Uhusiano wangu naye ulishika kasi sana. Tukawa kama tumepagawa na pepo la Romeo na mpenziwe Juliet wahusika wakuu kwenye riwaya nliyokua naskia wasomi wakiisifia sana, Romeo and Juliet chake William Shakespeare mwandishi na mtunzi wa mashahiri yaliyotia fora sana.
Nlihamia kwake chumbani naye akawa mwenye furaha sana. Alinibadilisha nikawa msafi ukongwe uliokua umeanza kuninyemelea ukapotea nikarudi kuwa kitoto chenye ubwabwa. Waama bingwa Wallah bin Wallah mwandishi wa kiswahili mufti nlimeremeta na kumetameta.
Tangu kuzaliwa sikuwai muona mwanamke mpole mwenye hela na mali zake kama Halua. Nlishindwa katumwa na malaika yupi aje kunirehemu ila mie sikua na langu ila kumwombea dua jema kwa maulana. Nlipomaliza wiki mwezi mmoja alianza kunipa mafunzo ya udereva nami nlikua na kiu cha kujua ufundi huo kwa hivyo haikumchukua muda kabla niwe mraibu wa kuliendesha dinka
"Darling sasa wajua wafaa uanze kunipa mawaidha nataka uwe ukichangia kwa mambo na maendeleo ya humu chumbani, wajua wewe sasa ni zaidi ya mpenzi wangu na wafaa uache woga ulionao ili tuishi na raha" aliniambia usiku mmoja nlipokua natoka sebuleni kumruhusu afanye hesabu za hisa na mapato ya kazi yake.
Siku iliyofuata mrembo wangu alinirausha mapema haikua kawaida ila baada ya kunieleza nlichohitaji kufanya nilikimbia bafu na kujirashia maji bila kujali kama yalikua moto au baridi.Ilikua siku ya kuzaliwa kwake na wazazi wake walitarajiwa kufika wakati wowote. Baada ya kuoga nlijifunga taulo kiufundi kisha nikabaki humo bafuni nikiwaza yatakayojiri pindi shemeji zangu watakapowasili humu.
Je wangenikubali? Wangeniskiza? Yalinisonga maswali hayo ila sikua na budi.Nilijitoma chumbani na kumkuta tayari alikua amenichagulia mavazi nami bila wasiwasi nliyavaa na tukaelekezana wote sebuleni kula chamshakinywa.
Wazazi wake waliwasili saa tatu unusu na wakawa wananitazama sana tukiwa kwenye mlo. Wakati wa keki ndipo walipasua kimya na kuuliza kunihusu naye mpenzi wangu akawa na wakati mgumu kujaribu kueleza kunihusu. Walifikia suluhu kwamba sikufaa kuitwa mwanao na hivyo nlifaa kuondoka mle na kutokomea kwenye machokoraa wenzangu wakati ule bila kuondoka na chochote kule.
Nlijikokota kama punda aliyebebeshwa zigo la uzani ulomzidi nikafunganya viguo vyangu na kutokomea. Usiku huo ndio nlioamua kwamba nitakapopata hali sitakosa kuandika hadithi ya maisha yangu. Asubuhi iliyofuata nliamua kuhama na kuelekea mtaa mwingine ambako hapangekua na mtu wa kuniletea balaa
YOU ARE READING
Ipo Siku
HumorWosia wa babu yangu ukitimia naapa nitakua mtu asiye na kiburi.Naapa kutimiza yote aliyoninongonezea na ninaapa kuitunza aila yangu bila kiburi wala dharau. Maana natumai IPO SIKU.