivyo hawakuwa na haja na mgeni aliyeletwa kama mkubwa wao asiyejua la kufanya. Kazi ilishika moto baada ya wiki moja nami nikawa nimejifunza kutumia tarakilishi kuyanunua magari na kupanga ratiba za kazi. Haikuwa rahisi ila kwa usaidizi wa mpenzi wangu nlifaulu.

Mwisho wa mwezi ulipowadia nlistaajabu jinsi malipo yalivyofanywa. Hakuna aliyelipwa mkononi hivyo nlilazimika kutumia ujuzi wangu kufungua akaunti ya benki. Sikuwa na kitambulisho ila kwa cheo changu kile,hapakuwa na haja yake. Nlilipwa nusu milioni kama mshahara wa kuanzia na marupurupu mengi ya kujikimu na bima za afya. Nlipomwambia mke wangu alifurahi na kunitia moyo niendelee kutia bidii maana wenye kampuni wakifurahishwa na kazi yangu wangenipa cheo kikubwa zaidi na gari langu la kifahari niwe nawahi kazi bila matatizo yoyote.

Wiki zikawa miezi na miezi ikaelekea kuwa mwaka, ndipo masaibu yangu yakaanza. Rose alinitembelea ofisini kama ilivyo desturi yake kila siku, ila siku hii,alikuja na ombi lililonitisha na kunifanya nikose cha kusema. "Nimekuwa nikikufuatilia sana na imetukia kwamba,Nakupenda. Sina ubaya wowote ila itabidi unikubalie niwe mpenzi wako halali. Najua waishi na dadangu Agnes ila hilo si tatizo. Nitakusaidia kujipanga tutoroke.

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Nov 19, 2020 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

Ipo Siku Where stories live. Discover now