Episode 2

77 2 2
                                    

Inaendelea…..

Mkewe bwana Tadi, Bi. Mterehemezi, aliketi mkabala wa mumewe. Mkoba wake kaukumbatia vizuri kwapani.

“Jihadhari sana wakati utakapokuwa ukiongea na wanatakia.” Bi. Mterehemezi alimuanza mumewe. “Si kitu cha busara kuchochea watu dhidi ya wenzako. Kilicho muhimu ni kuuza sera zako na kisha kungoja uamuzi wao.”
Mara walishtukia wamefika uwanja wa Takia.

“Haya haya! Tunyanyuke wote wakati mheshimiwa Tadi anapofika uwanjani.” Sauti ya Fahama ilitangaza. Kaumu ya watu ukanyanyuka huku wakishangilia.

Tadi na mkewe walipita na kuketi mbele walipokuwa wametengewa viti. Naye Fahama akaendelea kusifia tajriba ya Tadi. Tadi naye wakati huo fikira zimemwambaa anajinadi kindanindani. “Lazima mwaka huu nipate. Nimejaribu sana lakini sipati. Sasa ninajua mbinu nitakazotumia. Ninayo maarifa, tajriba na ushawishi. Tazama umati huu wote…” Alijisifia nafsini. Alisita kufikiria ghafla aliposikia jina lake likitajwa na Fahama.

“Ni bora yeye mwenyewe atutajie mipango aliyo nayo ikiwa atapewa fursa. Karibu sana ndugu.” Fahama alipisha.

“Asante sana !” Alianza Tadi.”Si ajabu kuona umati kiasi hiki hapa. Ni kwa sababu mwanipenda. Mwapenda maendeleo na mimi ni ndiye kiongozi atakayeleta maendeleo kwenu. Mwapenda maono na mimi ninayo maono ya kuleta mabadiliko na kuimarisha maisha yenu. Au vipi?!”

“Ndiyoo!” Umati uliitikia.

“Ninavyosimama hivi ninayo mipango chungu tele ambayo pasi na shaka itakuwa ya manufaa kwetu sisi sote. Kura yenu ni ufunguo mwafaka kuafikia malengo haya. Sina budi kusema kuwa mkinipigia kura mtakuwa mumejipa takazo la nyoyo zenu.” Alisita kumtazama mkewe na kisha akaendelea.

“Mimi si kama wanasiasa wengine hapa wanaopiga kelele bila maono yoyote. Wao ni kama debe tupu ambao hauachi kutika. Naamini kuwa maono yangu ni bora na ninalenga kuleta mabadiliko makuu.”
Bwana Tadi aliendelea kujipigia debe kwa muda mrefu huku akijimiminia sifa sufufu!
Baada ya mkutano umati ulifumukana kisha Tadi na mkewe wakaendelea na mikutano yao mingine sehemu nyingine ya Takia.

Itaendelea….

VUTA N'KUVUTE Wo Geschichten leben. Entdecke jetzt