Wapo wengi waliotamani sana wawe kama mimi.Hakuna aliyekua akitaka kuniuliza nlikotoka nami sikuwa na jibu la swali hili maana hali yangu ilikua nyingine.Sikua mlalahoi tena nlikula kwa kheri na matarajio yangu tu sikujiskuma kupata mlo kama nlivyokua nkijiskuma mbeleni
Watu wengi waliniita chokoraa anayeng'aa ila mimi nliishi na nia ya kuwaonyesha watoto wa mitaani na mayatima pia ni binadamu na wanaweza kutimiza ndoto zao kimaisha.Nlikua kinara mkuu kwenye kampuni moja maarufu ya uundaji filamu ya Smartcard Pictures.Wadhfa huu sikuununua popote wala kuugombea nliupewa tu kwa mapenzi ya mwenyezi mungu tu.Gari langu aina ya Range Rover sport jeusi kama jifya ila lilingaa gizani kukumbusha gharama na hadhi ya mwenyewe kimaisha.
Kasri langu lenye vyumba mia mbili na madirisha ya migodi na dhahabu lilisimama pembeni mwa uwanja nlioishi kuutamani tangu nikiwa mtoto na kuwaona watu wenye hadhi jinsi walivyoishi maisha yenye raha.......Jua lilikua limeshachomoza na watu nsiojua waendako walikua wakiharakishw mbele yangu nlipotoka ndotoni na kukosa mali haya yote nliyokua nkiyavinjari ulimwengu wa ndoto.ila nlijiambia moyoni hii ni ndoto isiyofutika heri nife nipotee ila ndoto yangu isifutike
YOU ARE READING
Ipo Siku
HumorWosia wa babu yangu ukitimia naapa nitakua mtu asiye na kiburi.Naapa kutimiza yote aliyoninongonezea na ninaapa kuitunza aila yangu bila kiburi wala dharau. Maana natumai IPO SIKU.