Hapakaliki kamwe

44 3 0
                                    

Utulivu uliokuwemo chumbani ulianza kuwa kishindo.Nlianza Kuona mabadiliko yasiyo kifani.hamna aliyetaka kufanya kazi ili kumlisha mkewe tena.Chumbani hapakua pale nlipoingia wakati mmoja nkiwa mkosa kwao.

Binti Mathlai alibaki tu katwanga tabasamu lake kama ilivyo desturi yake na hamna aliyetaka kumuuliza lolote sababu hakutaka kujihusisha na ugomvi uliokuwamo chumbani.Wakati mwingi tulishinda pamoja chumbani ama Chini ya mnazi mkuu uliokuwa umemea uani.

Aliishi kunambia ipo siku.Ipo siku yote nitakayo maishani yatakubalika machoni pa mola na ipo siku nitaondoka kwenye kasri hili lisilo mmiliki.kasri lililojaa chuki na ugomvi mkuu baina ya watu waliomgombania mwanamke.mwanamke asiyeweza kuzalia yeyote maana yeye hajaamua kuuharibu ujana.Ama kweli ipo siku.

Mimi huku hakukunifaa tena.Nlianza kupanga mikakati ya kuhepa kasri hili la Shems na kujiunga na maskini wenzangu.Walala hoi wasiojua jumatatu wala ijumaa.wasiojua Sultani kachaguliwa lini na anaishi wapi.

walala hoi wasiojua Krisimasi au iddi.Haya ndiyo maisha yangu mimi.sikutaka kuozea kasrini bila la kufanya eti sababu nliokolewa na Mwenye kasri.Nlivipanga vibegi vyangu vya nguo na kuyapakia makasha ya vyakula aina aina kwenye vifuko vya mgomba.Nlibeba ngozi ya Ngombe iliyotengezwa rasmi ili kubeba maji ya kunywa safarini na Wenye kasri walipokua wakitazama muujiza wao waliouita televisheni nikaponyoka na kuteleza toka chumbani humo huku nkiacha ujumbe wa barua juu ya kitanda changu na kupotelea kwenye umati wa watu waliokua wakielekea jijini

Ipo Siku Tempat cerita menjadi hidup. Temukan sekarang