Inaendelea…
Aligutuka toka kwenye fikira pale Mtanzi alianza kuzungumza. Mtanzi alivuta pumzi na kisha kuyapanga maneno yake sawasawa kabla ya kuyazungumza kwa Mariko.
“Kongole kwa uamuzi huu wako wa kutaka kuiongoza Takia. Ni vizuri kuona watu wengi wakijitokeza kuwa viongozi. Nadhani ari hii inatokana na mema tuliyoyafanya na nyinyi mnataka kujiweka katika ramani hii ya wapenda maendeleo.” Alisimulia Mtanzi.
Mariko alitabasamu na kisha kumshukuru Mtanzi kwa maneno hayo. Mtanzi alipoona Mariko hana zaidi la kuongeza aliendelea.
“Kulingana na mambo yalivyo ni vyema pia kwa watu kuungana pamoja ili kazi iwe rahisi, si wajua tena umoja ni nguvu utengano ni udhaifu?”
“Naam.” Mariko aliiitikia.
“Aghalabu wale watu wanaoingia siasani kwa mara ya kwanza hujipata hawana wafuasi wengi.” Mtanzi aliendelea. “Hawajui kuwa kupata ufuasi si kazi rahisi. Lazima uwe na mbinu mwafaka za kuvutia umati mkubwa.”
“Wajaribu kumaanisha nini mheshimiwa?” Mariko alikosa subira.
“Kuwa wewe ni mgeni katika uwanda huu na unahitaji mtu wa kukushika mkono. Ili udumu katika nyanja kama hizi pia unahitaji tajriba. Nimefikiri sana kuhusu hili na madhumuni yangu kukualika hapa ni kuwa ningetaka tuungane pamoja. Najua fika kuwa tukiwa pamoja Tadi hatatuweza kamwe.”
Lo! Mariko hakuamini masikio yake. Hili lilimpata kama dhoruba kali. Akamtazama Mtanzi huku akijaribu kuhakiki kama Mtanzi anataka kuungana naye. Alichukua muda kufikiria na pia kujibu. Akakimya.
Itaendelea…
CZYTASZ
VUTA N'KUVUTE
Tajemnica / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...