Ponda Mali

48 4 0
                                    

Vijana wale wawili walitambulika kama Ponda na Mali.Hawa walizoea mbwembwe za wamayai.Waliishi kiuzungu uzungu hivi.walionekana kuwa watu waliosomea sheria sana maana mara nyingi walikua tayari kupambana na yeyote aliyetaka kumnyanganya maskini urithi.
Mimi nlilelewa kwenye ulingo wa kukimya bila kuziropoka hisia ama shida maana mwanadamu aisee si wa kueleweka wala kuaminika.Hakuna siku nliwaambia kuhusu yaliyonikuta nyumbani na nlikokua ninaelekea.
Usiku wa tarehe mosi agosti naukumbuka kama leo.Usiku ambao Mathlai shems aliamua kunielezea sababu yake ya kuishi na waume wawili aliowaita waume zake na hamna aliyeonea mwengine wivu.
Kijana keti nkupe uhondo na umbea wa maisha.Usiwe mjanja kwa maisha iwapo yanakulemea
Wapo waja wanaojaribu kupenda ili wapendwe na wapo waja wanaopendwa bila kupenda wala kulazimisha na hao waja ni baadhi wa waja wanaoishi duniani bila mpango wowote lakini Mola anawalisha na kuwatunza kama ndege wa angani.
Binti Mathlai alikua mmoja kati ya hawa waja wapole waliopendwa bila kulazimisha na hivyo akajinyakulia waume wawili walio lala na yeye kwa zamu na hakuna aliyemwonea mume mwenza wivu au kuonesha gere kwamba mimi nlikua nmeongezwa kwenye familia yao pana.
Paliondokea siku moja nikaamua kujua iwapo binti Mathlai aliyafurahia maisha haya ya kuwa na wanaume wawili."Mwanangu maisha haya ni matamu japo itakuja siku moja pepo mbaya litazuka baina ya waume zangu waanze kuoneana gere.siku hiyo ndipo nitalazimika kumchagua yule ninayempenda.Siku hiyo nitamchagua mtu tofauti kabisa.Mtu aliye mbali na wao ila roho yangu imwonapo yatuta na kupasa kama ngoma za kimakonde .
Naingoja siku hiyo maana nitakua huru kutoka kifungo hiki cha ndoa mbili tata.Wapo wanaotaka kuwa kama mimi.ila huwa nawakanya sana maana ndoa kama hizi si za kukimbilia."

Nlishangaa sana kuskia maarifa ya binti huyu.Kweli alikua ameenda kusoma kwa Waajemi na Warumi na ndiposa aliweza sana kuwakanganya waume wawili vijana wa masultani wakuu walioheshimika na kuwaponda roho na wao wakamponda mali.

Nami roho yangu ilianza kutamani siku nitakayo kua huru.Siku ambayo roho yangu itaruhusu nafsi yangu impende mwanamke nimchumbie na nipeleke posa kwa wazazi wake

Ipo Siku Where stories live. Discover now