Mabadiliko yasiyo kifani

7 0 0
                                    

Jua la adhuhuri lililokuwa na miale mikali lilichoma kipaji cha uso wangu , walonitazama walidhani nlikua nayeyuka kwa jinsi kijasho kilivyonitiririka.

Sikua na mahali maalum nlikokua naelekea. Unguja sikupajua vyema ila nliwai kusikia redioni na magazetini kuwa ni patulivu sana na kulijaa watu wenye utu na ukarimu. Hili lilinitia moyo na kunifanya nikaze mwendo bila kujali ama kuogopa kungeharibika neno.

Nlipokaribia kijijini humo nliona chumba kimoja kilichokua kinang'ara kutokana na weupe wa chokaa iliyokua imepakwa kuta zake. Watu walionekana kuingia na kutoka chumbani humo kitu kilichonifanya kufikiria huo ulikua msikiti. Sikujali nlikaza mwendo kuuelekea.

Mlangoni palisimama wanaume wenye sura ngumu na ndevu zilizopakwa halua. Walionekana wenye bashasha na sare zao za kaki ziliwafanya kuonekana kama askari polisi ila rungu walizobeba zikakanusha fikra zangu. Nliwakaribia na kuwauliza "Je mwaweza kunielekeza kwa mkubwa wa kijiji hiki?"

Hawakunijibu, waliangaliana na kupasua kicheko kama radi. Nlizubaa nikakosa cha kusema maana nlikua mgeni pande zile. "Kijana hapa ni kwa chifu,kuonana naye ni hatia maana wewe si mkaazi wa huku" alisema mmoja wao.

Utulivu na ukarimu nliokuwa nausikia redioni, uko wapi?mbona walinda lango hawa wawe na roho chafu namna hii? Haidhuru nliondoka pale bila kuwaambia lolote na kuelekea kusini. Matumaini yote yalikua yamedidimia.

Mwanamke mmoja alinitazama usoni kisha akatoka mbio kuelekea nlipokua ninatoka. Hakuwa mrembo wala hakuwa mkongwe alikua tu mwanamke asiyekua na chochote ambacho kingemvutia mwanaume haswa nyinyi wa minisketi herini na lipstick uso wake hukuwa na tabasamu wala macho yake hayakuwa na mvuto wowote.

Nlikosa kuelewa kilichomfanya atoke mbio kiasi kile. Nlichanganyikiwa nsijue la kufanya. Baada ya hatua chache palitokea ngurumo nlizokua nimezizoea, ngurumo zilizoukumbusha moyo wangu mapenzi, ngurumo za gari zito likipambana na changarawe.

Kabla nipate muda wa kugeuka gari lile liliegezwa kando yangu. Nlipolitazama, nlihisi kutoka mbio. Lilikua gari la Halua, mwanamke aliyetumwa toka mbinguni kutetea kulea kutunza na kuokoa nafsi yangu dhaifu. Nilijikuta nimesimama na kungoja dereva anikabili.

"Hivi mpenzi, mbona ulinitoroka. Mbona umefanya nikapitia shida kiasi hiki,umenitesa nikapitia wakati mgumu kukutafuta. Nyumbani ulikosa nini kilichokufanya uhepe muda wote huu?" Sikua na muda wa kumjibu. Alinifungulia mlango wa Benz lake na kuniagiza niruke ndani bila kusema chochote.

Nlijikuta narukia kiti cha dereva mwenza bila kufikiria mara mbili. Mpenzi wangu alikua amenitafuta nusu ya nchi na hatimaye kanipata. Njiani kimya kilijiri na hakuna aliyetaka kusema na mwingine. Tulipofika Makongeni aliegeza akaniamuru nsitoroke na akaelekea mkahawani.

Alirudi na chakula kilichopakiwa nami njaa iliyokua imenikaba haikunipa ruhusa ya kungoja nikaribishwe. Nlimeza bila kutafuna, chipsi na kuku iliyopitishwa kwenye tanuri la moto mwepesi na kuokwa kwenye chili kali ya kimakonde. Nlipomwangalia usoni nlikuta machozi yanamtiririka. Nliamua kupasua na kuvunja kimya kimya kabla kiwe kishindo.

''mpenzi wakati wangu wa kuwa nawe ulikamilika,nlitaka sana nami niwe mwanaume halisi.Sikutaka kuwa gumegume linalowekwa na mwanamke." Wakati nkiyasema haya,nliukumbuka wimbo nliouenzi sana wa msanii mmoja wa kibongo aitwaye Beka Flavor. Wimbo huo nliukariri kila neno baada ya jingine. Unaitwa kibenten.

Alinitazama usoni kisha akapanguza machozi na kusema"nafurahi bado wanitambua kama mpenzi wako, hivyo utarudi nyumbani kisha tutapanga jinsi utakavyopata ajira kwenye kampuni moja lisilo la humu nchini kisha utanioa kwemye harusi ya kizungu (white wedding)

Ipo Siku Where stories live. Discover now