Nlisononeka sana hosipitalini baada ya kupona na kukosa mdhamini wa kuzilipia ada zangu na pia kukosa kitambulisho kuliwapa madaktari na wauguzi woga ambao uliwafanya kunitenga kabisa na wagonjwa wengine.
Nlianza kujirudi kwa kutoroka nyumbani mwa binti Mathlai Shems.Nikashindwa kipi kilichonifanya njilete kwenye hali ambayo hata watu wenye taabu na mahangaiko mengi kuzidi yangu hawawezi jileta.ila nikamkumbuka Mola.
Nikakumbuka imam wetu akisema kwenye shida au raha mkumbuke mwenyezi mungu tu.Nliamua kumpea nafsi na moyo avitwae vyote.Kila nlipoomba nlijipa tumaini kwamba patakuja mtu anitambue anisaidie.ila siku zilivyozidi kusonga ndipo nlianza kukata tamaa na kuamua kutoroka hosipitali humo.
Nlingoja hadi saa kumi jioni wakati ambapo wauguzi walibadilishwa na kuingia wapya wa zamu ya usiku.Nikavaa shuka nyeupe iliyokuwa malazi yangu kwa muda huo wote na kujipiga kilemba nikawa kama mtu aelekeaye kuswali msikitini.Nikaelekea upande wa chooni na kisha kutokomea kwenye umati uliokuwa umezingira mgonjwa aliyekuwa anapelekwa hosipitali nyingine ya hadhi ya juu ambayo nlisikia wakiita referral hospital hapo ndipo nlipojitoa pole pole na huo umati na kuingia barabarani ambapo nlifuata kijia cha kichochoro na kujikuta mbele ya jumba moja refu jeupe.
Mimi nlidhani nimefika ikulu ya mtukufu Mbunge ila haikua hivyo lilikua tu jumba la burudani.Nliingia humo na baada ya kuona nimepotea nlitoka mbio tena na kufululiza hadi panakotupwa majalala na mabaki ya chakula.Hapa nlipaona pakinifaa maana hapakua na mwenyewe na wote wapita njia walijishughulisha sana na mambo yao.
Nlitandika ile shuka na kupiga lepe la usingizi kama mtu aliyefika kwenye wafu na kuruhusiwa kuwasalimia.Nlipoamka taa yenye mwangaza mkali ilinimulika usoni.Nlidhani ni gari ila haikua gari ilikua tochi ya askari washika doria.walipoona nikinyanyuka walirudi wote nyuma na hakuna aliye zungumza.walitoka mbio na hadi leo sitambui kilichowafanya kutoka mbio njia hio na walikua na silaha
YOU ARE READING
Ipo Siku
HumorWosia wa babu yangu ukitimia naapa nitakua mtu asiye na kiburi.Naapa kutimiza yote aliyoninongonezea na ninaapa kuitunza aila yangu bila kiburi wala dharau. Maana natumai IPO SIKU.