Wapo wengi ambao walidhani niliporudi kwa Halua mambo yalikua shwari. Tulikaa raha mustarehe hadi tarehe ishirini na mbili mwezi wa pili mwaka huo. Siku hiyo nlitoka chumbani nikielekea kanisani kama ilivyokuwa desturi Halua alibaki nyumbani maana hakutaka mambo ya ulokole wangu
Nlipofika langoni nilipishana na janadume lenye uso mweupe na mwili wa miraba minne likiingia chumbani. Sikuwa na shauku nlienda zangu kanisani bila wasiwasi maana Halua alikua mfanyibiashara na wakati mwingi tulipokea wageni wa kila aina nyumbani.
Kanisani hapakua na mambo mengi hivyo kufikia saa sita tulikua tushamaliza misa ya siku nami nikapiga guu kurudi nyumbani. Lango lilikua wazi na hata mlango wa nyumba pia ulikua vivyo hivyo. Nlijitoma na kuketi sebuleni nkingoja malkia wangu aje anipe salamu na habari za siku.
Halua hakutokea kwa hivyo nikaamua kuingia chumbani nikabadilishe nianze shamra za kujiandalia maankuli. Nlichokutana nacho chumbani hadi leo chanipa jinamizi. Walikua kitandani wamelaliana uchi wa mnyama. Hawakuniskia nikiingia na hivyo nliondoka vile nlivyoingia. Nlitulia sebuleni kwa muda huku kichwa changu kimejaa mawazo
Sikuwai tarajia jambo kama hili lingewai nitendekea kwanza na mtu ambaye alijidai kunipenda. Aisee mkamia maji hayanywi nliondoka mle sebuleni na kuingia chumbani taratibu nikafunganya viguo vyangu nlivyokuja navyo kisha nikaazima kalamu yake ya wino wa kiarabu nikaandika kijibarua.
Halua mpenzi.Usijali mbona
Sikukuaga kwa njia
Inayofaa. Nimeondoka
Na niendako sijui ila
Najua mwenyezi mungu
Atanijalia nimpate kisura wa hadhi yangu
Mwenye mapenzi ya kweli na asiyetenda
Jambo kama hili ulilofanyaKwaheri Halua.
Baada ya kumaliza nlikiweka kijikaratasi hicho mezani mahali angekutana nacho na kutokomea jijini bila fujo. Nlitua Mwembetayari na kuanza kujitafutia makao maana huku nlijua hapangekuwa na shimo la taka wala chokoraa na ingebidi nitafute chumba cha kukodi.
Sijui kilichotendeka kule nyuma nlikotoka ila natumai alipoamka alipata barua yangu na kuisoma na akajua nishaondoka. Nilijiamulia uteule na kujitegemea na hivyo ndivyo nlivyopata kazi ya utarishi
YOU ARE READING
Ipo Siku
HumorWosia wa babu yangu ukitimia naapa nitakua mtu asiye na kiburi.Naapa kutimiza yote aliyoninongonezea na ninaapa kuitunza aila yangu bila kiburi wala dharau. Maana natumai IPO SIKU.