Inaendelea…
“Umejifanya sasa wajua siasa? Si basi ujiunge nao?” Tadi alipandwa na mafutu.
“Hata! Wajua kuwa hautaniruhusu. Lakini ningekuwa na uwezo wa kujinasua kutoka mtego huu wa kutawishwa nawe, ningeweza kuwa wa kusema na kufanya. Ila nyinyi mnadai sisi wanawake hatuna ujuzi wa kuongoza. Ati sisi ni vifaa vya kupika na kulea watoto. Hadi lini?”
“Nani kasema vile sasa?” Tadi alinywea.
“Nyinyi! Nyinyi mliotunga sheria na kuwapa wanawake nafasi finyu sana za uongozi. Nyinyi mnaosema wanawake hawana ujuzi wa kuongoza. Nadhani kama si sheria za kimataifa, nafasi zote hizo mngejilimbikizia.”
“Lo!” Alimaka Tadi. “Haya yote uliyajulia wapi?”
“Hahaha!” Mterehemezi alicheka kicheko yabisi. “Wadhani mimi ni bwege asiyejua lolote wala chochote?”
“Waanza kuuma ukivuvia eeh!” alionya Tadi.
“Nani? Mimi? Nyie zaidi. Mnatuuma miaka mitano uongozini kisha mnarudi kutupuliza na ahadi zisizotimizika.” Mterehemezi alihitimisha. Kimya kikajiri. Waama, uketo wa maji hupimika, uketo wa moyo wa mtu haupimiki. Tadi hakuamini aliyoyasikia kutoka kwa mkewe.
Itaendelea…
YOU ARE READING
VUTA N'KUVUTE
Mystery / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...